Mbabe wa kamera upande wa simu ametoa matoleo mapya
Si mwingine bali ni Google Pixel 10
Google Pixel 10 unaweza kuiona kuwa haina tofauti na Pixel 9
Lakini haipo hivyo google pixel 10 ya 2025 imeboreshwa hasa upande wa utendaji
Hiki ni kipengele muhimu ambacho simu za Samsung na iPhone zimekuwa zikiipita Google mara nyingi
Hizi ndio simu tunazoenda kutazama
- Google Pixel 10
- Google Pixel 10 Pro
- Google Pixel 10 Pro XL
- Google Pixel 10 Pro Fold
Google Pixel 10
Google Pixel 10 ni simu ya kimo kifupi cha inchi 6.3
Bei yake ni shilingi milion 3.5 kwa hapa Tanzania
Kimo hiki kinafiti vizuri kwenye mkono hivyo ni rahisi kushika
Kioo chake ni cha OLED chenye refresh rate ya 120Hz na HDR10+
Teknolojia ya hdr10+ inaongeza kwenye skrini kina kikubwa cha rangi na hivyo kioo huonyesha vitu kwa ustadi
Betri ina mAh 4970 sio kubwa ukilinganisha na matoleo ya simu nyingi siku hizi
Inakuja na kamera tatu pamoja na RAM ya GB 8 na memori ya GB 128 au 256
Google Pixel 10 Pro
Bei ya Google Pixel 10 Pro ni shilingi milioni 4
Kimo chake ni inchi 6.3 kama ilivyo simu ya kwanza
Kioo chake kimeboreshwa zaidi kwa kuwekwa LTPO OLED
Inakuja na processor iliyoboreshwa zaidi ya Tensor G5
Betri ina ukubwa wa 4870mAh na chaji ya wati 30
Inakuja na kamera tatu za ukubwa wa 50MP kwa 48MP
Google Pixel 10 Pro XL
Google Pixel 10 Pro bei yake ni shilingi milioni 5.7
Inakuja na RAM ya GB 16 na prosesa ya Tensor G5
Pia inakuja na kamera zipatazo tatu
Betri yake ina ukubwa wa 5200mAh na chaji ya wati 45
Kioo chake ni cha LTPO OLED chenye HDR10+
Inakuja na Android 16 na itapata maboresho kwa miaka 7 mfululizo
Google Pixel 10 Pro Fold
Google Pixel 10 Pro Fold ni simu ya kujikunja
Yaani unaweza itumia kama simu ya kawaida na ukiikunjua inakuwa tablet
Upana wake ukiikunjua ni inchi 8
Betri yake ina ukubwa wa mAh 5015
Na pia ina kamera tatu
Na inatumia kioo cha Foldable LTPO OLED
Bei yake ni shilingi milioni 5.7 kwa hapa Tanzania