Katika baadhi ya nchi, Infinix walitoa toleo jipya la Infinix Note 50
Matoleo hayo ni
- Infinix Note 50 4G
- Infinix Note 50s
- Infinix Note 50 Pro 4G
- Infinix Note 50 Pro+ 4G
- Infinix Note 50 Pro+
Na kwa Tanzania simu hizi zinaweza kuja kuzinduliwa muda si mrefu
Kwani hizi zilitangazwa mnamo mwezi machi 2025
Sio mbaya tukapitia sifa za muhimu na ubora uliopo kwenye kila infinix mpya
Infinix Note 50 4G
Infinix Note 50 4G ni infinix ya kamera mbili ambapo kamera kubwa ina megapixel 50 na pia ina OIS
Utendaji wake ni wa wastani kutokana na kutumia chip ya Mediatek Helio G100 Ultimate
Betri yake ina ukubwa wa 5200mAh ambayo inahifadhi umeme mwingi
Hii simu inasapoti chaji inayopeleka umeme mwingi wa wati 45
Hivyo betri haitochukua muda mrefu kujaa
Itapata matoleo mapya ya android kwa muda wa miaka miwili yaani itapokea Android 17
Infinix Note 50s
Infinix Note 50s inakuja na kamera mbili kubwa ikiwa na megapixel 60 yenye uwezo wa kurekodi video za 4K
Inasapoti mtandao wa 5G, na utendaji wa simu unaweza kufanya vitu vingi vikubwa
Kwani inatumia chip yenye utendaji mkubwa ya Dimensity 7300 Ultimate
Pia chaji yake inakubali umeme wa wati 45
Upande wa software inatumia Android 15 na itapokea matoleo mengine kwa miaka miwili mfululizo
Infinix Note 50 Pro 4G
Infinix Note 50 Pro 4G ina kamera mbili tu kubwa ikiwa na megapixel 50
Utendaji wake ni wa wastani kutokana na kutumia processor ya Mediatek G100 Ultimate
Na yenyewe itapata matoleo mapya ya android kwa miaka miwili mfululizo
Upande wa chaji simu inakuja na chaji yenye kasi kubwa
Kwani inasapoti chaji ya wati 90, ambapo simu haitochukua dakika nyingi kujaa
Pia ukubwa wa betri yake ni 5200mAh
Infinix Note 50 Pro+
Katika orodha ya matoleo mapya ya Infinix kwa 2025, hii ndio simu bora zaidi
Inakuja na processor yenye nguvu kubwa kiutendaji
Na ina kamera tatu ambapo kamera zina megapixel 50 na nyingine ina megapixel 8
Chaji yake inasapoti umeme wa wati 100
Ambao unaweza kujaza simu kwa dakika 30 tu
Betri ni kubwa pia kwani ukubwa wake ni 5200mAh