Mwezi wa Januari kampuni ya Samsung ilitangaza ujio wa matoleo matatu mapya ya Samsung Galaxy S25
Matoleo ya Samsung Galaxy S25 ni ya daraja la juu hivyo ubora na bei huwa mkubwa
Mbali matoleo ya S-series, mwishoni mwa 2024 kuna matoleo ya daraja la kati na la mwisho yalitoka
Hii ni orodha ya samsung mpya na bei zake kwa mwaka 2025.
Samsung Galaxy S25 Ultra – milioni 3.5
Samsung Galaxy S25 Ultra ndio samsung yenye ubora zaidi kuliko samsung zote kwa sasa
Hii ni bei ya ukubwa wa GB 512
Utendaji wake ni mkubwa na inaambatana na mifumo yenye AI usahihi mkubwa katika kufanikisha jambo fulani
Processor yake ni mpya na ni aina ya Snapdragon 8 Elite 3
Ina kamera nne ambazo lenzi zake ni wide, ultrawide, telephoto na periscope telephoto
Betri yake ina ukubwa wa 5000mAh na chaji yake inapeleka umeme wa wati 45 ambayo inachaji simu kwa haraka
Samsung Galaxy S25+ – milioni 2.8
Samsung Galaxy S25+ upande wa software na hardware zinafanana toleo la Ultra
Isipokuwa upande wa betri na kamera
Maana S25 Ultra kamera yake kubwa ina megapixel 200 ambapo Samsung Galaxy S25 Plus ina 50MP
Kioo chake kina kina kikubwa cha rangi kwa sababu ya uwepo wa HDR10+
Na yenyewe inatumia processor ya Snapdragon 8 Elite 3 ambayo nguvu ya utendaji ni kubwa
Samsung Galaxy 25 – milioni 2.3
Hii ni samsung ya kamera tatu
Upande wa kimo hii simu ni fupi ukilinganisha na samsung zingine
Urefu wake ni inchi 6.1
Na hata betri yake lina ukubwa wa 4000mAh
Hivyo ukaaji wake wa chaji hautokuwa mkubwa kama Samsung Galaxy S25 Plus au Ultra
Na kama ilivyo kwa samsung zingine za mwaka 2025, na yenyewe itakuwa inapokea android mpya kwa miaka 7
Samsung Galaxy A06 5G – laki 3.5
Hii ni samsung inayotokana na Samsung Galaxy A06 ambayo ni ya daraja la chini
Utofauti mkubwa uliopo ni uwepo wa mtandao wa 5G
Utendaji wake ni wa wastani kwa sababu inatumia processor ya Mediatek Dimensity 6300
Galaxy A06 ina kamera mbili ila kiuhalisia kamera yake ni moja tu
Betri yake ni kubwa(5000mAh) kasi ya kuchaji ni wati 25
Samsung Galaxy Z Fold Special – milioni 5.2
Hii ni simu ya kujikunja ambayo ilitoka mwishoni mwa 2024
Ukiikunjua upana wake unakuwa inchi 8
Ndio simu ya Samsung yenye bei kubwa kupititliza
Utendaji ni mkubwa a wenye nguvu kwani chip yake ni Snapdragon 8 Gen 3
Na ina kamera tatu huku kamera kubwa ikiwa na megapixel 200
Pia itakuwa inapokea updates kwa miaka saba
Samsung Galaxy A16 – laki 4
Samsung Galaxy A16 ni simu ya daraja la kati iliyotoka mwezi novemba 2024
Simu ina kamera tatu aina ya wide, ultrawide na macro
Ukubwa wa betri ni 5000mAh, na kasi ya juu ya kuchaji ni wati 25
Ina kioo cha super amoled chenye refresh rate ya 90Hz
La kufurahisha zaidi ni kuwa itakuwa inapokea matoleo mapya ya android kwa miaka 6
Ni nadra kukuta simu za laki nne kupata huduma kwa kipindi cha muda mrefu
Samsung Galaxy A16 5G – laki 5
Hii ni simu nyingine ya daraja inayosapoti mtandao wa 5G
Kama ilivyo mtangulizi wake na yenyewe itakuwa inapata toleo jipya la android kwa miaka sita
Hii simu ina waterproof aina ya IP54
Yaani inaweza kuzuia maji ya kiwango cha kunyunyulizika
Mfano wa mvua za manyunyu
Na yenyewe pia ina kioo cha super amoled chenye refresh rate ya 90Hz
Samsung Galaxy S24 FE – milioni 1.2
Unataka samsung galaxy s24 ya bei nafuu?
Basi Samsung Galaxy S24 FE ndio mbadala sahihi
Hautopata mambo yote ya Samsung Galaxy S24 ila kwa sehemu kubwa utaweza kupata hivyo vitu
Mfano kuwa na kamera inayoweza kurekodi video za 8K
Mng’ao wa video za 8K ni mkubwa na picha huonekana “clear” sana