SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Bei ya Samsung Galaxy A06 na Ubora wake

Sifa za simu

Sihaba Mikole

October 7, 2024

Samsung Galaxy A06 ina betri inayokaa na chaji muda mrefu na ni simu ya daraja la chini

Hii inamaanisha watu wengi kwa hapa Tanzania wanaweza inunua

Kwa sababu bei ya samsung galaxy A06 ni shilingi laki tatu na nusu (350,000)

Ni bei itakayokupa Galaxy A06 ya ukubwa wa GB 128 na RAM ya GB 4

Hakuna tofauti kubwa sana na toleo lilopita la Samsung Galaxy A05

Ila kuna tofauti ndogo upande wa software na utendaji

Sifa za Samsung Galaxy A06

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
  • CPU – Mediatek Helio G85
  • Core Zenye nguvu(2) – 2×2.0 GHz Cortex-A75
  • Core Za kawaida(6) – 6×1.8 GHz Cortex-A55
  • GPU-Mali-G52 MC2
Display(Kioo) IPS LCD
Softawre
  • Android 14
  • One UI 6.1
Memori eMMC 5.1, 128GB,64GB, na RAM 6GB,4GB
Kamera Kamera MBILI

  1. 50MP,PDAF(wide)
  2. 2MP(Macro)
Muundo Urefu-6.7inchi
Chaji na Betri
  • 5000mAh-Li-Po
  • Chaji-25W (haiji na chaji)
Bei ya simu(TSH) 350,000/=

Uwezo wa network

Samsung Galaxy A06 ni simu ya laini mbili na haisapoti eSIM

Inakubali mtandao wa 4G na haina uwezo wa 5G

Ukizingatia aina ya bei na wateja lengwa inaondoa ulazima wa uwepo wa 5G

Simu inasapoti masafa yote yanayotumiwa na mitandao ya simu nchini

Hivyo hakuna laini itakayoshindwa kusoma

Kama ikiwa hivyo basi utakuwa umenunua simu mbovu na huna budi kuirudisha

Kasi ya 4G ni kubwa kwenye hii simu kama utapata mtandao wenye nguvu madhubuti

Ubora wa kioo cha Samsung Galaxy A06

Hakuna maajabu kwenye ubora kioo cha Samsung Galaxy A06

Kwani refresh rate ipo ya kawaida ya 60Hz

Wakati huo simu mpya Tecno Spark 30C ina refresh rate inayofika 120Hz

Pitia hapa kuifahamu, simu ya tecno spark 30C kiundani

Pia kioo chake kina resolution ndogo ya HD+ na sio full hd

Uangavu wake ni wastani kutokana na kuwa na nits 500

Kwa maana kama ukiwa juani uangavu hautokuwa mkubwa sana

Nguvu ya processor Mediatek Helio G85

Utendaji wa Mediatek Helio G85 sio mkubwa ukilinganisha na chip ya Dimensity 6500

Lakini bado utaweza fanya vitu vingi japo sio kwa ubora mkubwa sana

Kwa mfano kwenye magemu ili ucheze vizuri itakulazimu kuweka settings za chini

Na pia helio g85 haitoweza ku-push fremu nyingi(60fps) ukiwa unacheza gemu

Fremu zikiwa nyingi muonekano wa gemu unakuwa mzuri kama vile unaangalia video

Lakini hii inasababishwa na chip kuwa na muundo wa zamani wa Cortex A75 kwenye core zenye nguvu kubwa

Uwezo wa betri na chaji

Betri ya hii simu ina ukubwa wa 5000mAh

Ukifungua box utakutana na waya wa kuchaji bila kichwa chaji

Yaani kama hauna chaji utalazimika kununua chaji yake

Uwezo wa kuchaji inakubali mpaka wati 25

Na inachukua dakika 90 kujaa kwa asilimia 100 kutoka zero

Ukaaji wa chaji ni wa kuridhisha sana

Kwa matumizi ya hapa na pale unaweza ukaitumia mpaka masaa 13

Na ukiwa unaperuzi intaneti muda wote simu inachukua masaa 12 mpaka chaji kuisha

Ukubwa na aina ya memori

Kuna matoleo mawili tu upande wa memori ambazo ni GB 64 na GB 128

Na RAM pia zimegawanyika katika sehemu mbili ambazo ni 4GB na 6GB

Kwa bahati mbaya mfumo wa memori wa hii simu sio ule wa UFS bali ni eMMC

eMMC haina kasi kubwa kama mifumo ya UFS na kiukweli simu nyingi siku hizi zimeacha kuweka mifumo eMMC

Ni eneo ambalo samsung hawakutenda haki kwenye hii simu

Uimara wa bodi ya Samsung Galaxy A06

Bodi ya Samsung Galaxy A06 ni ya plastiki kwa pande isipokuwa mbele kwenuye skrini ndio kuna glasi

Hii simu haijainishwa kuwa na viwango vya IP

Hivyo hakuna waterproof ya haina yoyote

Umakini lazima uzingatiwe unapokuwa kwenye mazingira ya mvua ama kwenye maji

Kiujumla simu inahitaji ulinzi wa ziada maana hii sio samsung galaxy s24

Ubora wa kamera

Ina jumla ya kamera mbili upande wa nyuma

Aina za zinazopatikana kwenye Samsung A06 ni wide na macro kwa ajili ya kupiga vitu vya karibu sana

Kuhusu ubora wa picha simu inapiga picha vizuri

Na ushahihi wa rangi hata kwa watu wenye ngozi nyeusi ni mkubwa

Haimg’arishi mtu kiasi cha kuondoa uhalisia mtu

Changamoto ukiwa unapiga mazingira yanayopokea mwanga mwingi wa jua usahihi wa rangi hupungua

Ubora wa Software

Kwenye upande wa software samsung wana mfumo mzuri sana unaoitwa One UI 6.1

Na hii simu ndio mfumo unaotumia pamoja na mfumo endeshi wa Android 14

One UI 6.1 imetumika pia kwenye samsung za mdaraja ya juu yaani Samsung Galaxy S24

Lakini hautopata vitu vyote vinavyopatikana kwenye Samsung Galaxy S24

Hata utaweza kupokea matoleo mapya ya Android kwa kipindi cha miaka miwili

Hii ikiwa na maana utapata Android 15 na Android 16

Maboresho ya namna yanakuhakikishia kupata maboresho mbalimbali yanayoambatana na android mpya

Washindani wa Samsung Galaxy A06

Kwenye hiki kipengele kuna washindani wengi wengi hasa toka kwa kampuni za China

Tecno wana simu mpya za Tecno Spark 30, na mojawapo inauzwa kwa bei ya chini ya hii

Kuna toleo la Realme C55, ni la mwaka 2023 ila utendaji wake ni mkubwa zaidi

Haitoshi pia kuna ujio wa simu ya Redmi 14C itakayotoka muda wowote

Kiumla machaguo yako mengi yanayoleta ushindani kwa hii samsung

Neno la Mwisho

Samsung Galaxy A06 imeongeza kitu kimoja kikubwa sana ukilinganisha na matoleo mengi ya daraja la chini

Kitendo cha kuzipa simu maboresho kwa kipindi kwa miaka miwili sio jambo ndogo

Kiuhalisia watumiaji wengi wa simu ndogo huwa hawapati maboresho mapya ya android baada ya kununua

Hivyo bei ya samsung galaxy 06 inaendana na thamani yake

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

No Featured Image

Bei ya Tecno Spark 30C na Sifa Zake Muhimu

Tecno wameleta toleo jipya la simu ya madaraja ya chini yenye maboresho Ina maboresho upande wa skrini(kioo) kuwa na refresh rate kubwa ambayo mara hupatikana kwenye simu za daraja la […]

thumbnail

[VIDEO]:Simu zote za iPhone za bei ndogo na zinazofaa

Kabla ya kununua iphone za bei rahisi ambazo mara nyingi huwa ni used, kitu cha kwanza cha kuangalia ni kama itakuwa inapata sapoti ya kupokea mfumo endeshi wa iOS Tofauti […]

[VIDEO]: Simu bora duniani na bei zake 2024

Huu ni muendelezo mwingine wa simu tano ambazo hazitumikii sana na watanzania. Lakini kiulimwengu ni kati ya simu bora duniani kwa mwaka 2024. Hizi ni simu zenye utendaji mkubwa kwenye […]

Simu bora duniani na bei zake 2024

Leo tuzungumzie kuhusu simu bora duniani na bei zake kwa mwaka 2024 Kuna matoleo mapya ya simu kali yenye ubora wa kiutendaji na wenye nguvu madhubuti katika maeneo mengi Ubora […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani
TUFUATE
Youtube Facebook Instagram twitter

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company