Tangu kuanza kwa mwaka 2024 kampuni ya Infinix zimeingiza sokoni takribani simu nane
Katika mrorongo wa simu mpya za infinix na tecno yapo matoleo ya daraja la chini na daraja la kati
Kwa maana kuna tecno na infinix za kuanzia laki mbili mpaka milioni
Kikubwa inategemea na aina ya sifa na ubora wa simu husika
Ukifuatilia simu za daraja la kati utaona kuna tofauti kubwa kati ya infinix za bei nafuu na za bei kubwa
Infinix Note 40 Pro+
Bei ya Infinix Note 40 Pro+: 900,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM: 8GB
Infinix Note 40 Pro+ ni simu ambayo imeingia sokoni mwezi machi
Utendaji una nguvu kwani inatumia processor ya Mediatek Dimensity 7020
Kioo chake ni cha aina ya super amoled chenye resolution ya 1080 x 2436 pixels
Kamera yake ina ukubwa wa megapixel 108 lakini hairekodi resolution kubwa zenye kufika 4K
Chaji yake ina kasi sana inapeleka wati 100 hivyo betri yake ya ukubwa wa 5000mAh inajaa ndani ya nusu saa
Infinix Note 40 Pro
Bei ya Infinix Note 40 Pro: 875,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM: 8GB
Infinix Note 40 Pro haitofautiani sana na Pro Plus
Tofauti kubwa utaipata kwenye kasi ya chaji
Ambapo kasi ya Infinix Note 40 Pro+ inapeleka umeme wa kiwango cha wati 100 wakati pro tupu ni 45
Mambo mengine yanaendana, yaani ukichukua hii na iliyotangulia hutoona utofauti mkubwa
Infinix GT 20 Pro
Bei ya Infinix GT 20 Pro: 750,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM: 8GB
Infinix GT 20 Pro imetoka rasmi mwezi April
GT 20 Pro ina vipengele vichache ambavyo vimeiacha kwa kiasi kikubwa simu za matoleo ya Note
Kwa mfano Infinix GT 20 Pro inatumia processor yenye nguvu zaidi ya Dimensity 8200
Kioo chake cha amoled kina refresh rate ya 144Hz yaani kama skrini za kompyuta za magemu
Chaji yake inapeleka umeme mwingi kiasi wa wati 45
Hivyo inawahi kujaza betri kwa dakika chahche
Infinix Note 40
Bei ya Infinix Note 40: 550,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM: 8GB
Infinix Note 40 na yenyewe imetoka mwezi machi mwaka huu
Nguvu ya kiutendaji ni ya wastani ila inaweza kufanya mambo mengi
Kamera zake tatu zinafanana na matoleo mengine ya note za infinix
Ina betri kubwa ya 5000mAh inatuza chaji
Na pia chaji yake ina kasi ya wati 45
Utendaji wake na wenye si mkubwa ni wa wastani kwani inatumia chip ya Mediatek Helio G99
Infinix Smart 8 Plus
Bei ya Smart 8 Plus: 280,000/= ,Ukubwa wa Memori: 64GB, RAM: 4GB
Infinix Smart 8 Plus ni simu ya daraja la chini ambayo imetoka mwezi februari
Haina utendaji mkubwa kwa sababu inalenga utendaji wa kwenye vitu vya msingi zaidi
Kwa maana kama unatumia muda mwingi kwa shughuli ndogo ndogo basi jua kwamba hii ni simu nzuri ya bajeti ndogo
Ila ukiwa unapenda sana gemu na mtu wa kamera jua kuwa hii haitokufaa kabisa
Kwani inatumia chip ya nguvu ndogo ya Mediatek Helio G33
Infinix Smart 8 Pro
Bei ya Smart 8 Pro: 280,000/= ,Ukubwa wa Memori: 64GB, RAM: 4GB
Simu ya Infinix Smart 8 Pro ilitoka rasmi mwezi februari ikiambana na infinix smart 8 plus
Na yenyewe ni simu ya daraja la chini hivyo bajeti yake sio kubwa
Hata hivyo inafaa kwa mtumiaji mwenye matumizi machache ya kawaida
Kioo chake ni cha IPS LCD sio amoled kama ilivyo kwa simu za daraja la kati za miaka hii
Betri yake ni kubwa lakini nchaji inapeleka umeme wa wati 10
Hivyo betri itajaa baada ya muda mrefu kwa takribani masaa matatu
Infinix Smart 8 HD
Bei ya Smart 8 HD: 240,000/= ,Ukubwa wa Memori: 64GB, RAM: 4GB
Infinix Smart 8 inatumia processor ya Mediatek Helio G36
Na imetoka mwezi desemba mwaka 2023
Kwa muhitaji wa simu za laki mbili na chini ya laki tatu, hii ni simu inayoweza kumfaa
Lakini weka akilini kuwa ubora wake sio mkubwa
Ni simu nzuri kwa matumizi ya kawaida
Maoni 14 kuhusu “Simu mpya za Infinix (Matoleo ya 2024)”
Hii ndo websites bora kwangu ya mda wote mnatoa taalifa za uhakika kweli
Kati ya infinix hot 20 na infnix hot 20i ip bora
Hot 20 ni nzuri zaidi
Mbona Infinix note 40 madukani ni 600000
Infinix wanatoa matoleo lakin karibu yote hayatofautiani
nawakubali sana, vp nikihitaji simu nipo mkoani inaweza kunifikia? na ni utaratibu gani unatumika mpaka napata simu nikiwa mkoani?
Infinix gt 20 pro kwani imefika hapa nchini kwetu.
Infinix Note 40 naweza kuipta mkoani jibu sms zetu tafadhari
Mkoa gani
Mkoa was ruvuma infnix note 40 zinapatikana?
Ndio inawezekana
Daaaa gali san
Mbona Yangu ni Infinix Smart 8 Gb64 Ram 3 hii ni Daraja gani? Na Nikiingia Setting>Special function (Action and gesture Siipati) Nahitaj msaada Zaid Make natake ile System Ya “Double Tapp On/Off Screen”
Daraja la chini