Apple iPhone 15 Pro Max ni simu yenye kamera tatu upande wa mbele na kamera moja ya mbele (selfie kamera)
Ukifuatilia ubora wake wa kamera utagundua sababu ya kuuzwa bei kubwa
Kamera zake zinatoa picha nzuri kwenye mwanga mwingi na pia kwenye mwanga mdogo vitu vinatokea na kuonekana kwa uzuri
Kwenye hii post tutaangazia kinaga ubara wa kamera ya iphone 15 pro max katika kupiga picha na kurekodi video
Hii tathmini imetokana picha mbalimbali watu walizopiga na tathmini nyingine za wataalamu
Kwanza inabidi ujue kila kamera na sifa zake
Kamera kuu(main camera)
Hizi ni baadhi ya sifa za kamera kubwa ya iphone 15 pro max katika vipengele muhimu
Resolution: Megapixel 48
Aperture(Uwazi wa kupitisha mwanga): f/1.8
Ukubwa wa pixel: 1.22µm
Ulengaji: dual pixel PDAF
Optical Image Stabilization(OIS): ipo
Ukubwa wa sensa ya kamera: 1/1.28 inchi
Kwa sifa zilizoorodheshwa zinaashiria uwezo wa kamera kuwa na vigezo stahiki kupiga picha na kurekodi video katika ubora stahiki
Kiwango cha ukiubwa wa pixel ambayo ni 1.22µm kinaipa nafasi kamera kukusanya mwanga mwingi
Pixel zikiwa ndogo sana hufanya simu kuwa na wakati mgumu kupiga picha vizuri
Kamera ya Ultrawide
Hii ni kamera maalumu kwa ajili ya kupiga picha ama kurekodi video eneo kwa upana mkubwa wa ziada
Ndio maana inaitwa kamera ya ultrawide
Tuchukulie upo kwenye mkutano wa hadhara na unataka kuchukua picha ya watu wengi kwenye uwanja kuonekana
Basi kamera ya ultrawide ndio inayofaa kutumika kwenye mazingira kama hayo
Hizi ni sifa za ultrawide ya iPhone 15 Pro Max.
Resolution:Megapixel 12
Aperture(Uwazi wa kupitisha mwanga): f/2.2
Ukubwa wa pixel: 1.4µm
Ulengaji: dual pixel PDAF
Optical Image Stabilization(OIS): ipo
Ukubwa wa sensa ya kamera: 1/2.55 inchi
Kamera hii ubora wake ni mzuri ila sio kama kamera ya kubwa
Lenzi(sensa) yake ni ndogo yenye inchi 1/2.55 inchi
Hata hivyo sifa zake bado zinaweza kupiga picha yenye ubora mkubwa
Kamera ya Telephoto
Resolution:Megapixel 12
Aperture(Uwazi wa kupitisha mwanga): f/2.8
Ukubwa wa pixel: 1.12µm
Ulengaji: dual pixel PDAF
Optical Image Stabilization(OIS): ipo
Zoom:5x optical zoom
Ukubwa wa sensa ya kamera: 1/3.06 inchi
Kamera ya telephoto hutumika kupiga kitu ambacho kipo umbali mrefu kutoka simu inapopiga picha
Kiasi cha kwamba ukitumia kamera ya kawaida mtu anaiweza aisonekane vizuri
Lakini telephoto tena yenye optical zoom(zoom inayotumia lenzi na sio app ya simu) inasaidia kukinasa kitu ambacho kipo mbali bila kupunguza ubora wa simu
Mpaka sasa simu yenye telephoto nzuri zaidi ni Samsung Galaxy S23 Ultra
Ubora wa picha wa kila kamera
Kwenye hiki kipengele tutaangazia ubora wa picha nyakati za mchana yaani kwenye mwanga mwingi na nyakati za usiku ambapo kuna mwanga mdogo
Kitu kikubwa tunachokitazamia ni usahihi wa rangi, kiwango cha noise(chengachenga) na uimara wa kutofautisha rangi kwenye mwanga hafifu na mwanga mwingi bila kusahau muonekano wa vitu pindi picha ikikuzwa
Kamera kuu(mwanga mwingi)
Wakati wa mchana ambapo kuna mwanga mwingi kamera inachukua picha vizuri bila kupoteza usahihi wa rangi
Vitu vinavyoonekana kwenye eneo huonekana kwa usahihi wake wa rangi kwa kiwango kikubwa
Ukiikuza(kuzoom) picha kwa ajili ya kuona vitu vingine kiundani bado utaweza kuona hata kama maandishi ambayo yapo mbali
Moja ya kitu unachoweza kukipata kutoka kwenye hii picha ni kuwa kamera kamera kuu inahitaji vitu visiwe mbali sana na kamera
Kadri kinachopigwa picha kinapokuwa kuna kiwango cha noise(chengachenga) kinajitokeza
Hili unaweza kuliona kwa kutazama muonekano wa kamera
Kwenye mwanga mdogo
Wakati wa usiku ambapo ndipo kuna mwanga hafifu kamera kuu inapiga kwa ustadi bila kuwa na kiwango cha noise cha aina yoyote
Lakini kwa vitu ambavyo vipo apando wa pembeni wa kitu kinacholengwa hasa kikiwa mbali inakuwa ngumu hata kutambua rangi
Kwa kitu ambacho kimelengwa ubora wa picha ni mzuri
Ukiangalia rangi za vitu haziathiriwi na kiwango kikubwa cha giza usiku
Kila kinaweza kuonekana na kutambulika kwa usahihi
Ukitazama picha za magari na picha hilo jengo la ghorofa, rangi za vitu zinaweza tambulika na kutofautisha
Hii ina maana kamera inajitahidi kwa kiasi kikubwa katika utofautishaji wa rangi
Ila sasa ukiangalia upande wa kushoto mwa jengo kuna sehemu ina giza kubwa kiasi cha kwamba ni ngumu kujua kitu kilichopo
Maana yake utofautishaji wa rangi ni changamoto mwanga ukiwa mdogo zaidi
Njia apple wameitumia kutatua tatizo ni kuwa na chagua la kuseti Night Mode, hii inafanya picha isiwe na noise hata kidogo kwa kitu kinacholengwa na vile ambavyo vipo pembeni
Hii ni setting ya nighy mode inavyosaidia kuonyesha kila kitu kwa usahihi mkubwa
Ultrawide(mwanga mwingi)
Kwa kulinganisha ubora wa picha kati ya kamera kuu na ultrawide , ultrawide ipo nyuma kidogo
Hata hivyo vitu vinaonekana hata kama ukiikuza picha na kuwa kubwa
Utaona kiwango cha chengechenga kuwa kidogo
Utofautishaji wa rangi kwenye kamera hii una usahihi unaoridhisha hasa nyakati za mchana
Kama picha jinsi unavyoonyesha, kamera imeweza kunasa eneo pana wakati huo unaweza muonekano wa kila kilichopo kwa uzuei
Rangi za majani, maji, majengo na mawingu zina muonekano halisi
Hata kwa vitu ambavyo vipo pembeni hakuna meonekano wa chengachenga hata kidogo
Changamoto ya noises ipo kwa kiasi nyakati za usiku
Si kila kilichopo kwenye eneo pana kitaonekana kwa uzuri kama picha zilizopigwa
Telephoto(mwanga hafifu)
Kikawaida simu ambayo haitumii optical sensor kuzoom kitu cha mbali mara nyingi hupoteza ubora wa picha
iPhone 15 Pro Max kamera yake ina optical sensor inayoweza kunasa picha kwa kitu ambacho kipo mbali kwa kukuza mara tano kama kiwango cha juu
Ukilinganisha na samsung galaxy s23 ultra, samsung iko vizuri sana kwenye eneo hili
Kwenye mwanga mwingi hasa nyakati za mchana kamera ya telephoto inachukua picha vizuri
Na picha zinakuwa na muonekano usiopoteza ubora hata ukiizoom picha mara tano unapotumia hii kamera
Hii ni picha iliyochukuliwa na kamera ya telephoto kabla ya kuzoom(kuikuza)
Chukulia unataka kuliona bati kwa ukaribu kitu kitachokulazimisha kuikuza(kuzoom) kamera mara tano
Hii ndio picha iliyochukuliwa baada ya kuzoom
Je kuna upungufu wa ubora kwa kutazama muonekano wa awali na wa muonekano baada ya kukuzwa?
Ubora wa video
iPhone 15 Pro Max inaweza kurekodi mpaka video za 4K kwa kiwango cha fremu 60 kwa sekunde
Kamera kuu na kamera ya telephoto zina OIS ambapo kazi yake kubwa ni kutuliza video wakati wa kurekodi
Wakati unarekodi video huku ukiwa unatembea, iphone haitikisiki kwa kiwango kikubwa
Iko “stable” na nzuri kwa wanaopenda kurekodi video za selfie
Kiujumla video zake ziko safi kwa nyakati zote yaani usiku(kwenye mwanga hafifu) na kwenye mwanga mwingi
Hitimisho
iPhone 15 Pro Max ni moja ya simu nzuri zenye kamera nzuri
Kwa kiasi kikubwa kamera zake zinanasa picha nzuri japo si kwa mazingira yote simu itachukua kwa uzuri
Maana kwenye mwanga hafifu sana tegemea kiasi kidogo cha noises ama baadhi ya vitu kutoonekana kwa uzuri
Maoni 2 kuhusu “Ubora wa iPhone 15 Pro Max Upande wa Kamera[hatari tupu]”
MA.COMPANY MENGI YA SIM YAMETOWA SIM MYPA JE NI SIM GANI YENYE CAMERA NZURI KWASASA…?? NAITAJI NIJUE
Samsung s24, iPhone 15, Vivo x90, oppo find x6 pro. Hizi ni simu za bei kibwa