Jibu jepesi, simu za iphone zote ni nzuri.
Kwa nin?
Apple imejikita zaidi kuunda simu za gharama na hadhi ya juu
Hivyo wanajitahidi kwa kila namna kutengeneza smartphone yenye vitu vingi vizuri.
Ubora wa simu za iphone unatofautiana.
Tangu 2018 mpaka 2022 kuna matolea zaidi ya 11 ya iphone ambayo bado yapo sokoni pia.
Kwa wakati uliopo si kila simu ya iphone inafaa.
Hapa kuna orodha ya simu nzuri za iphone ambazo zinaweza kushindana na matoleo ya simu kutoka brand zingine za mwaka 2022.
Hizi ni iPhone ambazo zinapokea update za IOS kila mara kwa maana zinakubali apps zote.
Hizi ni baadhi.
Ni vizuri kuelewa ubora wa kila iphone kwa kuangazia sifa za simu husika.
iPhone 11
Simu ya iphone 11 inatumia processor yenye uwezo mkubwa kiutendaji aina ya Apple Bionic A13.
Procesor ya bionic A13 ina modem inayosapoti mtandao wa 4g hivyo simu haina 5g.
Bionic A13 inaweza kufanya kazi kubwa kuliko processor mpya zenye 5G ambazo zimetoka 2020-2021.
Processor ya Dimensity 810 inazidiwa zaidi ya mara na Bionic A13.
Hii inamaanisha iPhone ya mwaka 2019 inaizidi mbali Redmi note 11(china) ya mwaka 2021
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Liquid Retina IPS LCD |
Softawre |
|
Memori | NVMe, 64GB,128GB,256GB na RAM 4GB |
Kamera | Kamera mbili
|
Muundo | Urefu-6.1inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 1,039,500/= |
Kioo chake sio cha Super Retina Oled ambacho kinaonyesha vitu kwa uharisia kuliko IPS LCD.
IPS LCD za apple hufahamika kama Liquid Retina.
Simu hii inatumia iOS 13 ila inaweza kupokea iOS 15.3 ambayo ni mpya.
Mfumo wake wa memori ni tofauti na mifumo wa UFS unaotumiwa na simu za android.
NVMe ni mfumo unaotumika kwenye iPhone una kasi kubwa ya kuhifadhi vitu kuliko UFS.
Kuna aina tatu za iphone 11 upande wa memori kama jedwari linavyoonesha.
Betri yake aina ya Li-Ion ni dogo na mfumo wa chaji wake 18W unajaza betri kwa haraka.
Simu si ndefu ni fupi upande wa kimo.
Simu ina kamera mbili upande wa nyuma, zote zina megapixel 12.
Mfumo wa kamera una OIS na dual pixel PDAF.
OIS hutuliza video wakati ikichukuliwa huku mchukuaji video akiwa anatembea.
Dual pixel PDAF hufanya kamera kurenga kitu kinachopigwa kwa usahihi hivyo kutokea vizuri
Pamoja na kuwa kamera zake zinakosa optical zoom bado iphone ina kamera nzuri.
Kamera ambazo zinaweza kurekodi video za 4K
iPhone 11 Pro
Simu ya iphone 11 pro ni toleo moja na iphone 11.
Utofauti wa simu hizi mbili upo katika pande zifuatazao.
- Kimo
- Ujazo wa betri
- Kioo(Display)
- Memori
- Bei
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Super Retina XDR OLED |
Softawre |
|
Memori | NVMe, 64GB,256GB,512GB na RAM 4GB |
Kamera | Kamera TATU
|
Muundo | Urefu-5.8inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 1,386,000/= |
iPhone 11 ni ndefu kuliko iPhone 11 pro kwa sababu pro kimo chake inchi 5.8
iPhone 11 pro ina kamera iliyoongezeka ambayo ni telephoto yenye kupiga vitu ambavyo vipo mbali kiasi.
Telephoto ya iphone 11 pro inatumia optical zoom kukuza kitu kilichopo mbali.
Ila zoom yake ni ndogo, inakuza kitu mara mbili.
Kioo chake ni cha OLED, Apple wanakibrand kama super retina XR OLED.
Kina resolution kubwa na ni angavu hata ukiwa unaitumia kwenye jua, screen itaonyesha vitu vizuri.
Upande wa memori upo sawa na iphone 11 ila kuna iphone 12 pro ambayo ina ukubwa wa 512GB.
Betri yake ni dogo hivyo umeme wa wati 18 unaweza kujaza betri hili mapema.
Ukaaji wa betri wa hii simu si wa kuridhisha sana.
Betri yake inadumu kwa masaa 13 simu ikiwa inatumia intaneti.
Kwenye majaribio ya betri ya gsmarena iphone 12 pro inakaa na chaji masaa 17 ukiwa unaongea
iPhone 11 Pro Max
Simu ya iPhone 11 pro max ni ndefu kuliko iphone 11 na iphone 11 pro.
iPhone 11 pro inafana vitu vingi na simu ya iPhone 11 Pro Max.
Tofauti kubwa ipo tu upande wa betri.
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Super Retina XDR OLED |
Softawre |
|
Memori | 64GB,256GB,512GB na RAM 4GB |
Kamera | Kamera TATU
|
Muundo | Urefu-6.5inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 1,476,090/= |
Betri yake na inakaa na chaji muda mrefu kuliko iphone 11 zingine.
Kmarea zipo nne na iliyoongezeka ni ya Ultrawide ambayo hupiga eneo pana.
iPhone 12
Mwaka 2020 apple walizindua iphone toleo la 12 moja wapo ni iPhone 12.
Simu ya iphone 12 inatumia processor ya Apple A14 Bionic.
Apple wanadai A14 uwezo wake umeongezeka kwa 40% ukilinganisha na processor zilizotangulia.
App kama GeekBench 5 zinazopima uwezo wa chip zinaonyesha Bionic A14 kuwa na nguvu kubwa kiutendaji.
Kwa maana hiyo app zinazotumia nguvu kubwa zinafunguka kwa wepesi na haraka bila kukwama.
Processor iliyopo kwenye iphone 12 inakubali aina zote tatu za 5G.
Aina tatu za 5G ni mmWave, Mid Band na Low Band 5G.
Matoleo ya iPhone 12 yanashindana na samsung matoleo ya S20.
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Super Retina XDR OLED |
Softawre |
|
Memori | NVMe, 64GB,128GB,256GB na RAM 4GB |
Kamera | Kamera mbili
|
Muundo | Urefu-6.1inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 1,386,000/= |
Simu ina iOS 14.1 lakini inakubwali kuwekwa iOS 15.3
Kioo kilichopo cha OLED kimeboreshwa upande wa uangavu tofauti na iPhone 11.
Upande wa kamera zipo kamera mbili ambazo zinarenga na kupiga picha vizuri.
Kubwa kamera kubwa inapitisha mwanga wa kutosha na zote kamera kuu ina OIS na dual pixel PDAF.
iPhone 12 ni ndefu kiasi kwani ina kimo cha 6.1
Betri yake ni ndogo la 2815mAh.
Mfumo endeshi wa iOS huwa una matumizi mazuri ya umeme hivyo betri yake inaweza kukaa na chaji kwa masaa 12 ikiwa kwenye intaneti.
Udogo wa betri unachangia umeme wa chaji wa 18W kujaza betri kwa haraka.
iPhone 12 zipo za aina, kuna za 64GB, 128GB na 256GB.
Kitu kimoja ambacho karibu simu zote za iPhone inacho ni IP68.
IP68 huonyesha uimara wa simu kuzuia maji kupenya ndani simu.
Ukiidumbukiza iphone 12 kwenye maji ya kina cha mita 6 maji hayatopenya ndani ya simu kwa muda wa nusu saa.
https://www.youtube.com/watch?v=Lv1kofMtpFs
iPhone 12 Pro
Simu ya iPhone 12 Pro pia inatumia processor Apple Bionic A14.
Tofauti iliyopo kati ya iPhone 12 Pro na iphone 12 ni upande wa kamera.
Vitu vingine vinafanana.
iPhone 12 Pro ina kamera nne.
Kamera mbili zilizoongezeka ni telephoto na TOF 3D LiDAR
Kirefu cha Light Detection and Ranging.
Ni kamera ambayo inatoa miyale ya mwanga kuscan vitu vinavyopigwa picha.
LiDAR hutumika sana kwenye Augmented Reality.
Augmented Reality ni kitendo cha kuweka vitu kwenye picha au video ambayo havikuwepo.
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Super Retina XDR OLED |
Softawre |
|
Memori | NVMe, 64GB,128GB,256GB,512GB na RAM 6GB |
Kamera | Kamera nne
|
Muundo | Urefu-6.1inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 1,963,500/= |
iPhone 12 pro zipo za aina tatu ambazo ni 64GB, 128GB na 256GB
iPhone 12 Pro Max
Simu ya iPhone 12 Pro max ni ndefu kuliko iphone 12 na iphone 12 pro.
Pia iPhone 12 Pro max ram yake ni kubwa.
Pia iphone 12 pro max ina betri kubwa na chaji yake inapeleka umeme mwingi kiasi wa 22W.
Sifa zingine zipo sawa.
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Super Retina XDR OLED |
Softawre |
|
Memori | NVMe, 64GB,128GB,256GB,512GB na RAM 6GB |
Kamera | Kamera TATU
|
Muundo | Urefu-6.7inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 2,286,900/= |
iPhone 13
Matoleo ya iPhone 13 yazinduliwa mwaka 2021 yakiwa yanatumia mfumo endeshi na processor mpya.
Processor yenye uwezo mkubwa kuliko processor yoyote ya simu kabla ya ujio wa processor ya Snapdragon 8 gen 1.
Apple A15 Bionic ina modem ambayo inasapoti mtandao wa 5G.
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Super Retina XDR OLED, |
Softawre |
|
Memori | NVMe,
128GB,256GB,512GB na RAM 4GB |
Kamera | Kamera mbili
|
Muundo | Urefu-6.1inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 2,217,600/= |
Apple 13 ina kamera mbili upande wa nyuma.
Kamera kuu inayo OIS na dual pixel PDAF ambazo hufanya video na picha kupigwa kwa ubora.
Betri lake lina ukubwa 3240mAh na mfumo wake wa chaji unapeleka umeme wa 23Wati.
Hivyo betri hili dogo linaweza kujaa kwa haraka.
Matoleo ya iPhone 13 yanasifika kwa ukaaji wa chaji.
Simu ya iPhone 13 inauwezo wa kuzuia maji kupenya endapo ikidumbukia kwenye maji ya kina cha mita 6 kutokana na kuwa IP68.
Bodi ya iphone 13 upande wa nyuma na mbele imeundwa kwa glasi ya gorilla ambayo huwa ni ngumu kuchunika na kupasuka.
Mfumo wake wa memori una kasi na iphone 13 zipo za aina tatu kama jedwali linavyoonekana upande wa memori.
Upande wa ram simu inatumia RAM ya 4GB.
iPhone 13 Pro
Simu ya iphone 13 pro ina kamera nne.
Display iliyopo kwneye hii simu ni sawa na ile iliyopo kwenye iPhone 13 ambayo ni OLED.
Kamera zilizoongezeka ni Ultrawide na LiDAR.
iPhone 13 pro inatumia RAM yenye ukubwa wa 6GB
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Super Retina XDR OLED |
Softawre |
|
Memori | NVMe , 128GB, 256GB,512GB, 1TB na RAM 6GB |
Kamera | Kamera nne
|
Muundo | Urefu-6.1inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 2,310,000/= |
Betri yake imepungua ujazo tofauti na mtangulizi wake.
iPhone 13 pro zipo za matoleo manne(Kuna yenye memori ya 1T yaani 1000gb)
iPhone 13 Pro Max
Simu ya iphone 13 pro max ina fast chaji inayopeleka umeme mwingi wa wati 27.
Hivyo betri lake kubwa la 4352mAh linajaa ndani ya muda mfupi.
Ni simu inayokaa sana na chaji ukilinganisha na samsung s21 ultra.
iPhone 13 pro max ni ndefu kuliko iphone 13 pro na iphone 13.
Ukizitazama sifa za simu ya iphone 13 pro max nyingi zinafanana na iphone 13 pro.
Kila sifa iliyopo kwenye iphone 13 ipo kwenye iphone 13 pro na iphone 13 pro max
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Super Retina XDR OLED |
Softawre |
|
Memori | NVMe,
128GB,256GB,512GB, 1TB na RAM 6GB |
Kamera | Kamera nne
|
Muundo | Urefu-6.7inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 2,538,690/= |
iPhone XR
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Liquid Retina IPS LCD |
Softawre |
|
Memori | NVMe,64,128GB,256GBna RAM 3GB |
Kamera | Kamera MOJA
|
Muundo | Urefu-6.1inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 713,790/= |
Maoni 2 kuhusu “Simu Nzuri za iPhone na Bei Zake 2022”
Je naweza kuapata IPhone used yenye GB 256 kwa bei ya laki 5
Mbona matoleo ya iphone wanafeli upande wa betri ya simu
Ukilinganisha na matoleo mengine ya simu kama Infinix yenye betery yenye ngu 6000 na kuendelea?