Iwapo unapanga kununua simu chini ya laki tatu au zisizozidi laki nne usitarajie kupata simu yenye ubora mkubwa
Kwa maana usitarajie kamera kali na utendaji mkubwa
Ila kwenye hii post kuna simu zote za laki tatu na chini ya laki nne zenye memori kubwa na utendaji wa wastani
Ubora ambao unakuwezesha kutumia app za muhimu zinazokidhi mahitaji yako
Aina za simu ni kutoka makampuni yafuatayo
- Infinix
- Samsung
- Xiaomi
- Oppo
- Vivo
- Tecno
- Realme
Sasa tuzitazame sifa za muhimu zinazohitajika zaidi na watumiaji wa simu wengi
Infinix Smart 9
Infinix ni simu yenye kamera ambayo ukubwa wake ni megapixel 13
Inaweza kurekodi video za full hd pekee
Bei yake ya GB 64 ni shilingi laki mbili na sabini (270,000)
Ina betri ya ukubwa wa 5000mAh ila kasi ya chaji yake ni wati 10 kama kiwango cha juu
Utendaji ni wa wastani kwa sababu inatumia chip ya Helio G81 ambayo inatumia core aina ya Cortex A75 kwenye yenye nguvu kubwa
Inakuja na mfumo endeshi wa Android 14 Go edition na haitopata android inayofuata
Infinix Smart 9 HD
Simu ya Infinix Smart 9 HD inauzwa kiasi cha shilingi 250,000 (laki mbili na nusu)
Hii ikiwa na ukubwa wa GB 64 na RAM ya GB 4
Pia ina kamera yenye ukubwa wa MP 13 haina vitu vingine vya ziada
Betri yake ina ukubwa wa mAh 5000 na chaji ya kasi ni wati 10
Utendaji sio mkubwa ukilinganisha na infinix smart 9
Hii inatokana na smart 9 hd kutumia processor Helio g50 ambazo zinatumia muundo wa Cortex A53
Tecno Spark 30C
Tecno Spark 30C inauzwa shilingi laki tatu na elfu ishirini
Iwapo simu za mbili za mwanzo hadhikizi unachotaka Tecno Spark 30C ni mbadala sahihi
Kuanzia skrini, inakupa refresh rate ya kiasi cha 120Hz
Kamera kubwa na lenzi moja ya usaidizi na kamera yake ina ukubwa wa megapixel 50
Utendaji wake ni mzuri unaoweza kusukuma vitu vingi japo si kwa ukubwa sana ila inafaa
Kizuri zaidi ina waterproof ya kuzuia maji ya kunyunyuluzika
Betri uku0bwa wake ni mAh na inachaji mpaka wati 18
Samsung Galaxy A06
Samsung Galaxy A06 kuipata kwa bei ya shilingi laki mbili na tisini
Haina tofauti kubwa na Tecno Spark 30C
Isipokuwa Samsung inaahidi kuipa simu maboresho kwa muda wa miaka miwili
Yaani itapata hadi android 16
Inatumia chip ya Mediatek Helio G85, hivyo utendaji wake ni wa wastani
Kamera yake ni kubwa na ina megapixel 50
Pia ina kamera nyingine ambayo haina umuhimu wa kihivyo
Samsung Galaxy A05
Samsung Galaxy A05 ni simu ya mwaka 2023 ila bado inaendana na wakati wa sasa
Bei yake kwa sasa ni shilingi laki mbili na sabini
Inasapoti chaji ya wati 25 hivyo betri yake ya mAh 5000 inawahi kujaa kwa haraka
Utendaji wake uko sawa na Galaxy A06 kwa sababu zinatumia processor moja
Ina kamera mbili na kamera kubwa ina 50MP
Inakuja na android 13 na haipati toleo lingine jipya
Tecno Pop 9
Bei ya Tecno Pop 9 ni shilingi 270,000 ikiwa ni ya GB 64
Utendaji wake ni mzuri kwa sababu inatumia chip ya Unisoc T615
Kamera yake ukubwa ni megapixel 13 ikiwa na ulengaji wa PDAF
Inakuja na mfumo endeshi wa Android 14 Go Edition
Kioo chake kinakuja na refresh rate ya 120Hz
Chaji inasapoti umeme wa wati 15
Redmi 14C
Bei ya Redmi 14C ni shilingi laki tatu na nusu (350,000)
Bei yake ipo juu kidogo ukilinganisha na simu zingine zilizopo hapa
Ila kiutendaji haina tofauti kubwa na simu zingine
Kitu cha ziada inakuja na skrini prtotecta yenye uwezo wa kuzuia michubuko
Inatumia Android 14 na haitopata Android 14
Kamera yake kubwa ina megapixel 50
Betri yake ukubwa ni mAh 5160, na chaji inapeleka hadi umeme wa wati 18
Oppo A3X
Oppo A3X inauzwa kwa shilingi 300,000 (laki tatu) japo kwa sasa inapatikana India
Betri yake ina ukubwa wa mAh 5100
Pia utendaji wake ni mzuri kutokana kutumia processor ya Mediatek Dimensity 6300
Ni simu inayopleleka chaji kwa kasi kubwa inayofika wati 45
Hii inajaza simu kwa 50% ndani ya nusu saa
Kamera yake sio kubwa ina megapixel 8 tu ila ina ulengaji wa PDAF
Pi aina waterproof aina ya IP54
Vivo Y19s
Vivo Y19s inauzwa kwa kiasi cha shilingi laki tatu na nusu (350,000)
Kwa ufanano wa kiutendaji inaendana na Oppo A3X
Inakuja na toleo la Android 14 na haitokuwa na update ya android mpya
Betri yake ina ukubwa 5500mAh, inakaa na chaji muda mrefu
Ila itachukua muda kujaa kwa sababu chaji inayosapoti kiwango cha juu ni wati 15
Utendaji wake pia ni wa kuridhisha kwani inatumia chip ya Unisoc Tiger T612
Ukubwa wa kamera yake ni megapixel 50
Realme C63
Bei ya Realme C63 ni shilingi 350,000 kwa Tanzania
Realme inaweza kuwa ni jina geni ila ni moja ya kampuni ya china inayotengeneza simu nzuri
Realme C63 ina kamera moja yenye megapixel 50
Chaji yake inasapoti umeme wa wati 45 hivyo simu inawahi kujaa kwa haraka
Utendaji wake ni wa wastani kwa sababu ya uwepo wa processor ya Unisoc Tiger T612
Na inakuja na Android 14, haitapokea toleo lingine la Android