Infinix Hot 60 ni matoleo ya daraja kati yaliyoingia rasmi sokoni mnamo mwezi Julai 2025
Bei zake sio kubwa ni za wastani huku ukiwa na uhakika wa kupata mifumo mingi ya AI ambapo kwa brand zingine huweka kwenye simu za daraja juu
Infinix hot 60 zimekuja na maboresho upande wa betri, skrini na uimara wa bodi bila kusahau softaware
Hapa utaona simu zote za mpya za infinix hot 60 na bei zake kwa wakati huu kwa hapa Tanzania
Infinix Hot 60 Pro
Bei ya Infinix hot 60 Pro ni shilingi laki nne (400,000)
Hii ni infinix yenye ukubwa wa RAM GB 8 na ukubwa wa GB 128
Pia kuna infinix ya ukubwa wa GB 256 na bei yake pia ni kubwa zaidi ya GB 128
Sifa kubwa nzuri za hii simu ina kioo cha amoled chenye refresh rate inayofika 144Hz
Ina ulinzi wa kioo aina ya Corning Gorilla glass 7i
Pia betri kubwa ya mAh 5160 na chaji ya wati 45 na uwezo wa kuchaji vifaa vingine kwa umeme wa wati 10
Infinix Hot 60i
Bei ya Infinix Hot 60i ni shilingi laki tatu (300,000)
Hii ikiwa na ukubwa wa GB 128 na RAM ya GB 8
Ndio infinix hot 60 yenye bei ndogo zaidi kati ya zilizotoka mwaka 2025
Sifa yake kubwa ni kwamba bei yake ni rahisi ila inakupa mifumo mingi ya AI kama ilivyo kwenye simu za Infinix Note 50
Pia chaji inapeleka umeme mwingi wa wati 45
Na pia ina ulinzi wa waterproof aina ya IP64
Infinix Hot 60 Pro+
Infinix Hot 60 Pro+ ya GB 256 inauzwa shilingi laki tano na elfu therathini (530,000)
Hii ikiwa na ukubwa wa RAM ya GB 8
Kisifa hii simu haina tofauti sana infinix hot 60 pro
Vitu vingi vinafanana
Kwenye makara zijazo tutazama kiundani kuangalia kila sifa na upekee wa simu
Maoni 8 kuhusu “Simu mpya za Infinix Hot 60 na bei zake”
Iko vizuli kweli namimi nimeipenda
Zanzibar
Kama itakuwa nyembamba na siyo nzito kama Infinix hot 40i, nanitakuwa mtajawao daima kwa betri wapi vizuri hawajawai feli
mimi nimfanya biashara pia ninarekebisha
hizisim
sawa karibu
Naitaka hi sim chap
Karibu kwa mawasiliano
Naitaka