Mwaka 2021 oppo ilishika nafasi ya tano katika soko la smartphone kutokana na watumiaji wa simu kuvutiwa na matolea ya oppo.
2021 kulikuwa kuna simu nzuri za oppo nyingi na ambazo bado zinauhitaji mwaka 2022.
Oppo ni kampuni bunifu sana katika uundaji wa simu iliyo kamiri katika idara nyingi upande wa hardware na software pamoja na simu zenye kuvutia kimuonekano.
Simu za oppo huwa zinatumia betri zinazotunza chaji, processor zenye nguvu, screen zenye uangavu wa kuonyesha vitu kwenye mazingira yoyote.
Mara nyingi smartphone bora za oppo zinahitaji bajeti kubwa.
Lakini pia zipo smartphone kali za oppo ambazo yeyote anaweza kuzipata kwa bajeti ndogo.
Utazijua sifa za simu za oppo ambazo ni ghari yaani matoleo ya OPPO Find x na OPPO Reno series.
Na matoleo ya bajeti za kati na chini yaani OPPO A Series.
Hizi ni baadhi ya simu bora za oppo na bei zake.
Kwa kifupi, ukitaka kufahamu ubora wa oppo ambao unatoa ushindani kampuni za samsung na apple inabidi ujue sifa ya kila simu zilizopo kwenye orodha.
OPPO A96
Oppo A96 ni smartphone ya bei nafuu kwa upande wa oppo ambayo ina mtandao wa 5G na ni toleao la mwaka 2022.
Ubora wa A96 umejikita hasa kwenye chaji, mtandao, kioo yaani display.
Japokuwa ina 5g ila inatumia processor(SoC) yenye ubora wa kati aina ya Snapdragon 695 5G.
[Image of OppoA96]
Snadragon 695 inasapoti aina mbili za ya mtandao wa 5G ambazo ni sub-6 na mmWave.
Sub-6 inatumia miundombinu ya mtandao wa 4G ambayo inakuwa imeboreshwa.
Sub-6 inafanya kazi kwenye masafa ya 2GHz-6GHz ambayo spidi yake haina tofauti sana na 4G.
Ila mmWave haya ni masafa mapya kabisa na ni makubwa kati ya 30GHz-300GHz.
Spidi ya mmWave ni kubwa.
Hii inaifanya OPPO A96 kuwa na spidi kubwa ya intaneti.
OPPO A96 inatumia display(kioo) cha OLED ai uangavu wake ni kiwango cha 400nits mpaka 600nit.
600nits inafanya screen ioneshe vizuri vizuri ikiwa inatumika kwenye mazingira ya jua kali.
Unajua kuwa kuna simu ukitoka nje ya nyumba unashindwa kuona vizuri. Hii inasababishwa na nits ndogo.
Kwa wapenda picha wanaweza wasivutiwe na hii sababu ina kamera ambazo hazina OIS na video ya 4k.
Ukipiga picha huku unatembea picha haitatokea vizuri.
Betri sio kubwa ila ina chaji kwa haraka ndani ya dakika 30 simu hujaa kwa asilimia 67.
Sifa za oppo a96 kwa ufupi
Sehemu za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | OLED |
Softawre |
|
Memori | UFS 2.2 256GB na RAM 8GB |
Kamera | Kamera mbili
Selfie-16MP |
Muundo | Urefu-6.4inchi |
Chaji na Betri |
|
Unaweza kuzicheki sifa nyinginezo kiundani za kuhusu sifa za oppo a96 gsmarena
OPPO A94
Oppo A94 ni smartphone inayotumia processor ya MediaTek yenye ubora wa kati.
Simu hii iliyozinduliwa ina network 2G,3G na 4G pekee.
Sababu kuu inachangiwa na SoC Helio P95 kutokuwa na modem ya 5G.
Kamera ya selfie ina gyro-EIS, kamera za nyuma zipo tatu na hazina OIS.
gyro-EIS inaipa utulivu kamera wakati unachukua video ya kitu kinachotembea ama ukiwa unatembea kwenye gari ama kwa mguu.
Utulivu huu uboresha video kuonekana vizuri.
[Video]
Kamera za nyuma hazina hii teknolojia ya OIS.
OPPO A94 ina jumla ya kamera nne.
Kamera kuu ina sensa ya ukubwa wa kawaida(1/2.0”) inayoweza toa picha yenye ubora wa megapixel 48.
Kamera ya ultrawide kwa ajili ya kupiga picha eneo kwa upana wa angle 119 inatumia sensa ndogo sana yenye ukubwa wa inchi (1/ 4.0”).
Hii inamaanisha kamera ya ultrawide ya OPPO A94 inapiga picha kwa ubora wa chini kama sio hafifu.
Storage(memory) inawezesha kuweka vitu vingi na kuinstall apps za kutosha na inaload kwa spidi kubwa.
Ukubwa wa memory upande wa RAM 8GB na memory kawaida ina 128GB.
Memory yake haina spidi kubwa.
Mfumo wa chaji unajaza betri kwa spidi kubwa.
Betri yake ina saizi ya 4500mAh, hii betri hujazwa kwa asilimia 50 ndani ya nusu.
Kiwastani simu hujaa chaji chini ya dakika 100.
Kiuhalisia ubora wa A94 upo kwenye spidi ya kujaza betri.
Na kasoro yake betri ni dogo 4310mAh aina ya Li-Po.
Simu hii haina uwezo wa kuchaji vifaa vingine kwa maana haina mfumo wa reverse charging.
Simu pia si imara hasa inapokumbana na maji lakini imeundwa kwa kutumia plastiki na haina screen potector aina ya gollilla ambazo hufahamika kwa uimara wake.
Sababu ya kukosekana huu ni kukosekana kwa viwango(rating) IP(Ingression Protection).
Kiukweli simu haina uwezo kuzuia maji kuingia.
Lakini pia chaji yake inatumia USB-Type C 2.0
Sifa za simu ya OPPO A94 kwa ufupi.
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g na 4G |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | AMOLED, Uang’avu-800nits |
Softawre |
|
Memori | 128GB na RAM 8GB |
Kamera | Kamera nne
|
Muundo | Urefu-6.4inchi |
Chaji na Betri |
|
OPPO A94 5G
Simu ya oppo A94 5G ni toleo ambalo linatumia SoC(processor) bora za mediatek aina ya Dimensity 800U 5G.
Toleo hili halina tofauti na smartphone ya OPPO A94 isipokuwa kwenye processor pekee.
Processor ya Dimensity 800U 5G ina nguvu kubwa kuliko Helio P95.
Dimensity 800U 5G ina modem ya 5g yenye spidi ya 2.3Gbps kwa mujibu wa MediTek.
Ieleweke 5g spidi yake ni kubwa mara mia ya spidi ya 4G.
Pia SoC ya dimensity ina uwezo wa kufungua vitu vingi vinavyoitaji nguvu kubwa bila kukwama.
Utaenjoi ukiwa unacheza gemu kwenye hii ukizingatia Mali-G57 MC3
Na gpu ya Mali G57 MC3 ina gemu kwa ubora wa juu(High resolution) kubwa bila kupoteza ubora wa picha.
Dimensity inatumia core aina ya Cortex A76 na Cortex A-55.
Cortex A76 ni core zinazochakata vitu vinavyohitaji nguvu kubwa na kinyume chake kwa Cortex A55.
Memori ya hii simu pia ina spidi kubwa ya kukopi vitu ukilinganisha na mtangulizi wake kwani inatumia UFS 2.2
Sifa za simu ya oppo A94 5g kwa ufupi.
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Super Amoled, Uang’avu-800nits |
Softawre |
|
Memori | 128GB na RAM 8GB |
Kamera | Kamera NNE
|
Muundo | Urefu-6.4inchi |
Chaji na Betri |
|
OPPO A74 5G
Simu ya oppo A74 5g ambayo inatumia SoC yenye uwezo wa kati ambayo imetengenezwa na Kampuni Qualcomm.
Processor ya OPPO A74 5G ni Snapdragon 480 5G.
Hii smartphone inatumia mfumo wa memory wenye kasi japo si kubwa lakini una kasi ya kuridhisha ukiwa unakopi vitu ama kudownload basi kazi inamalizika kwa haraka.
Kasoro moja wapo ya hii simu ni kuwa na mfumo wa chaji ambao unapeleka umeme kidogo wa Wati 18.
Inafanya betri iliyopo kwenye simu ya ukubwa wa 5000mAh kuchukua zaidi ya masaa matatu kujaa.
Hitarajiwi simu ya aina kuwa taratibu namna hii.
Oppo A74 5g inatumia display za kawaida ambazo zinahitaji taa za redi LED kumulika screen.
Display hizo hufahamika kama IPS LCD yenye refresh rate 90Hz.
Ni kweli refresh ya 90Hz inafanya screen kufanya kazi kwa haraka hasa ukiwa unacheza gemu.
Lakini IPS LCD ina uwezo wa kuonyesha rangi chache kulinganisha na AMOLED hivyo baadhi ya vitu havitaonekana kwa uhalisia.
Pia display ina nits chache kiasi cha 480 nits.
Ukiwa unatumia simu kwenye jua unaweza usione vizuri kwa sababu ya uangavu mdogo.
Sifa za simu ya oppo A74 5g kwa ufupi
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD, Refresh rate:90Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS 2.1, 128GB na RAM 8GB |
Kamera | Kamera mbili
|
Muundo | Urefu-6.5inchi |
Chaji na Betri |
|
OPPO A95
Smartphone ya oppo a95 inatumia SoC ya ubora wa kati inayofahamika Snapdragon 662.
Processor hii uwezo wake ni wa kawaida kwa sababu Core mbili zenye nguvu zina spidi ya 2.0GHz yaani 2×2.0GHz zikiwa zinatumia muundo wa Kryo 260 kufanya kazi.
Kryo 260 inamaanisha nini?
Kikawaida processor huwa ina muundo wa namna ya kutekeleza kazi(Instructions).
Kryo ni muundo ambao umebuniwa na Snapdragon.
Kuna miundo ambayo inaipa procsessor uwezo wa kufanya kazi nyingi na nyingine ndogo.
Kiwango cha kazi hupimwa GHz kwa mzunguko mmoja.
Kryo 260 ni muundo unaofanya kazi za kawaida na si nyingi.
Kiwango cha juu cha juu 2GHz.
Hivyo hii ina maana OPPO A95 inafanya kazi zinazohitaji nguvu ndogo ndogo.
Ukiwa unaitumia kucheza gemu na wakati huo upo kwenye intaneti unaweza ukawa unapata tatizo la simu kukwama na simu kupata moto.
Ujazo wa memori yake ni 128GB inatosha sana kuhifadhi vitu vya kutosha.
Na RAM yake ni 8gb ambayo inafaa tu kufungua apps nyingi.
Simu ina 4G lakini ni ile yenye spidi ya kasi ya 600Mb/s.
Kumbuka kuna makundi mengi ya 4G.
Haina 5G.
OPPO A95 ni moja ya smartphone inayokaa na chaji muda mrefu.
Na mfumo wa chaji unawahi kujaza simu ndani ya muda mfupi(Kimakadirio chini ya dakika 90).
Chaji yake hupeleka umeme mkubwa(fast charge) wa wati 33
Mara nyingi mabetri ya simu yenye 5000mAh hutunza moto.
Simu hii haina kamera nzuri kwa kutazama ukubwa wa sensa.
Na pia haina HDR.
Na haina ultrawide kamera ya kuchukua picha za eneo kubwa.
Kwenye kamera wamefeli.
Sifa za simu ya OPPO A95 kwa ufupi.
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g na 4G |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Amoled |
Softawre |
|
Memori | 128GB,256GB na RAM 8GB |
Kamera | Kamera tatu
|
Muundo | Urefu-6.4inchi |
Chaji na Betri |
|
OPPO FIND X3 PRO
OPPO Find x3 ni simu nzuri ya oppo karibu kwenye idara zote tofauti na oppo zilizotangulia.
Tukianza na SoC(processor).
Ni Snapdragon 888 5G inayoipa nguvu find x3 pro.
SoC ya snapdragon 888 ina GPU ya 660 nzuri sana kwa ajili ya gemu na kazi zingine nzito.
Qualcomm 888 ina core(processor) nane na zote zina uwezo wa kupiga kazi kubwa kubwa kwa ufanisi.
Maana ya Core
-Kikawaida CPU(processor) hugawanyika katika makundi ya kiutendaji
Huu mganyo hufahamika core kwa hiyo core pia ni processor
Hivyo procssesor inaweza ikagawanyika zaidi ya mara moja.
Tukirudi kwenye simu,
Ina 5G network yenye spidi na uwezo wa kuchakata mawimbi ya aina yote 5G.
5G zipo za aina zaidi ya mbili ambazo ni Sub-6 na mmWave.
Na inaweza kuunganisha sub-6 na mmWave.
Kuhusu kasi ya inteneti ya OPPO finfd x3 PRO ni kubwa.
Inatumia memori(storage) yenye kasi ya UFS 3.1
Ukiwasha OPPO FIND X3 PRO simu inawaka chini ya sekunde 3 na ukikopi kitu kinamalazika kwa haraka kulinganisha na simu zisizo na UFS 3.1
Ina fast charge inayojaza simu kwa asilimia 40 ndani ya dakika 10.
Kioo chake ni cha amoled ambacho kinaonyesha picha kwa uhalisia.
Kina HDR10+ inayosaidia picha zilizopigwa kwenye mwanga hafifu kuonekana vizuri.
Na kioo chake kinafanya simu kuwa nyepesi sababu ya REFRESH RATE ya 120Hz
Simu ina uwezo wa kuzuia maji kutokana na kuwa na IP68
Sifa za simu ya OPPO Find X3 Pro kwa ufupi.
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g na 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | LTPO AMOLED |
Softawre |
|
Memori | UFS 3.1, 256GB, 512, RAM-8GB na 12GB |
Kamera | Kamera nne
|
Muundo | Urefu-6.7inchi |
Chaji na Betri |
|
OPPO FIND X2 PRO
Ubora wa simu ya OPPO Find X2 Pro upo kwenye chaja.
Ndani ya dakika 38 betri yake ya 4260mAh hujaa.
Ina 5G na inatumia processor Snapdragon 865 5g
Ina nguvu lakini si kama Snapdragon 888
Kioo cha amoled na refresh rate ya 120Hz inafanya simu kuwa laini pale unapotachi.
Memori yake ina nafasi kubwa.
Zipo OPPO Find X2 Pro zenye ram ya 12gb na Rom ya 256GB na 512GB ya UFS 3.0.
Kama ni mtu wa kudownload sana basi 512 gb itafaa zaidi.
Inawezo kuzuia maji hata ukiizamisha kwenye kina cha 1.5m kwa dakika 30.
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Amoled |
Softawre |
|
Memori | UFS 3.0, 256GB na RAM 8GB, 512 na RAM 8GB |
Kamera | Kamera tatu
|
Muundo | Urefu-6.7inchi |
Chaji na Betri |
|
OPPO RENO5 5G
Smartphone ya oppo reno5 5g ni nzuri lakini sio nzuri kiivyo ukilinganisha na bei yake.
Mfumo wake wa kamera hauna OIS kwenye kamera zake zote nne.
Hakuna ulinzi pale simu inapozamishwa kwenye maji.
Maji tiririka tu yanaweza haribu simu.
Kitu kikubwa kizuri cha oppo reno5 5g ni mfumo wa chaji unaojaza betri yake ya Li-Po kwa asilimia 100 ndani ya dakika 35 tu.
Kwa mtumiaji mwenye matumizi ya kawaida bado atapata performance kubwa kutokana na processor yenye uwezo wa kati ya Snapdragon 765 5g.
Betri yake hukaa na chaji kwa masaa 109(data ikiwa imezimwa).
Kwa kuhifadhi mafaili mengi inafaa ina memori kubwa na RAM ya kutosha.
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Amoled |
Softawre |
|
Memori | UFS 2.1, 128GB na RAM 8GB, 256GB na RAM 12GB |
Kamera | Kamera mbili
|
Muundo | Urefu-6.43inchi |
Chaji na Betri |
|
OPPO RENO6 5G
Toleo la OPPO RENO6 5G ni toleo lililoboreshwa la reno5.
Maboresho yapo kwenye processor.
Reno6 inatumia chip ya mediatek dimensity 900.
Dimensity 900 ni SoC yenye uwezo wa kati.
Na inauwezo kufanya utendaji mkubwa wa screen yenye refresh rate 120Hz.
Lakini kioo cha reno5 ni cha AMOLED chenye refresh rate ya 90Hz.
90Hz bado ni kiwango kizuri kinachofanya simu kuwa nyepesi.
Ubora wa betri ni ule ule wa wati 65 ambayo inajaza betri ya 4300mAh ndani ya dakika 35.
Haina waterproof, simu ikiingia ndani ya maji. Maji yanaweza yakapenya kwenye simu.
Upande wa memori, zipo za 128GB na 256GB na RAM ya 8GB na 12GB.
Kamera zake tatu bado si za kuvutia hakuna kamera depth sensor.
Depth sensor inatoa miale inayoscan kila pande ya kitu kinachopigwa picha.
Pia simu ina 5G kama jina la simu linavyojianisha.
Sifa za simu ya OPPO RENO6 5G kwa ufupi.
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g na 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Amoled |
Softawre |
|
Memori | UFS 2.1, 128GB na RAM 8GB, 256 na RAM 12GB |
Kamera | Kamera tatu
|
Muundo | Urefu-6.43inchi |
Chaji na Betri |
|
OPPO RENO7 PRO 5G
OPPO RENO7 PRO 5G ni simu mpya ya oppo ambayo imeingia sokoni mwaka mwishoni mwa 2021.
Inatumia processor yenye nguvu ya MediaTek Dimensity 1200 Max.
Dimensity 1200 Max inaweza kufungua app kubwa nyingi ikiwemo magemu na applikesheni za graphics kwa pamoja bila kukwama.
Sababu kuu processor ina core mbili(2) zenye nguvu ya kazi kwa kiwango cha 3GHz
Zina memori zenye kasi aina ya UFS 3.1.
Ukubwa wa memori ni 256GB na RAM zipo za 8GB na 12GB.
Simu pia ina 5G na intaneti yake ina kusi kubwa.
4G ya oppo Reno7 Pro 5g ina sapoti mitandao yote.
Ina betri ndogo yenye uwezo wa kustahamili kukaa na chaji kwa masaa karibu 100 data ikiwa imezimwa.
Mfumo wake wa chaji unapeleka umeme mkubwa wa 65W(wati 65).
Umeme wa wati 65 hujaza simu ya 4500mAh ndani ya dakika 35 tu.
Upande wa kioo, inatumia kioo cha AMOLED chenye refresh rate 90Hz.
Uang’avu wake ni 920nits ambao unafanya screen ioneshe vitu vizuri hata ukiwa nje ya nyumba kwenye jua.
Kasoro moja ya oppo reno7 pro 5g ni kutokuwa na waterproof(IP68).
Simu ikizama kwenye maji, maji lazima yapenye kwenye simu.
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Amoled |
Softawre |
|
Memori | UFS 3.1, 256GB na RAM 8GB, 256GB na RAM 12GB |
Kamera | Kamera tatu
|
Muundo | Urefu-6.55inchi |
Chaji na Betri |
|
HITIMISHO
Simu za oppo zenye uwezo mkubwa huwa na vioo aina ya AMOLED na Processor ya Snapdragon 888. Simu nzruri zinakuja na fast chaji za wati 65. Karibu simu zote kali za oppo hujaa chaji ndani ya muda.
OPPO A-Series ni simu za bei nafuu lakini zenye maneno find x na reno ni matoleo ya gharama.
Maoni 9 kuhusu “Simu Nzuri za Oppo na bei zake”
Kichwa cha habari kizuri kabisa”SIMU NZURI ZA OPPO NA BEI ZAKE” sasa cha kushangaza nakuta sifa tu za simu bei wala sioni vipi hapo?
Tunashukuru kwa kutukumbisha tutaorodhesha bei za simu zote na kuongeza mpya
nahitaji simu ya oppo ya laki nne naweza kuipata
Inawezekana
Mbona aujaweka bei
oppo yangu programu zote zipo ka lugha ya kichina naomba msada kubadilishaa kuwa za kiingerza
Oppo toleo lipi
Andika bei
Ok nitaziweka