Hii ni orodha ya simu mpya za redmi na Xiaomi ambazo zimetoka mwanzoni mwa 2025 na mwishoni mwa 2024
Simu zilizoorodheshwa zipo za bei kubwa na bei ndogo
Hivyo basi utafahamu bei zake na sifa pamoja na ubora mkubwa kwenye kila simu iliyopo
Utaona simu ya Xiaomi iliyopo kwenye ligi moja na iPhone na Samsung
Tuzione sasa.
Xiaomi Redmi Note 14 Pro+ 5G
Bei ya Xiaomi Redmi Note 14 Pro+ 5G ni shiling milioni 1.1 ya ukubwa wa GB 256 na RAM GB 8
Utendaji wake unaweza kuhimili kucheza magemu tofauti bila shida
Kwani inatumia processor ya Snapdragon 7s Gen yenye ufanisi wa matumizi mazuri ya umeme
Ni simu yenye kamera tatu na kamera kubwa ina 200MP
Betri yake ina ukubwa wa 5110mAh na nguvu ya kuchaji ni kubwa ambayo ni 120W
Xiaomi Redmi Note 14 Pro 4G
Bei ya Xiaomi Redmi Note 14 Pro ni shilingi laki saba (700,000) ya ukubwa wa GB 256 na RAM GB 8
Na hii pia ina kamera tatu kubwa ikiwa na megapixel 200
Inakuja na mfumo endeshi wa Android 14 na haitopata toleo lingine
Betri yake ni kubwa sana ambayo ni 5500mAh ila chaji yake kasi ni 45mAh
Utendaji wake ni wa wastani kwa sababu inatumia processor Mediatek Helio G100 Ultra
Xiaomi Redmi Note 14 5G
Bei ya Redmi Note 14 5G ya GB 256 na RAM GB 8 ni shilingi laki saba
Boresho kubwa kwenye hii simu ni uwepo wa mtandao wa 5G
Kwenye kamera yapo yaliyopunguzwa, kamera kubwa ina 108MP
Hii simu itapokea matoleo mapya ya android kwa miaka miwili
Betri yake ina ukubwa wa 5110mAh na chaji inapeleka kasi ya wati 45
Xiaomi Remi Note 14 4G
Bei ya Redmi Note 14 4G ya ukubwa wa GB 128 na RAM ya GB 6 ni shilingi laki tano (500,000)
Haina utendaji mkubwa ila utendaji wake ni wa wastani
Inatumia chip ya mediatek helio G99 Ultra
Mfumo wake wa kamera ni wakawaida hauna vitu vingi ila kamera kubwa ina 108MP
Hii simu inakuja na Android 14 na itapata matoleo mengine mara nne
Xiaomi Redmi 14C 5G
Bei ya Xiaomi Redmi 14C 5G ya ukubwa wa GB 128 na RAM ya GB 4 ni laki tatu na elfu hamsini (350,000)
Ni simu ya daraja la chini ila utendaji wake ni mzuri ukilinganisha na bei
Kwani inatumia processor ya Snapdragon 4 Gen 2
Simu itapokea matoleo mapya mawili ya Android
Upande wa kamera kuna kamera moja tu yenye megapixel 50
Betri yake ina mAh 5160 na spidi ya chaji ni wati 18(sio kubwa)
Xiaomi 15 Ultra
Xiaomi 15 Ultra bei yake ni shilingi milioni mbili na kaki tano (2,500,000)
Hii ndio simu yenye ufunano na matoleo ya iphone 16 ama Samsung Galaxy S25
Ina jumla ya kamera nne na kamera kubwa ina megapixel 200 huku zingine zikiwa na megapixel 50
Betri yake ni kubwa na ina mAh 6000 na chaji ya kasi ya 90W
Ina nguvu kubwa ya kiutendaji kwa sababu ina processor ya Snapdragon 8 Elite
Simu inakuja na Android 15 na itapata matoleo mapya ya android mara nne tu.
Xiaomi Poco X7 Pro
Bei ya Xiaomi Poco X7 Pro ni milioni moja na laki moja yenye GB 256 na RAM ya GB 8
Ina kamera mbili tu huku kamera kubwa ikiwa na 50MP
Inatumia processor ya Dimensity 8400 Ultra hivyo utendaji wake ni mzuri
Inakuja na mfumo endeshi wa Android 15 na hakuna taarifa kama itapata toleo jipya
Betri yake ni kubwa (mah 6000) na chaji yake inasapoti wati 90