Unajua kuwa mwaka 2025, Tecno imezindua simu tatu mpya katika familia ya Spark 40?
Simu hizo ni:
📱 Tecno Spark 40
📱 Tecno Spark 40 Pro
📱 Tecno Spark 40 Pro+
Bei zke zinaanzia Tsh 260,000 hadi kufikia takribani Tsh 500,000.
Kila toleo lina sifa tofauti zinazolifanya lifae kwa matumizi maalum. Hii ina maana kuna Spark inayokufaa kulingana na bajeti na mahitaji yako.
Ni muhimu kuelewa vizuri kila moja ili ujue ipi inakufaa zaidi.
Twende tukazichambue moja baada ya nyingine
Tecno Spark 40
Bei ya Tecno Spark 40 ni shilingi laki mbili na sitini (260,000)
Hii ikiwa na ukubwa wa ram ya GB 4 na memori ya GB 128
Utendaji wake unafaa zaidi kwa matumizi ya kawaida ya kila siku
Kwa sababu prosesa yake ya Helio G81 ina nguvu ya wastani
Hii simu ina kamera moja yenye ukubwa megapixel 50
Inasapoti chaji ya wati 45 na betri yake ina ukubwa wa mAh 5200
Tecno Spark 40 Pro
Tecno Spark 40 Pro bei yake ni shilingi laki nne na ishirini (420,000)
Utendaji wake unakidhi kucheza baadhi ya gemu ila kwa settings za chini
Kwa sababu inatumia prosesa yenye nguvu ya wastani ambayo ni Mediatek Helio G100 Ultimate
Inakuja na kioo kizuri cha amoled chenye refresh rate inayofika hadi 144Hz
Upande wa betri ina 5200mAh na chaji inayopeleka umeme hadi wati 45
Ina kamera ya ukubwa wa 50MP inayoweza kurekodi video za ubora wa 1440p
Tecno Spark 40 Pro+
Tecno Spark 40 Pro+ inauzwa shilingi laki tano
Hii ni bei ya Spark 40 Pro+ ya GB 128 na RAM GB 8
Spark 40 Pro+ inasapoti kuchajiwa kwa njia ya wireless kwa umeme wa wati 30
Ni simu yenye cheti cha IP67 chenye kuashiria uwezo wa simu kuzuia maji ya kina cha mita 1.5
Ukiondoa vitu hivi viwili sifa zingine zote zinafanana Tecno Spark 40 Pro
Maoni 6 kuhusu “Simu mpya za Tecno Spark 40 na bei zake”
Hiii ya mwisho no nzur zaidi japo na ghari ila ni Bora na inafaa
Nahitaji tecno spark 40 mnapatikana wapi?
Sim nimeipenda Tecno Spark 40 unaweza kuonasifazake apa ukienda kuchukuwa huzikuti kwann nirinunua tecno pop8 nasikukuta nirivo
viitaji nikakutatofauti
Nahitaji tecno spark 40 pron GB 256 Bei yake
Ina mana Tecno spark 40 pro + ni toleo la mwisho kwenye mpangilio wa Tecno spark au Kuna zaidi ya spark 40 pro + na kama ipo inauzwa bei gani
laki tano