Simu mpya za Samsung kwa mwaka 2026 zina maboresho makubwa kwa simu za madaraja yote
Maboresho makubwa zaidi yammefanyika kwenye utendaji
Hivyo hii hapa ni orodha ya baadhi ya simu za Samsung zinazopatikana hapa Tanzania
Kila siku utajua ubora wake na bei yake hapa nchini
Samsung Galaxy S26 Ultra
Bei ya Samsung Galaxy S26 Ultra ni shilingi milioni 3.8 hasa kwa dar es salaam
Samsung hii inakuja na prosesa mpya aina ya Snapdragon 8 Elite Gen 5
Snapdragon 8 Elite Gen 5 ina pafomansi kubwa kwenye kila idara
Na ufanisi wake wa kukaa chaji ni mkubwa
Boreshwa la ajabu zaidi ni upande wa skrini
Skrini ya samsung galaxy s26 ultra ina uwezo wa kuzuia mtu wa pembeni asione kile unachokiangalia
Inadumisha faragha
Samsung Galaxy 26+
Bei ya Samsung Galaxy S26+ ni shilingi milion 3.2
Ina sifa zote kama za Samsung Galaxy S26 Ultra
Isipokuwa Galaxy S26+ ina kimo cha inchi 6.7
Pia chaji yake kasi ya juu ya kupeleka umeme ni wati 45
Samsung Galaxy S26
Bei ya Samsung Galaxy S26 ni shilingi milioni 2.8
Upande wa betri inatumia betri dogo zaidi kuliko samsung zingine
Ni simu yenye kimo kifupi cha inchi 6.3
Samsung Galaxy Z Trifold
Samsung Galaxy Z Trifold ndio samsung ya gharama zaidi kwa sasa
Bei ya Samsung Galaxy Z Trifold ni shilingi milioni 7.8
Hii simu ina skrini zipatazo tatu
Ukiikunjua skrini zote upana wake unafika inchi 10 sawa na Tablet za walimu
Betri lake lina ukubwa wa mAh 5600
Utendaji wake pia ni mkubwa