Kuna simu mpya za matoleo ya iPhone 17 ambayo apple wameyazinduwa septemba 2025
Kuna kipya lakini si kikubwa sana
Ila kinaweza kukuvuta kuinunua moja iphone za mwaka 2025
Kama una hamu ya upekee wa hizi iphone 17 ukilinganisha na toleo la iphone 16 basi pitia sifa za kila iphone
Hapa kuna sifa muhimu za iphone mpya za matoleo ya:
- Apple iPhone 17
- Apple iPhone 17 Pro
- Apple iPhone 17 Pro Max
- Apple iPhone Air
Apple iPhone 17
Bei ya iPhone 17 kwa Tanzania ni shilingi milioni 3
Ni simu ya kimo cha inchi 6.3 kimo cha wastani
Upande wa mifumo ya memori inakuja na RAM ya GB 8 na ukubwa wa memori GB 256 au 512
Inatumia mfumo endeshi mpya wa iOS 26
Betri yake ni ndogo kwani ukubwa wake ni mAh 3692
Kasi chaji yake ni ya wastani, inapeleka umeme unaofika hadi wati 25
Inakuja na kamera mbili za lenzi upana wa kawaida na lenzi ya upana mkubwa mkubwa sana zote zina 48MP
Apple iPhone 17 Pro
Bei ya iPhone 17 Pro ni shilingi milioni 4 kwa Tanzania
Na yenyewe kimo chake ni inchi 6.3
Ila utendaji wake ni mkubwa zaidi ya Apple iPhone 17
Kwani inatumia chip aina ya Apple 19 Pro
Ukubwa wa betri ni wa wastani kwani ina mAh 3988
Wakati kiwango cha juu cha kuchaji ni wati 25 ambayo sio kikubwa sana
RAM ina ukubwa wa GB 12, huku kamera zikiwa tatu zenye 48MP
Kamera iliyoongezeka ni ya lenzi ya periscope telephoto kwa ajili ya kupiga vitu vilivyo mbali sana na kamera
Apple iPhone 17 Pro Max
Bei ya iPhone 17 Pro Max kwa Tanzania ni shilingi ni milioni 4.5
Ni apple yenye ndefu zaidi kwa sababu kimo chake ni inchi 6.9
Pia ina betri kubwa, kwa matoleo ya USA ni mah 5088, na kwingineko ni mah 4832
Na yenyewe inakuja na kamera tatu kama ilivyo Pro
Utendaji wake ni mkubwa, inatumia chip ya Apple 19 Pro
RAM yake ina ukubwa wa 12GB ukubwa wa memori unaanzia GB 256 hadi 1TB
Kiujumla kilichoongezeka kwenye pro max ni betri na urefu wa simu
Apple iPhone Air
Bei ya iPhone Air ni shilingi milioni 3.7
iPhone Air haina tofauti sana iPhobe 17 Pro
Utofauti wake ni wembamba
Hii ni iphone nyembamba zaidi kama ilivyo kwa samsung galaxy 25 edge
Pia ina betri dogo lenye ukubwa wa mAh 3149
Kwa bahati mbaya ama nzuri toleo hili linatumia laini za eSIM pekee