Kwa mwaka 2024, soko la simu janja yaani smartphone duniani lilitawaliwa na makampuni ya Apple, Samsung, Xiaomi, Vivo na Oppo
Kwa hapa Afrika kampuni ya Samsung inaongoza kwa mauzo ikifuatiwa na Tecno, Apple, Infinix, Huawei na Xiaomi
Kwenye hii post tunaenda kuangalia simu bora duniani kwa mwaka 2024 kwa kuzingatia vigezo vya
- Bei nafuu uwezo mkubwa
- Uwezo wa betri
- Ubora wa kamera
- Muundo wa simu
- Ubora na sapoti ya software
- Na nguvu ya utendaji
Hivyo basi baadhi ya simu zinazoongoza kimauzo kwa sasa hazitokuwepo kwenye hii orodha
Samsung Galaxy S24 Ultra
Samsung Galaxy S24 imekamilika katika idara zote na ndio simu kwa mwaka 2024 kwa mujibu wa maoni mengi
Utendaji wa simu ni mkubwa sababu ya kutumia chip ya Snapdragon 8 Gen 3
Simu hii itakuwa inapokea matoleo mapya android kwa miaka saba mfululizo
Simu ina peni(stylus) kwa ajili ya kutumia kwenye skrini
Inaambatana na mifumo ya akili bandia kama vile kutafsiri sauti inayopiga simu kuwa lugha nyingine kwa maandishi
Kamera zake zote ni nzuri na ubora wa picha haupungui ni mzuri katika mazingira yote yaani mchana na usiku
Ni rafiki kuitumia maana ina miundo wa multitask
Vivo X200 Pro
Vivo X200 Pro ni moja ya simu zenye kamera nzuri sana
Hii simu inaweza kurekodi mpaka video za 8K
Na utendaji wake ni mkubwa maana chip yake ya Dimensity 9400 nguvu yake ni kubwa
Yenyewe inatumia android 15, itapokea matoleo mapya ya android kwa miaka minne mfululizo
Muonekano wake wa Funtouch 15 ni simple na mpangilio wake app ni rahisi kutumia
Simu inaweza kukaa na chaji kwa takribani masaa kumi na tano
iPhone 16 Pro Max
Linapokuja swala la utendaji na kamera, iPhone 16 Pro Max inaweza ikawa inaongoza kwa mwaka 2024
Hii ni simu ya kamera tatu na imekuja na kitufe cha ziada cha kukuwezesha kuwasha kamera kwa haraka
Mfumo wake wa software uko smooth sana na hauna matangazo kabisa
Na simu za iphone hupokea matoleo mapya ya iOS mara kwa mara
Katika majaribio mengi, iPhone 16 Pro Max inakaa na chaji mpaka masaa 18 kwa matumizi ya kawaida
Muundo wake una kamera tatu na ina urefu wa inchi 6.9
Google Pixel 9 Pro XL
Kigezo kikubwa kinachoipa nafasi hii simu kuwa moja wa simu bora ni ubora mkubwa kwenye kamera
Kamera yake inaambatana na mifumo ya Artfificial Intelligence
Kwa mfano, mko wawili na mnataka mtokee kwenye picha moja na hakuna mtu wa tatu wa kuwapiga
Google pixel inaweza kutatua hiyo changamoto kwani inaweza kuunganisha picha na kuonekana kama mmepiga kwa pamoja
Hili ni eneo moja wapo ila pia ubora upo mwingi katika maeneo mingine mengi
Moja wapo ni kuwa itapata matoleo mapya ya Android kwa miaka 7 mfululizo
Nothing Phone 2A
Bei ya Nothing Phone 2A inakaribia laki nane
Ubora wa simu unaachwa mbali na simu zilizopo hapa, ila ina kitu kimoja kikubwa sana cha kuzingatia
Ni kwamba bei yake inakupa vitu vingi vinavyopatikana katika matoleo mengi yaliyopo hapa
Karibu simu bora nyingi bei zake zinaanzia milioni mbili kwenda juu
Wakati huo nothing phone 2A inakupa simu inayopokea android mpya kwa miaka 3
Kioo chake ni kizuri kina hdr10+ na refresh rate ya 120Hz
Betri yake inaweza kudumu kwa takribani masaa 16 kwa matumizi ya kawaida
Oppo Find X8 Pro
Oppo Find X8 Pro imetoka mwezi Oktoba 2024
Hii inatarajiwa kuwa itapokea matoleo mapya ya android kwa kipindi cha miaka miaka minne
Muonekao wake ColorOS 15 hauna tofauti sana na mionekano ya simu zingine
Ila kuna vitu vya ziada vinavyoambatana na hii simu
Kwa mfano uwezo wa kufupisha taarifa ndefu na kuwa fupi na pia inabadilisha maandishi kuwa matamshi
Na vitu vingine ambavyo kwa sasa ni vya kawaida ikiwemo Gemini
ZTE Nubia Red Magic 10 Pro
ZTE Nubia Red Magic 10 Pro ndio simu yenye betri kubwa zaidi kwa mwaka 2024
Hii ni simu janja ambayo imeundwa kwa ajili ya kucheza magemu
Red Magic 10 Pro inakaa na chaji karibu masaa kumi na nane kwenye matumizi ya kawaida
Kama ukiwa unacheza gemu wakati wote, chaji itaisha baada ya masaa kumi na tatu
Hii simu imetengenezewa mifumo ya kupooza simu hivyo hautoona simu ikipata joto jingi kupitiliza
Kitu kimoja ambacho kipo nyuma ni kutokupata matoleo mapya ya Android kwa muda mrefu
Maana inapokea toleo jipya mara moja tu yaani itapata android 16 pekee
Huawei Mate XT Ultimate
Huawei Mate XT Ultimate sio bora sana kama kisifa kama simu zingine
Kinachoipa sifa kubwa ni muundo wake
Hii ni simu skrini tatu, yaani ni simu ya kujikunjua mara mbili na kuifanya skrini kuwa kubwa kama tablet
Huu muundo wa Tri-Fold ni wa kipekee kwani mpaka sasa hakuna simu ya muundo huu
Siku hizi hakuna mabadiliko makubwa ya simu
Ila Huawei Mate XT Ultimate imekuja kitofauti sana
Honor Magic V3
Honor Magic V3 ni simu ya kujikunja na ina nguvu ya kiutendaji
Kama ilivyo kwa simu zingine, AI (Akili mnemba) imechukuwa nafasi kubwa upande wa software
Moja ya kitu utakachokuta ni hiki kinachoitwa Face to Face translation
Ambayo inampa nafasi mtumiaji kutafsiri lugha ya mzunguzaji anayeongea lugha usiyoijua
Utendaji wake ni mkubwa kwa sababu ya kutumia processor ya Snapdragon 8 gen 3
Kamera zake zinapiga picha vizuri ukilinganisha na baadhi ya folding zingine
Google Pixel 9 Pro Fold
Katika simu za fold nzuri na bora kwa mwaka 2024, Google Pixel 9 Pro Fold inaongoza
Kwa nini
Hii ni simu ambayo imekamilika kila idara na muundo wake ni simpo sana na mzuri
Software itakuwa inapata maboresho ya Android kwa miaka 7
Kamera zake tatu zote ni nzuri na zinaweza kurekodi video za 4K
Kulingana na muundo wake, software inakupa nafasi ya kutumia apps zaidi ya mbili kwa wakati mmoja
Na yenyewe inaambatana na mifumo mbalimbali ya AI ikiwemo Gemini
OnePlus 12R
OnePlus 12R ni simu ya daraja la kati inayouzwa chini ya milioni moja
Ufananishi wa bei na aina ya sifa ilizoneza unaweka simu katika kundi la simu bora 2024 duniani
Hii simu ina ufanano na Samsung Galaxy A55
Ila samsung A55 inazidiwa kwa mbali sana kwenye utendaji na ubora wa skrini
OnePlus 12R itapata matoleo mapya ya android kwa miaka mitatu
Ubora wa picha wa kamera zake mbili ni wa kuvutia hasa kwenye usahihi wa rangi na kiasi kidogo cha noise nyakati za usiku
Poco F6
Poco F6 ni simu yenye utendaji mkubwa
Inatumia chip ya Snapdragon 8 Gen 3 ambayo utaikuta kwenye Samsung Galaxy S24 Ultra
Lakini bei ya Poco F6 ni ndogo ambayo ni chini ya laki tisa, japo poco f6 haina ubora kama samsung
Hii simu itapokea matoleo ya Android kwa miaka mitatu na inatumia mfumo HyperOS
HyperOS haina tofauti sana MIUI ambao kwa kweli ulikuwa una changamoto nyingi
Ila mfumo wake kamera ni wa kawaida sana
Asus Rog Phone 9
Asus Rog Phone 9 ni simu nyingine inayomlenga mpenda magemu sana
Ukilinganisha na simu zingine haina vitu vingi vikubwa sana ila ina mfumo mzuri wa kupooza simu kupata joto
Na pia betri lake ni kubwa kwa kiwango cha 5800mAh
Hivyo hii inakaa na chaji masaa mengi sana
Simu ina skrini nzuri kutokana na refresh rate kubwa inayoenda hadi 185Hz
Yaani ni kama skrini ya kompyuta katika magemu
Samsung Galaxy Z Flip6
Samsung Galaxy Z Flip6 ni simu kufunua na kufunika kwa mtindo wa kujikunja
Katika matoleo ya simu za ku-flip hili ni toleo zuri kwa mwaka 2024
Lakini haina ubora mkubwa sana wa kuzipita simu zingine
Maana hata kwenye kamera kuna vitu ina vikosa
Ina skrini yenye hdr10+ hivyo ina kina kikubwa cha rangi
Betri yake sio kubwa ukilinganisha na simu zingine zilizotajwa hapa
iQOO 13
iQOO 13 ina muundo simpo na ina kamera tatu aina ya ultrawide, wide na telephoto
Chaji yake inadumu kwa masaa yapatayo kumi na nane ukiwa katika matumizi ya kawaida
Katika kucheza gemu muda wote simu itaisha chaji baada ya masaa 11
Hii inatokana na betri lake kuwa kubwa (6100 mAh)
Utendaji wake una nguvu inayotokana na chip ya Snapdragon 8 Elite yenye utendaji mkubwa wa zaidi ya 45% ya Snapdragon 8 gen 3
Simu hii inakuja na android 15 na itapokea matoleo ya android kwa miaka minne
Xiaomi 15
Xiaomi 15 imetoka mwishon mwa 2024 mnamo mwezi oktoba
Inatumia processor mpya ya Snapdragon 8 Elite hivyo utendaji wake ni mkubwa
Ina kamera zipatazo tatu na zinaweza kurekodi mpaka video za 8K
Inasapoti chaji ya wati 90 hivyo betri inawahi kujaa ndani ya muda mfupi
Mfumo endeshi uliopo kwenye simu ni Android 15