Mwishoni mwaka 2021 simu ya redmi note 11 pro plus(pro+) iliingia sokoni.
Sifa kubwa Redmi note 11 pro+ 5g ni kioo kikali chenye uwezo wa kuonyesha rangi za vitu kama zinavyoonekana kwenye mazingira halisi.
Mapungufu machache ya simu ya redmi note 11 pro+ 5g yanazibwa na ubora wa simu kwenye nyanja karibu zote.
Ukitizama taarifa za simu kwenye jedwari utakubariana na mtazamo wa hii post
Sifa za Redmi note 11 pro+ 5g
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Super AMOLED, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS 2.2, 128GB,256GB na RAM 8GB,6GB |
Kamera | Kamera taut
|
Muundo | Urefu-6.67inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 800,000/= |
Upi ni ubora wa simu ya Redmi note 11 pro+ 5g?
Ubora wa redmi note 11 pro+ 5g unapatikana kwenye display.
Display ya hii inaundwa kwa teknolojia hdr iliyoboreshwa
Hdr huboresha muonekano wa rangi za picha unaoendana na jinsi jicho la mwanadamu linavyoona hiko kitu
Utendaji wa simu ni wa juu kiasi cha kucheza gemu kubwa kiurahisi.
Memori yake inasafirisha data kwa spidi ya haraka
Ubora mkubwa wa redmi iliyopo hapa ni chaji inayojaza simu kwa dakika chache kama utakavyoona baadae
Kamera ya simu inapiga picha za ubora wa aina tatu.
Ubora huu wa kamera haupo kwenye Redmi note 11 pro 5g
Network
Ukiwa eneo lenye 2G, 3G, 4G na 5G network ya simu itakamata kiufasaha
Upande wa 4G simu ina network bands 22
Tanzania kuna network bands tano pekee.
Hivyo laini zote za mitandao ya simu zinakubali intaneti ya 4g kwenye redmi note 11 pro plus 5g
Bands za mtandao wa 5G zipo 13
Ni bands za masafa ya kati zenye spidi ya wastani
Na bands za 5g za masafa ya chini yenye spidi zinazokaribiana na mtandao wa 4G
Ubora wa kioo cha Redmi note 11 pro+ 5g
Simu ya redmi note 11 pro+ 5g inatumia kioo cha Super amoled.
Kioo cha super amoled husufika kuonyesha rangi nyeusi tiiii(halisi)
Hautaona uweupe kwenye rangi nyeusi
Uangavu wa kioo cha redmi note 11 pro+ 5g unafikia 1200nits
Kiwango hiki kinawezesha screen kuonyesha vizuri ukiwa kwenye jua
Ukicheza gemu utafurahia kwa sababu refresh rate inaweza kufika 120Hz
Hivyo simu inakuwa nyepesi na laini kutachi na ku-scroll
Picha ambazo sceen inaonyesha ni nzuri kwa sababu kioo kina HDR10
HDR10 hufanya rangi za vitu kuonekana kwa uharisia kwa sehemu kubwa hata vikiwa vimepigwa picha kwenye mwanga mdogo
Pia resolution yake ni nzuri ya 1080 x 2400 pixels
Nguvu ya processor ya Dimensity 920
Nguvu ya processor iliyomo kwenye redmi note 11 pro+ 5g ina utendaji wenye nguvu.
Chipset ya dimensity imeundwa na GPU ya Mali-G68 MC4
GPU ya Mali G68 MC4 inaweza kucheza gemu ya simu ya Armajet 2020 kwa kasi 60fps kwa resolution
Hilo linasababibishwa na core mbili zenye nguvu kubwa kuwa na kasi kubwa.
Hata core ndogo zimeboreshwa spidi hivyo utendaji umeongezeka.
Uwezo wa core kubwa
Core ndogo mbili kila moja ina kasi ya 2.4GHz
Na core zote zinatumia muundo wa Cortex A78.
Ni muundo uliotumika kwenye core kubwa za Snapdragon 695 5g
Lakini MediaTek Dimensity 920 ina nguvu kubwa kuliko Snapdragon 695 5g iliyotumika kwenye simu ya Oppo A96 5G
Kwenye geekbench Dimensity ina alama 791 wakati snapdragon ina 702
Hii inatokana na Dimensity 920 kuwa na clock spidi ya kasi zaidi ya snapdragon
Uwezo wa core ndogo
Core ndogo zipo sita na kila ina spidi ya 2.0GHz
Core zote zinatumia muundo wa Cortex A55
Cortex A55 ya Dimensity ina nguvu zaidi ya snapdragon 695
Kwa sababu kuna ongezeko la clock spidi kwenye processor ya dimesnity.
Kuna vitu vingi vinatumika kujua nguvu ya processor.
Pitia linki hii chini kujua namna ya kutazama processor za simu.
Jinsi ya kujua uwezo wa processor za simu
Uwezo wa betri na ukaaji wa chaji
Moja ya kitu kinachostahajabisha kuhusu hii simu ya xiaomi ni spidi ya kuchaji.
Simu ya redmi note 11 pro+ 5g inaweza kujaa chini ya dakika 20 kwa asilimia 100.
Gsmarena wameshaijaribu hii chaji katika uchambuzi wao
Kwa mujibu wa gsmarena inachukua dakika 16 tu kujaza betri ya redmi note 11 pro+ 5g
Kumbuka betri yake ina ukubwa wa 5000mAh
Ustahamilivu wa simu kutunza chaji ni masaa 105
Ukiwasha intaneti bila kuzima itachukua masaa karibu 12 betri kuisha
Ni redmi note 11 pro+ 5g ni simu inayokaa na chaji muda mrefu lakini sio kwenye intaneti
Ukubwa na aina ya memori
Redmi note 11 pro+ 5g inatumia memori za UFS 2.2
Usafirishaji wa data ni mkubwa kwa aina hii ya memori ukilinganisha na eMMC
Simu mojawapo ya eMMC ni samsung galaxy a22
Ram zake ni za LPDDR5
Usafirishaji wa data wa LPDDR5 unafikia 6400Mbps.
Ni kasi kubwa kuliko LPDDR4x inayoutmika kwenye simu nyingi kwa sasa
Ukubwa memori
Kuna redmi note 11 za aina tatu upande wa memori
- 128GB ROM, 6GB RAM
- 128GB ROM, 8GB RAM
- 256GB ROM, 8GB RAM
Bei za hii simu zinatofautiana kulingana na ukubwa wa memori
Uimara wa bodi ya Redmi note 11 pro+ 5g
Muundo wa bodi ya redmi note 11 pro+ 5g kudumu muda mrefu.
Kwa sababu bodi upande nyuma ina glasi.
Na upande wa display kuna ulinzi wa kioo cha gorilla 5
Kioo cha Gorilla 5 kinastahamili kupasuka simu ikianguka kwa urefu wa mita 1.2(kwa mujibu wa gorill wenyewe)
Unaweza kuweka screen kuongeza ulinzi wa kioo lakini huwa haina umuhimu
Simu ni nzito kidogo
Ina uzito wa 204 gramu
Ubora wa kamera
Katika kamera tatu za redmi note 11 pro+ 5g hakuna kamera yenye OIS.
Apperture kamera inapitisha mwanga wa kutosha na ina ukubwa wa f/1.9
Maana ya apperture imelezewa hapa simu zenye kamera kali
Ubora wa picha
Kmaera ya note 11 pro plus inatoa picha safi sana nyakati za sana.
Rangi za vitu zinatokeo kama zinavyoonekana kwenye mazingira yake
Exposure na contrast ya kamera inatofautisha kwa usahihi mkubwa rangi za vitu mbalimbali na mwanga kiujumla
Nyakati za usiku vitu vinaonekana kwa ubora na noise ndogo sana.
Ukipata nafasi,
Zitazame picha za gsmarena zilizopigwa kwa kutumia simu hii ya redmi
Ubora wa video
Kamera ya redmi note 11 pro+ 5g inaweza kurekodi video za aina tatu
Na spidi ya kurekodi video inafikia mpaka 960fps
Hizi ni ubora wa video na spidi ya kurekodi
- 720p(HD), 960fps
- 1080p(Full HD), 30fps, 60fps na 120fps
- 3840p(4k), 30fps
Kuelewa maana ya fps na umuhimu wake soma posti hii : fps ya oppo a96 5g
Ubora wa Software
Redmi note 11 pro+ 5g ni simu ya android 11 yenye software ya MIUI 12.5
MIUI ina toleo jipya la MIUI 13
Toleo ambalo xiaomi wanadai inaongeza ufanisi wa matumizi ya betri
Zipo taarifa zinadai simu hii inapokea toleo jipya la android 12 na MIUI 13
Bei ya Redmi note 11 pro+ 5g Tanzania
Bei ya redmi note 11 pro+ 5g kwa Tanzania inaweza kuzidi 800,000/=
Kama unanunua kwa kuagiza aliexpress utaipata kwa bei nafuu kulingana na ukubwa wa memori.
Hizi hapa bei zake kwa baadhi ya store aliexpress.
- 128GB na 8GB inauzwa shilingi 791,928.26
- 256GB na 8GB inauzwa shilingi 885,959.01
Washindani sahaihi wa hii simu zenye processor Snapdragon 865
Simu kama Vivo V23 5G inaweza kushindana na redmi hii
Lakini vivo v23 5g inapigwa kirahisi upande wa kamera
Yapi Madhaifu ya Redmi note 11 pro+ 5g
Ksoro kubwa ya redmi note 11 pro+ 5g ni kukaa na chaji muda mfupi ukiwa unatumia intaneti.
Unaweza ukasema ni kwa sababu ya processor na kioo
Lakini hali iko tofauti kwenye simu kama iPhone 13 Pro Max
iPhone 13 Pro Max inakaa na chaji kumi nane ukiwa unatumia intaneti
Na apo processor ya iphone ina nguvu kuliko processor ya simu yoyote
Neno la Mwisho
Simu ya redmi note 11 pro+ 5g ni simu yenye kamera nzuri.
Ina utendaji wenye nguvu
Chaji yake inapeleka umeme unaojaza simu ndani ya myda mchache.
Simu inakaa na chaji muda mrefu vilevile japo si sana.
Hivyo ni simu ya kununua na bei yake ni nafuu kwa kutazama sifa zake
Pia kwa kuangalia sifa za simu zingine zenye uwezo sawa.