Kwa sasa Oppo Find X9 Pro ndio simu inayotunza chaji zaidi duniani
Hivi ndivyo Oppo Find X9 Pro inavyozizidi simu zingine kwenye ukaaji wa chaji
Kwanza kabisa betri yake ni aina ya silicon carbon
Pili, ni betri yenye ukubwa wa mAh 7500
Hili betri linaifanya simu kudumu na chaji mpaka masaa 21 kwenye matumizi ya kawaida ya kila siku

Tatu, kwenye kuperuzi intaneti siku nzima simu inadumu hadi masaa 22
Upande wa kucheza gemu masaa yote mfululizo, betri inadumu hadi masaa 13
Ila utata wa hii upo kwenye bei
Hii ndio bei yake
Bei ya Oppo Find X9 Pro Tanzania
Oppo Find X9 Pro kwa Tanzania bei yake ni shilingi milioni tatu (3,000,000)
Hii ni simu ya daraja la juu inayochuana na Xiaomi 17 Pro, Samsung Galaxy S25 Ultra, Vivo X300 Pro na iPhone 17 Pro
Hivyo sifa zake ni kubwa sana
Kila kipengele kuanzia utendaji, kamera, software, memori, network na uimara wa bodi ni levo nyingine
Kwa maana bei yake haiwezi kuwa sawa na simu za madaraja ya kati
Kama una shaka endelea kusoma baadhi ya sifa zake hizi hapa chini
Utendaji
Simu inatumia prosesa ya Mediatek Dimensity 9500
Hii prosesa ina nguvu kubwa ya kusuma kila aina ya app hata ambazo zinazohitaji nguvu kubwa
Kweye app ya kutest nguvu za prosesa ya geekbench inaonyesha yafuatayo
Inaweza kufungua kurasa(pages) 288 kwa sekunde
Pia inaweza kuchakata picha 107 kwa sekunde pasipo kukwama
Hii ni tofauti na uwezo wa prosesa ya Mediatek dimensity 7300
Mediatek dimensity 7300 imetumiwa na simu ya Tecno Camon 40 Pro
Tecno Camon 40 Pro inaweza kufungua kurasa 55 kwa sekunde
Ubora wa Kamera
Hii ina kamera zipatazo tatu
Kamera zina lenzi aina ya wide, ultrawide na periscope telephoto
Kamera zake mbil zina ukubwa wa megapixel 50 na moja ina 200MP
Ubora na mfumo mzima wa kamera ni balaa
Kamera zinatoa picha nzuri kwenye mazingira yote
Usahihi wa rangi wa vinavyopigwa rangi ni kiwango kikubwa
Kamera inabalansi vizuri na kuepuka kuathiriwa na mwanga mwingi
Ukubwa na aina ya memori
Unajua kuwa ziko za aina tofauti na zinatofautiana kasi ya kuhifadhi vitu?
Oppo Find X9 Pro inatumia mfumo wa memori wa UFS 4.1
Huu mfumo unasafirisha data kwa kasi inayofika 41Gbps
Yaani kama kama unakopi kitu cha 4GB simu inaweza kukopi ndani ya sekunde chache
Mbali na hayo simu ina matoleo tofauti kwenye ukubwa wa memori
Inaanzia GB 256 hadi TB 1, na zote zina RAM ya GB 16
Uimara wa bodi
Bodi ya Oppo Find X9 Pro imeundwa na uwezo wa waterproof
Ina cheti cha IP68/IP69
Hii inamaanisha maji hayaingia ndani ya simu hata ikizama kwenye kina kikubwa cha mita 1.5
Hilo linawezekana ndani ya muda wa nusu saa
Ina skrii protekta aina ya Corning Gorilla Glass Victus 2
Ambayo ina uwezo wa kuzuia skratchi vitu vya ncha kali kama sindano
Pia ni himilivu simu inapoanguka kwenye kina cha mita 2
Ubora wa software
Simu hii inakuja na mfumo endeshi wa andtoid 16
Na itakuwa inapata matoleo mapya ya android kwa muda wa miaka 5
Hivyo itapata hadi Android 21
Maboresho ya muda mrefu huongezea thamani kwa muda mrefu
Na mambo mengine ni matumizi ya AI ambayo yameshika hatamu kwa sasa
Neno la mwisho
Kama unataka simu inayotunza chaji kuliko zingine basi simu hiyo Oppo Find X9 Pro
Ila unapaswa ukumbuke ni simu ya bajeti kubwa
Kama bajeti yako ni ndogo inabidi utafute simu mbadala
Zipo infinix na Tecno za bei ndogo zenye betri kubwa ila sifa sio za ubora mkubwa