Unaiona hii picha ya simu mbili za toleo la Apple iPhone 14 Pro Max
Moja ya kati hizi iphone ni feki.

Je kwa kutazama unaweza kuijua ipi ni iphone original kati ya hizi simu mbili?
Kama umeshindwa nitakuonyesha njia nyepesi kabisa za kuijua iphone halisi
Hizi njia zimegawanyika katika sehemu zifuatazo ambazo unaweza kuitumia moja wapo
Njia hizo inahusisha.
- Muonekano wa iphone
- Software za iphone
- Kutumia apps nje ya iphone
- Kutumia njia za online
Angalizo
Kabla hujaamua kununua iphone, jitahidi kufuatilia taarifa za hizo katika hasa kuhusu prosesa, memori, aina ya kamera, kioo, tabia za mfumo endeshi(iOS) na pia muundo halisi wa iphone origino
Ukielewa simu husika baada ya kufuatilia video mbalimbali na sifa za simu unaweza kuigundua iphone feki bila hata kuitazama kiundani
Hivyo kwa njia hizi chache utaigundua iphone feki mapema tu.
Muonekano wa iPhone
iPhone origino na feki mara nyingi hutofautiana katika muonekano hasa rangi ya bodi, muonekano wa skrini na pia hata kamera
iPhone feki rangi zake hazikolei kama ilivyo origino
Na muonekano wa logo ya apple vilevile haviendani
Kwa mfano picha ya juu mwanzoni, logo ya apple ya simu ya kwanza inang’aa kuliko kuliko ya upande wa kulia ambayo imekolea weusi
Ya kushoto ni feki.
Pia tazama hii picha ya iphone 17 pro max feki na original

Ya kulia ni feki hata logo ya apple haionekani vizuri
Pia muonekano wa kamera wa iphone feki hufanana
Kamera zote lenzi zake huwa na ukubwa sawa tofauti na iphone orijino ya upande wa kulia picha ya kwanza na upande wa kushoto kwenye picha ya iphone 17 pro max
Muonekano wa skrini
Skrini inakupa utofauti wa wazi kati ya iphone orijino na feki
Itazame hii picha

Na kisha tazama upande fremu kushoto na kulia, juu na chini
Kwenye simu feki(kulia) kuna fremu ya rangi nyeusi pana inazunguka skrini
Hivyo skrini haikavi eneo lote hasa upande wa chini fremu ni pana
Wakati simu ya kulia(iphone orijino) skrini imekava kioo chote
Na upana wa fremu yenye rangi ni mwembamba na upo sawa kwenye pande zote
Software za iPhone
iPhone inatumia mfumo endeshi wa iOS na sio android
Hivyo apps za mfumo endeshi wa android hazifanyi kazi kwenye iPhone
Kwa mfano app ya kupakua apps mbalimbali kwenye iPhone huitwa App store
App store haipatikani kwenye android
Simu feki huweka mfano wa icon ya app store lakini huwa haifanyi kazi huwezi kuinstall app

Pia kwenye ya utiltity za simu feki utakuta app ya google play store
Kutumia apps za kutest simu
Moja ya njia nyingine rahisi zaid ya kugundua iphone feki ni kwa kutumia apps za kutest prosesa
Data za prosesa sio rahisi kuzichezea hasa spidi ya prosesa
App moja wapo nzuri kwa kazi hii ni CPU Z na geekbench
Ila inabidi ujue prosesa na spidi yake ya juu
Kwa mfano iphone 16 pro max prosesa yake ni Apple A18 Pro
Na spidi yake ya juu ni 4.05GHz na 2.42GHz na idadi ya core zipo sita
Taarifa hizi unaweza zipata kwenye gsmarena.com
CPU Z itakuonyesha taarifa zote na spidi inavyoenda kwa wakati kwa kila core(huandikwa cpu 0, cpu 1 nk)

Simu feki huwa kasi ya cpu haiwezi kuwa kubwa
Na huwa ndogo na huwa haibadiliki badiliki
Kwa hiyo spidi haiendani na cpu ilivyoainishwa basi jua hiyo simu feki