Samsung Galaxy S10 na iPhone 11 zilitoka rasmi mnamo mwaka 2019
Wakati zinatoka bei ya samsung galaxy s10 na iphone 11 zilikuwa zinazidi milioni moja
Ila baada ya miaka mitano tangu zilipotoka bei zake zimeshuka na nyingi ni used
Kwa sasa Samsung Galaxy S10 inauzwa kwa shilingi laki nne na elfu hamsini
Wakati iPhone 11 ya GB 64 unaipata kwa shilingi 550,000(laki tano na elfu hamsini)
Bei zinavutia ila swali la msingi je ubora wa samsung s10 na iphone 11 unaendana na wakati uliopo ikizingatiwa kuna mabadiliko makubwa ya teknolojia.
Utapata hilo jibu kwenye hii post katika vipengele vitano
Nguvu ya utendaji
Kujua uwezo wa simu kiutendaji inakupasa ujue aina ya processor iliyotumika kwenye kifaa husika
Samsung Galaxy S10 inatumia processor ya Snapdragon 855 wakati apple iphone 11 inatumia chip ya Apple A13 Bionic
Snapdragon 855 ina nguvu ya wastani kwa standard za sasa
Ila ipo tofauti kidogo japo kimuundo inaendana na processor iliyotumika kwenye simu mpya ya Infinix Hot 50 Pro Plus
Kwa ufupi chip inacheza gemu nyingi tena kwa fremu nyingi zinazofika 60fps
Gemu ikicheza kwa fremuĀ nyingi inakuwa na muonekano mzuri kama vile unarekodi video
Hata Snapdragon 855 inapitwa na matoleo mengi ya simu mpya za daraja la kati zilizotoka hivi karibuni
Hali ni tofauti kwa processor ya iPhone 11, kwani hakuna processor ya daraja la kati inayoifikia Apple A13 Bioni mpaka sasa
Kitu kinachoifanya iphone 11 kuendelea kuwa shindani kwa simu nyingi mpya
Maboresho ya Software
Wakati iphone 11 ilipotoka rasmi, mfumo wake endeshi ulikuwa ni iOS 13
Kwa sasa mfumo mpya wa iphone 16 ni iOS 18 ambao unaambatana na mifumo ya akili bandia (AI)
iPhone 11 inapata toleo la iOS 18 hivyo simu inapata teknolojia mpya za software
Upande wa Samsung Galaxy S10 ilikuja na Android 9, toleo la sasa la Samsung Galaxy S24 ni Android 14, pia itapata Android 15
Bahati mbaya ni kwamba Samsung Galaxy S10 inapokea mwisho toleo la Android 12
Hii ina maanisha mifumo mipya ya faragha iliyopo kwenye Android 15 haitopatikana kwenye Samsung Galaxy S10
Maboresho mapya ya mifumo endeshi hutunza thamani ya simu
Na inaipa simu uwezo wa kupata maboresho ya teknolojia mpya na kuimalisha usalama wa data zako kwenye simu
Ukubwa na uwezo wa betri
Ukubwa wa betri ya Samsung Galaxy S10 ni 3400mAh
Ni kiwango kidogo ukilinganisha na betri za siku hizi ambazo huwa na 5000mAh
Wakati ya iPhone 11 ni 3110mAh, pia ni ndogo vilevile
Kasi ya Galaxy S10 inasapoti wati 15, iphone 11 inasapoti hadi wati 18, ambapo kwa sasa simu nyingi kubwa husapoti hadi wati 120
Betri ya samsung ikiwa mpya inakaa na chaji hadi masaa 10 ukiperuzi intaneti muda wote
Na ya iphone 11 inakaa na chaji hadi masaa 15 ukiperuzi intaneti muda wote
Hata hivyo kwa sasa hizi simu nyingi ni used hivyo ubora wa betri lazima upungue
Na ni ngumu kupata ikiwa mpya kwa sasa
Ubora wa kamera
Simu zote za Samsung Galaxy S10 na iPhone 11 zinatoa picha nzuri
Ubora wa picha unaendana na matoleo mengi mapya ya daraja la kati
Hizi simu zinaweza kurekodi mpaka video za 4K kwa kiwango cha 60fps
Galaxy S10 ina kamera tatu ambazo ni lenzi za wide, ultrawide na telephoto
Na zote zina megapixe 12 ambayo ndio standard hata mpaka sasa
iPhone 11 ina kamera ambazo ni za wide na ultrawide
Ulinganishi na simu za madaraja ya kati
Kwenye hiki kipindi cha miaka mitano mpaka sita simu mpya zimeingia sokoni
Simu za sasa za madaraja kuna ambazo ni bora kuliko matoleo ya daraja ya juu ya miaka iliyopita
Hizi ni baadhi ya simu unazoweza kununua kwa sasa badala ya kununua Samsung Galaxy S10 au iPhone 11 used
Samsung Galaxy A35
Samsung Galaxy A35 imetoka mwaka 2024
Ni simu inayotumia mfumo endeshi wa android 14 na itakuwa inapokea matoleo mapya kwa miaka minne
Processor yake ina nguvu ya kiutendaji na ufanisi mkubwa wa utunzaji wa chaji kuliko Samsung Galaxy S10
Pia inapiga picha vizuri japo inarekodi video za 4K kwa kiwango cha 30fps
Betri lake ni kubwa na chaji yake inapeleka umeme wa wati 25 ambayo hujaza betri kwa haraka
Xiaomi Redmi Note 14
Xiaomi Redmi Note 14 imetoka mwezi septemba mwaka 2024
Inatumia processor yenye nguvu ya Mediatek dimensity 7025
Inakuja na Android 14 japo haijaainishwa kupokea android za mbele
Betri yake ni kubwa na inaweza kupokea chaji ya kasi ya wati 45
Hivyo betri inawahi kujaa
Kuna matoleo mengi yanayoweza kuwa mbadala
Neno la mwisho
Uchaguzi ni wako kuchagua simu ipi sahihi ya kununua
Kitu kimoja cha nyongeza sio vitu vote ambavyo simu za madaraja ya kati zimeipita hii simu
Moja ya kitu ambacho kinakosekana ni kwenye iphone na samsung hizi ni kukosekana kwa mtandao wa 5G
Ila iPhone 11 bado ni simu shindani zaidi ukilinganisha na Samsung Galaxy S10