Simu mpya za Google Pixel hupatikana kwa bei kubwa ambayo kwa Tanzania ni wachache wanayomudu
Simu za google pixel hutengeneza simu za madaraja ya juu kama uonavyo iPhone
Hivyo katika hiii orodha ya simu za bei rahisi za google pixel utakutana na simu used na sio mpya
Na used zenyewe ni matoelo ya zamani japo mengi yana ubora wa kushindana kwa nyakati za sasa
Simu zote zilizopo hapa zinauzwa chini ya laki tano
Fuatalia uone ipi ina sifa zitakazokidhi mahitaji yako kwa wakati huu na ujao
Google Pixel 4
Google Pixel 4 bei yake ni laki nne(400,000) na ilitoka rasmi mwaka 2019 ikiwa na Android 10
Toleo la mwisho Android simu itakayopokea ni Android 13
Ina kamera mbili zinazoweza piga video za 4K na zinatumia ulengaji wa dual pixel pdaf
Utendaji wake sio mkubwa kwa viwango vya sasa kwani inatumia processor ya Snapdragon 855
Changamoto utaipata upande wa betri kwani ina betri dogo
Ukubwa wa betri ni mAh 2800 na haizidi masaa 10 ukiwa unatumia simu muda wote mpaka chaji kuisha
Google Pixel 4a
Bei ya Google Pixel 4a ni shilingi 400,000 kama ilivyo kwa mtangulizi
Ilitoka mwaka 2020
Na yenyewe inapokea mpaka toleo la Android 13
Betri yake sio kubwa kwani ina mAh 3140 na kasi ya chaji yake ni wati 18
Inakuja na kamera moja na inaweza kurekodi video za 4K
Utendaji wake ni wa wastani sio mkubwa ukilinganisha na matoleo ya kati ya miaka hii
Google Pixel 5a
Bei ya Google Pixel 5a ni shilingi 500,000(laki tano) ni simu za awali za pixel kuwa na 5G
Utendaji ni wastani japo inaweza kufungua vitu vingi
Na simu inayokuja na mfumo wa eSIM
Ina kamera mbili na inaweza kurekodi video za 4K kwa kiwango cha 60fps
Betri yake ni kubwa kiasi ambayo ni 4680mAh
Ni sehemu yenye waterproof ya Ip67 ila hakuna uhakika kama waterproof itaendelea kuwepo kama simu iliwahi kufunguliwa
Google Pixel 3 XL
Google Pixel 3 XL ina miaka takribani minane tangu ilipotoka
Toleo la android la mwisho simu kupokea ni Android 12
Ina kamera moja tu inayoweza pia kurekodi za 4K
Ina utendaji wa wastani kwa sababu ya kutumia chip ya Snapdragon 845
Betri yake ina ukubwa mAh 3430 hivyo sio betri kubwa
Google Pixel XL unaweza ipata kwa shilingi 360,000
Google Pixel 3a
Google Pixel 3a ilitoka mwaka 2019 na inauzwa kwa kiasi cha shilingi 280,000
Ni simu inayokuja na RAM ya GB 4 na utendaji wake sio mkubwa kihivyo
Hii simu inapokea mpaka Android 12 hivyo android za mbeleni hutopata
Betri yake na yenyewe sio kubwa ina mAh 3000
Simu ina kamera moja tu na inaweza kurekodi video za 4K
Inasapoti laini za eSIM
Google Pixel 3
Google Pixel 3 inauzwa kiasi cha shilingi 300,000
Na ilitoka mwaka 2018 hivyo ina miaka saba tangu itoke
Hii simu ina kamera moja ila ina uwezo kuvutia
Kwani inaweza kurekodi video za full hd kwa kiwango cha fps 120
Ila betri yake ni dogo kwani mAh 2915
Na yenyewe ina waterproof ya IP68
Google Pixel 6a
Iwapo matoleo ya awali hayajakuridhisha basi Google Pixel 6a ni mbadala sahihi zaidi
Inauzwa shilingi laki tano (500,000)
Simu inakuja na kamera mbili huku kamera mbili na zinaweza kurekodi video za 4k kwa kiwango cha 60fps
Utendaji wake ni mkubwa kwani inatumia chip ya Google Tensor
Betri yake ni kubwa kiasi kwani ina mAh 4410mAh
Kasi ya chaji yake ni wati 18