Tecno Spark 40 Pro imewasili!
Mwezi Julai 2025, Tecno imezindua rasmi toleo jipya lenye nguvu na muonekano wa kisasa zaidi.
Spark 40 Pro inakuja na maboresho makubwa katika maeneo manne muhimu, ikizidi mbali uwezo wa Tecno Spark 30 Pro ya mwaka 2024.
Ni kweli, bei yake imepanda kidogo ukilinganisha na mwaka uliopita.
Lakini tofauti ya uwezo na teknolojia kati ya hizi simu mbili ni kubwa kiasi kwamba utaona thamani yake mara tu ukizifahamu zote.
Bei ya Tecno Spark 40 Pro
Tecno Spark 40 Pro ya GB 128 na RAM ya GB 8 inauzwa shilingi laki nne (400,000)
Matoleo yote yanakuja na RAM ya GB 8
Maana kuna ya GB 256
Hivyo utofauti mkubwa ni saizi ya memori pekee
Kipengele hiki cha Spark 40 kinafanana na Spark 30
Sifa za Tecno Spark 40 Pro
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | AMOLED, Refresh rate:144Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS 2.2,256GB,128GB na RAM 8GB |
Kamera | Kamera MOJA
|
Muundo | Urefu-6.78inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 400,000/= |
Uwezo wa network
Tecno Spark 40 Pro inasapoti mtandao wa 4G
Na unakupa nafasi ya kutumia laini mbili
Ila hautopata mfumo wa laini za eSIM kwa sababu haisapoti
Kasi yake ya kudownload inafika 650Mbps kama mtandao upo vizuri
Ila hii simu haina 5G
Ubora wa kioo
Simu ina kioo angavu aina ya Amoled
Amoled huwa na kina kikubwa cha rangi
Hivyo vitu kwa rangi zilizokolea na zenye uhalisia kwa sehemu kubwa
Ina refresh rate inayofika Hz 144
Hii inafanya kila mguso kuwa mlaini na wa haraka
Uangavu wake unafika nits 1600
Kiasi hiki cha nits kinafanya kioo kuonyesha vizuri hata ukiwa nje chini ya mwanga wa jua kali
Nguvu ya processor
Tecno Spark 40 Pro inatumia processor ya Mediatek Helio G100
Utendaji wa helio G100 ni wa wastani kutokana na uundo wake
Unaweza kutumia vizuri kwa matumiz ya kawaida ya kila siku pasipokuwa na shida
Ila kwenye kucheza gemu itakulazimu upunguze settings ziwe za chini
Hii itakusaidia kucheza magemu makubwa bila kuganda ganda
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya Tecno Spark 40 Pro ina ukubwa wa mah 5200
Kiwastani, betri inaweza dumu na chaji takribani masaa 12 ukiwa unatumia intaneti muda wote
Pia inasapoti kuchajiwa kwa njia ya wireless
Wireless yake inaweza kupokea umeme wa wati 30
Chaji yake inapeleka umeme mwingi wa wati 45,
Chaji hii inalijaza betri lake ndani ya dakika 60
Uimara wa bodi
Bodi ya Tecno Spark 40 Pro ina cheti cha IP64
Ni cheti kinachoashiria uimara wa simu kuzuia maji na vumbi
Ila sio kwa kiwango cha kuizamisha kwenye kina kikubwa
Ikizama kwenye maji kama hujaitoa mapema simu itapata madhara
Pia upande wa kioo kuna skrini protekta ya vioo aina gorilla glass 7i
Gorilla glass 7i inaweza kuilinda simu na mikwaluzo pia kutopasuka ikianguka kwenye kimo cha mita 2
Hata hivyo swala la kutopasuka inategemea sana na uso wa simu ilipoangukia
Hivyo kuwa makini
Ubora wa kamera
Tecno Spark 40 Pro ni simu ya kamera moja ya 50MP
Ina uwezo wa kurekodi video za resolution ya 1440p
Ubora wa picha ni wa kawaida
Na picha zinatokea vizuri hasa katika mwanga mwingi
Kiujumla hakuna maboresho upande wa kamera kati ya spark 40 pro na spark 30 pro
Ubora wa Software
Spark 40 Pro inaendeshwa na HIOS 15 ikiwa juu ya mfumo endeshi Android 15
Hii simu itapata maboresho ya android kwa muda wa miaka 3
Kwa maana utapata hadi Android 18 hivyo kasoro za kimifumo zinaweza tatuliwa kupitia hayo maboresho
HIOS 15 itakupa mifumo mbalimbali ya AI kama circle to search na nyinginize
Washindani wa Tecno Spark 40
Kuna simu nyingi sana zimetoka mwaka 2024 na 2025 zenye ufunano kisifa na Tecno Spark 40 Pro
Xiaomi Redmi 14 Pro 4G ina sifa sawa na hii tecno hii
Wakati huo Redmi ina maboresho kidogo upande wa kamera na betri
Mshindani mwingine ni Infinix Note 40 4G
Karibu kila kitu kinafanana
Hata Tecno Spark 30 Pro inaweza kuwa ni mbadala mzuri
Bila kusahau Samsung Galaxy A16 4G
Neno la Mwisho
Kwa wanaohitaji simu ya bajeti yenye ubora Tecno Spark 40 Pro ni chaguo zuri
Bei yake inaendana na sifa ilizonazo
Na sifa zake nyingi zinakidhi mahitaji ya watu wengi