Simu mpya ya Tecno Spark 40 tayari imeingia sokoni
Kuna maboresho ila sina uhakika iwapo maboresho yake yanaweza mshawishi mtumiaji wa Spark 30 kutumia spark 40
Ukizingatia bei ya Tecno Spark 40 haitofautini sana na toleo lililopita
Wakati huo Spark 40 ikiwa imepunguzwa baadhi ya vitu
Kama una shauku ya kujua basi fuatilia posti yote
Bei ya Tecno Spark 40 ya GB 128
Spark 40 ya ukubwa huu inauzwa shilingi laki tatu na ishirini (320,000) kwa Tanzania
Hii ikiwa na ukubwa wa RAM ya GB 4
Tofauti na mwaka jana iliyokuwa na GB 8
Spark 40 ya gb 256 inaambatana na ram ya gb 8 ila bei yake ni 420,000
Kwa hiyo tathmini matumizi yako ufanye chaguo sahihi
Sifa za Tecno Spark 40
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | 256GB,128GB na RAM 8GB,6GB,4GB |
Kamera | Kamera MOJA
|
Muundo | Urefu-6.67inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 320,000/= |
Uwezo wa network
Tecno Spark 40 ni simy ya 4g haisapoti mtandao wa 5g
Na inatumia laini za kawaida kwa maana haina eSIM
Inatumia 4g aina ya lte cat 7 yenye kasi inayofika 300mbps
Ukiwa eneo lenye 4g+ unaweza kuifikia hii kasi
Hiyo itakusaidia kudownload kwa muda mfupi faili la gb kubwa
Hata hivyo inategemea mtandao unaotumia
Ubora wa kioo
Kioo Tecno Spark 40 ni cha ips lcd chenye refresh rate inayofika 120hz
Hii refresh rate inaifanya simu na mguso laini n wa haraka
Tofauti na spark 30 iliyokuwa na 90hz
Bahati mbaya ni kuwa kioo cha spark 40 kimenguwa resolution yaani ina 720p
Hivyo muonekano wa vitu haukolei sana na uangavu kidogo
Nguvu ya utendaji
Utendaji wa hii ni wa wastani kutokana na kutumia prosesa ya mediatek helio g91
Inafaa zaidi kwa matumizi ya kawaida kama whatsapp na hata kucheza gemu kwa settings za chini
Ukinunua yenye RAM ya gb 8 utendaji utaimalika kiasi fulani
Kwenye app ya geekbench hii chip ina alama 405
Ambayo kiuhalisia sio kubwa linapokuja swala la utendaji
Uwezo wa kamera
Hii simu ina kamera moja inayopiga picha na kurekodi video
Uubwa wake ni MP 50 na ina ulengaji aina PDAF
Ubora wa picha ni mzuri kwa maingira yenye mwanga mwingi
Na kamera inaweza kurekodi video za full hd
Software
Tecno Spark 40 inakuja na mfumo wa HIOS 15 ukiwa kwenye Android 15
HIOS 15 inakupa mifumo kadhaa ya AI kama vile circle to search, AI writing
Kwa maana utakuta kuna mifumo inayofupisha taarifa kuwa fupi
Hakuna taarifa kama itapokea toleo jipya la Android
Kwa sababu hata Tecno Spark 30 haijapokea Android 15
Neno la mwisho
Kama una simu ya tecno ya zamani sana, basi ukimiliki tecno spark 40 ni hatua kubwa
Ila kama una spark 30 toleo sahihi zaidi kumiliki ni Tecno Spark 40 Pro+