Simu za madaraja zinazotoka miaka ya karibuni zinashawishi kuachana na kununua simu za gharama kubwa
Maana matoleo mapya yamekuwa na ubora wenye tofauti ndogo na simu za bei kubwa
Tofauti ambazo mtu wa kawaida anaweza asizione
Ubora huo upo kwenye Tecno Camon 40 kama utakavyoona ikiwemo na bei yake
Bei ya Tecno Camon 40 Tanzania
Tecno Camon 40 ya GB 128 inauzwa shilingi laki sita na nusu (650,000)
Ukubwa wa RAM ni GB 8 ambayo ni kubwa inayoweza kuendesha vitu vingi pasipo na shida
Pia zipo Camon 40 za GB 256 na hadi RAM ya GB 12
Na bei yake ni kubwa zaidi ya hapo hata hivyo kiwastani GB 8 inatosheleza katika vitu vingi
Uzuri ni kuwa simu pia inatumia mfumo wenye kasi upande wa memori ambao ni UFS
Sifa za Tecno Camon 40
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | AMOLED, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | 256GB,128GB na RAM 8GB,12GB |
Kamera | Kamera MBILI
|
Muundo | Urefu-6.78inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 650,000/= |
Uwezo wa network
Tecno Camon 40 ni simu ya 4G
Inatumia laini za kawaida hivyo inakosa mfumo wa eSIM
Aina ya 4G inayotumia LTE Cat 13 yenye uwezo wa kupakua vitu kwa kasi inayofika 650Mbps
Lakini kasi inategemea na nguvu ya mtandao unaotumia na nadra kwa hapa kupata kasi hiyo
Pia hii simu haina 5G
Ubora wa kioo
Kioo cha Tecno Camon 40 ni cha aina ya AMOLED chenye refresh rate 120Hz
Refresh rate husaidia gemu kuonekana vizuri
Pia muonekano wenye mwitikio mzuri unapokuwa una-scroll
Refresh rate kubwa hutumia kiasi kikubwa cha chaji
Processor ya Tecno Camon 40 ina mifumo ya kutambua nyakati ambazo haziihitaji refresh rate kubwa
Nguvu ya processor
Tecno Camon 40 inatumia processor ya Mediatek Helio G100
Imegawanyika katika sehemu mbili zenye core nane
Sehemu zenye nguvu zinatumia muundo wa Cortex A76
Utendaji wa Cortex A76 ni wastani unaoendana na standard za sasa
Kwa mujibu wa geekbench, helio g100 inaweza fungua peji 50 kwa sekunde
Uwezo wa betri na chaji
Ukubwa wa betri ya tecno ni 5200mAh
Ni betri na chaji inaweza kupeleka umeme wa wati 45
Hivyo betri kubwa haitoleta shija katika kujaza betri kwa haraka
Kiwastani, tecno camon 40 inakaa na chaji kwa takribani masaa 14
Muda huo unafikiwa ukiwa na matumizi ya kawaida
Uimara wa bodi
Simu ya Tecno Camon 40 ina bodi imara kutokana uwezo wa kuzia maji yenye presha kubwa
Kwani ina viwango vya IP66
Kwa mfano ukilowesha simu kwa kutumia mabomba ya kuoshea magari kwa uelekea wowote maji hayatopenya
Lakini inafaa kuepuka mazingira ambayo yatazamisha simu kwenye kina kikubwa muda mrefu
Maana haina waterproof ya IP67 ama IP68
Ubora wa kamera
Simu inakuja na kamera mbili za wide na ultrawide
Kamera kuu ina megapixel 50 lakini inaweza kurekodi video za full hd
Ubora wa picha kwa nyakati za mchana hauna tofauti na Infinix Note 50
Yaani inajitahidi kwa sehemu kubwa katika utofautishaji na utoaji wa rangi sahihi
Lakini kuna mazingira kamera na dynamic range ndogo hasa muangaza ukiwa mkubwa sana
Ubora wa Software
Simu inakuja na Android 15 na HIOS 15
HIOS 15 imeunganishwa na AI ya deepseek ambayo unaweza itumia kuuliza maswali mbalimali
HIOS 15 ina mifumo mingi ya akili badnia mifumo hiyo kama live translation(inatafsiri lugha ya mtu unayeongea naye lugha tofauti)
Pia ina mfumo wa kuondoa kitu usichokihitaji kwenye picha
Na utendaji wake ni mzuri
Washindani wa Tecno Camon 40
Katika kipengele cha simu za matoleo ya daraja la kati kuna simu nyingi zinazoendana ubora
Mshindani wa kwanza ni Infinix Note 50 ambayo ina bei sawa na hii
Lakini kuna Redmi Note 14 yenye ufanano wa vitu vingi na wakati huo redmi note 14 haifiki laki sita
Pia kuna Samsung Galaxy A16 na yenyewe bei yake sio kubwa ukilingnisha na Camon 40
Pia kuna Oppo A5 Pro japo haina ubora mkubwa sana lakini ni mbadala na mshindani pia
Neno la Mwsiho
Bei ya Tecno Camon 40 kwa sehemu kubwa inaendana na sifa zake
Ukitazama juhudi kubwa upande wa software utakubaliana na hili
Baadhi ya vitu vya AI kampuni zingine huzieka katika matoleo yenye ghrama
Lakini kwa tecno ipo tofauti