Samsung Galaxy A06 ina betri inayokaa na chaji muda mrefu na ni simu ya daraja la chini
Hii inamaanisha watu wengi kwa hapa Tanzania wanaweza inunua
Kwa sababu bei ya samsung galaxy A06 ni shilingi laki tatu na nusu (350,000)
Ni bei itakayokupa Galaxy A06 ya ukubwa wa GB 128 na RAM ya GB 4
Hakuna tofauti kubwa sana na toleo lilopita la Samsung Galaxy A05
Ila kuna tofauti ndogo upande wa software na utendaji
Sifa za Samsung Galaxy A06
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD |
Softawre |
|
Memori | eMMC 5.1, 128GB,64GB, na RAM 6GB,4GB |
Kamera | Kamera MBILI
|
Muundo | Urefu-6.7inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 350,000/= |
Uwezo wa network
Samsung Galaxy A06 ni simu ya laini mbili na haisapoti eSIM
Inakubali mtandao wa 4G na haina uwezo wa 5G
Ukizingatia aina ya bei na wateja lengwa inaondoa ulazima wa uwepo wa 5G
Simu inasapoti masafa yote yanayotumiwa na mitandao ya simu nchini
Hivyo hakuna laini itakayoshindwa kusoma
Kama ikiwa hivyo basi utakuwa umenunua simu mbovu na huna budi kuirudisha
Kasi ya 4G ni kubwa kwenye hii simu kama utapata mtandao wenye nguvu madhubuti
Ubora wa kioo cha Samsung Galaxy A06
Hakuna maajabu kwenye ubora kioo cha Samsung Galaxy A06
Kwani refresh rate ipo ya kawaida ya 60Hz
Wakati huo simu mpya Tecno Spark 30C ina refresh rate inayofika 120Hz
Pitia hapa kuifahamu, simu ya tecno spark 30C kiundani
Pia kioo chake kina resolution ndogo ya HD+ na sio full hd
Uangavu wake ni wastani kutokana na kuwa na nits 500
Kwa maana kama ukiwa juani uangavu hautokuwa mkubwa sana
Nguvu ya processor Mediatek Helio G85
Utendaji wa Mediatek Helio G85 sio mkubwa ukilinganisha na chip ya Dimensity 6500
Lakini bado utaweza fanya vitu vingi japo sio kwa ubora mkubwa sana
Kwa mfano kwenye magemu ili ucheze vizuri itakulazimu kuweka settings za chini
Na pia helio g85 haitoweza ku-push fremu nyingi(60fps) ukiwa unacheza gemu
Fremu zikiwa nyingi muonekano wa gemu unakuwa mzuri kama vile unaangalia video
Lakini hii inasababishwa na chip kuwa na muundo wa zamani wa Cortex A75 kwenye core zenye nguvu kubwa
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya hii simu ina ukubwa wa 5000mAh
Ukifungua box utakutana na waya wa kuchaji bila kichwa chaji
Yaani kama hauna chaji utalazimika kununua chaji yake
Uwezo wa kuchaji inakubali mpaka wati 25
Na inachukua dakika 90 kujaa kwa asilimia 100 kutoka zero
Ukaaji wa chaji ni wa kuridhisha sana
Kwa matumizi ya hapa na pale unaweza ukaitumia mpaka masaa 13
Na ukiwa unaperuzi intaneti muda wote simu inachukua masaa 12 mpaka chaji kuisha
Ukubwa na aina ya memori
Kuna matoleo mawili tu upande wa memori ambazo ni GB 64 na GB 128
Na RAM pia zimegawanyika katika sehemu mbili ambazo ni 4GB na 6GB
Kwa bahati mbaya mfumo wa memori wa hii simu sio ule wa UFS bali ni eMMC
eMMC haina kasi kubwa kama mifumo ya UFS na kiukweli simu nyingi siku hizi zimeacha kuweka mifumo eMMC
Ni eneo ambalo samsung hawakutenda haki kwenye hii simu
Uimara wa bodi ya Samsung Galaxy A06
Bodi ya Samsung Galaxy A06 ni ya plastiki kwa pande isipokuwa mbele kwenuye skrini ndio kuna glasi
Hii simu haijainishwa kuwa na viwango vya IP
Hivyo hakuna waterproof ya haina yoyote
Umakini lazima uzingatiwe unapokuwa kwenye mazingira ya mvua ama kwenye maji
Kiujumla simu inahitaji ulinzi wa ziada maana hii sio samsung galaxy s24
Ubora wa kamera
Ina jumla ya kamera mbili upande wa nyuma
Aina za zinazopatikana kwenye Samsung A06 ni wide na macro kwa ajili ya kupiga vitu vya karibu sana
Kuhusu ubora wa picha simu inapiga picha vizuri
Na ushahihi wa rangi hata kwa watu wenye ngozi nyeusi ni mkubwa
Haimg’arishi mtu kiasi cha kuondoa uhalisia mtu
Changamoto ukiwa unapiga mazingira yanayopokea mwanga mwingi wa jua usahihi wa rangi hupungua
Ubora wa Software
Kwenye upande wa software samsung wana mfumo mzuri sana unaoitwa One UI 6.1
Na hii simu ndio mfumo unaotumia pamoja na mfumo endeshi wa Android 14
One UI 6.1 imetumika pia kwenye samsung za mdaraja ya juu yaani Samsung Galaxy S24
Lakini hautopata vitu vyote vinavyopatikana kwenye Samsung Galaxy S24
Hata utaweza kupokea matoleo mapya ya Android kwa kipindi cha miaka miwili
Hii ikiwa na maana utapata Android 15 na Android 16
Maboresho ya namna yanakuhakikishia kupata maboresho mbalimbali yanayoambatana na android mpya
Washindani wa Samsung Galaxy A06
Kwenye hiki kipengele kuna washindani wengi wengi hasa toka kwa kampuni za China
Tecno wana simu mpya za Tecno Spark 30, na mojawapo inauzwa kwa bei ya chini ya hii
Kuna toleo la Realme C55, ni la mwaka 2023 ila utendaji wake ni mkubwa zaidi
Haitoshi pia kuna ujio wa simu ya Redmi 14C itakayotoka muda wowote
Kiumla machaguo yako mengi yanayoleta ushindani kwa hii samsung
Neno la Mwisho
Samsung Galaxy A06 imeongeza kitu kimoja kikubwa sana ukilinganisha na matoleo mengi ya daraja la chini
Kitendo cha kuzipa simu maboresho kwa kipindi kwa miaka miwili sio jambo ndogo
Kiuhalisia watumiaji wengi wa simu ndogo huwa hawapati maboresho mapya ya android baada ya kununua
Hivyo bei ya samsung galaxy 06 inaendana na thamani yake