Kiuhalisia Infinix Smart 20 ni simu moja na Infinix Smart 10
Sifa karibu zote zinafanana ila utofauti upo maneneo matatu
Hizi tofauti zinaweza kuonekana kuwa ndogo lakini zinaweza leta upekee kulingana na aina ya matumizi
Tutaangalia bei ya infinix smart 20 na sifa zake kama inashawishi kuitupa infinix smart 10
Bei ya Infinix Smart 20 GB 128
Infinix smart 20 ya GB 128 inauzwa shilingi 350,000 (laki tatu na nusu)
Hii ni bei ya infinix ya GB 4 kwa ukubwa wa RAM
Na ya ukubwa wa GB 64 inauzwa shilingi 320,000

Hata hivyo toleo smart 20 linakuja na RAM ya GB 4
Tofauti na infinix smart 10 ina mgawanyo wa RAM za GB 3, 4, 6 na 8
Na hizi hapa chini ndio sifa za jumla za Infinix Smart 20
Sifa za Infinix Smart 20
| Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
|---|---|
| Network | 2g, 3g, 4g |
| Processor(SoC) |
|
| Display(Kioo) | IPS LCD, Refresh rate:120Hz |
| Softawre |
|
| Memori | 64GB,128GB, na RAM 4GB |
| Kamera | Kamera moja
|
| Muundo | Urefu-6.9inchi |
| Chaji na Betri |
|
| Bei ya simu(TSH) | 320,000/= |
Uwezo wa network
Infinix smart 20 ni simu inayosapoti mpaka 4G
Haina mfumo wa eSIM
Na pia haisapoti mtandao wa 5G
Upande wa WIFI pia masafa yake yanafika hadi 2.4GHz
Ambayo hayana tofauti na 4G hivyo hata ukishea hotspot(router wifi) spidi inatosheleza kabisa
Ubora wa kioo
Kioo cha hii simu ni cha aina IPS LCD
Ambacho resolution ni ya hd yaani pixels 720 x 1576 pixels
Kina chake cha rangi sio kikubwa kama vioo aina ya amoled
Hata hivyo hii ina refresh rate inayofika 120Hz
Hivyo mwitiko wa kioo unapotachi na ku-scroll ni mzuri
Nguvu ya utendaji wa prosesa
Prosesa ndio ubongo wa simu na kigezo kikubwa kinachotambulisha nguvu ya utendaji
Infinix Smart 20 inatumia prosesa ya Mediatek Helio G81 Ultimate
Uwezo wake sio mkubwa ikizingatiwa simu ina RAM ndogo ya GB 4
Hata hivyo inaweza kucheza gemu nyingi
Na kwa baadhi ya gemu kubwa muonekano wa picha unafika 30fps kwenye settings za juu
Bado ni ndogo lakini kucheza gemu kama Genish Impact inatosha kuonyesha kuwa simu inatosheleza mahitaji ya mtumiaji wa kawaida
Uimara wa bodi
Infinix Smart 20 ni himilivu simu inapoanguka katika kimo cha mita 1.5
Na ina waterproof inayoainishwa na cheti IP64
Cheti cha IP64 kinaashiria uwezo wa simu kuzuia maji ya kumiminika
Hivyo simu ikizama kwenye kina kikubwa itaharibika ndani ya muda
Lakini kwenye mvua simu itaweza kuzuia hayo maji
Hata hivyo umakini unahitajika bila kujali mambo mengine
Ubora wa kamera
Infinix Smart 20 sio simu sahihi kwa anaependa kujirekodi na kupiga picha
Simu ina kamera moja yenye ukubwa wa megapixel 8
Haina mifumo ya ziada inayosapoti kamera kama vile OIS na dual pixel pdaf
Lakini inaweza kurekodi video kwa uangavu wa full hd+
Hivyo kamera yake inatoa zenye mng’ao mzuri japo kwa 30fps
Uwezo wa chaji na betri
Infinix Smart 20 ina betri kubwa ukilinganisha na toleo lililopita
Hii simu betri ina ukubwa wa mAh 5200
Ongezeko hili linaleta tofauti ndogo kwenye muda wa betri kudumu na chaji
Kasi ya chaji ni wati 15
Hii itachukua muda kidogo mpaka ijaze hili betri
Hii simu inasapoti reverse charging, simu inakuwa kama power bank
Kwa maana unaweza kuchaji kifaa kingine japo spidi yake ya umeme ni wati 5
Ubora wa software
Infinix Smart 20 inaendeshwa na mfumo wa XOS 16 ulio ndani ya mfumo mkuu wa Android 16
Hii haitopokea toleo linalofuta la Android 17 na kuendelea
XOS 16 inakupa matumizi mingi ya mifumo ya AI
Mfano ni AI call assistant
Yaani AI inaweza kupokea simu na kufanya mazungumzo
Na pia unaweza kutengeneza theme kwa kutumia AI
Simu Mbadala
Infinix Smart 20 inafanana na simu ya Samsung Galaxy A07
Kama hujalizika na smart 20 galaxy inakupa vitu vya ziada japo ilitoka 2025
Moja ya eneo zuri la samsung ni upande wa kamera
Kamera ya Galaxy A07 ina megapixel 50
Na pia Samsung inapokea matoleo mapya ya Android kwa miaka 6
Na chaji yake inasapoti umeme hadi wa wati 25
Neno la mwisho
Utofauti wa kisifa wa Infinix Smart 20 na Smart 10 upo kamtika maeneo matatu
Maeneo hayo ni ukubwa wa betri, mfumo mpya wa android na urefu wa simu
Kama haya mabadiliko sio muhimu basi Infinix Smart 10 bado inafaa kwa sasa