SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Bei ya Infinix Note 50 na Sifa zake muhimu

Sifa za simu

Sihaba Mikole

June 13, 2025

Infinix wametoa matoleo mapya na yameshaanza kupatikana Tanzania

Moja ya toleo hilo ni Infinix Note 50 ambayo ina maboresho upande wa software, kioo na uimara wa simu kiujumla

Kwa sifa zake za ziada imepelekea bei yake kuongezeka kidogo ukilinganisha na Infinix Note 40 ya 2024

Na pia ina toleo la aina moja upande wa memori

Bei ya Infinix Note 50 ya GB 256

Kwa Tanzania Infinix Note 40 inauzwa shilingi laki sita na elfu sitini (660,000)

Hii ikiwa na RAM ya ukubwa wa GB 8

Hakuna aina nyingine ya RAM matoleo yote yana RAM ya GB 8

Pia mfumo wake wa memori ni aina ya UFS 2.2

Ni vizuri ukazielewa sifa za Infinix Note 40 kisha ukalinganisha na bei yake kujua kama zinashahabiana

Sifa za Infinix Note 50

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
  • CPU – Mediatek Helio G100 Ultimate
  • Core Zenye nguvu(2) – 2×2.2 GHz Cortex-A76
  • Core Za kawaida(6) –  6×2.0 GHz Cortex-A55
  • GPU-Mali-G57 MC2
Display(Kioo) Amoled, Refresh rate:120Hz
Softawre
  • Android 15
  • XOS 15
Memori UFS 2.2,256GB na RAM 8GB
Kamera Kamera MBILI

  1. 50MP,PDAF(wide)
  2. 2MP(Macro)
Muundo Urefu-6.78inchi
Chaji na Betri
  • 5200mAh-Li-Po
  • Chaji-45W
Bei ya simu(TSH) 660,000/=

Uwezo wa network

Infinix Note 50 ni simu inayosapoti mtandao wa 4G haina 5G

Aina ya 4G inayosapti ni LTE Cat 13

LTE Cat 13 inaweza kupakua kitu kwa spidi inayofika 650Mbps

Ni kasi kubwa kama mtandao wa simu utakuwa una nguvu hiyo

Kwa wanaopenda eSIM, Note 50 haina huo mfumo bali inatumia laini za kawaida

Ubora wa kioo cha Infinix Note 50

Kioo cha hii simu ni cha aina ya Amoled

Refresh rate yake inaweza kufika hadi 144hz

Refresh rate kubwa hufanya simu kuwa na mwitikio na muonekano mzuri unapokuwa una-scroll na hata wakati wa kucheza gemu

Hata hivyo si mara zote utahitaji kutumia refresh rate kubwa

Uangavu wake kwenye kuonyesha vitu unafika nits zaidi ya 2000

Hivyo ukiwa maeneo ya juani bado utaweza kuona kwa uzuri

Nguvu ya processor ya Mediatek Helio G100 Ultimate

Chip ya Mediatek helio g100 ultimate ina nguvu ya wastani

Inaweza kufanya vitu vingi pasipo kukwama kwama

Kwenye geebench inaonyesha helio g100 ultimate inaweza kufungua kurasa zaidi ya 50 kwa sekunde

Haina tofauti kubwa sana na processor ya Snapdragon 4 gen 2 iliyotumika kwenye simu za Redmi Note 12R ya 2023

Hii chip ina sehemu mbili zilizotengwa kwa kufanya kazi zinazohitaji kazi kubwa

Sehemu zinatumia muundo wa Cortex A76

Uwezo wa betri na chaji

Betri ya Infinix Note 50 ina ukubwa wa mAh 5200

Ni betri kubwa inayoweza kukaa na chaji muda mrefu

Chaji yake inapeleka umeme wa wati 45

Hii inamaanisha chaji yake inawahi kujaa chaji ndani ya dakika 80 kutoka 0%

Hii simu inaweza kuchajiwa kwa njia ya wireless kwa kasi ya wati 30

Uimara wa bodi

Infinix Note 50 ina waterproof aina ya IP64

IP64 humaanisha simu inaweza kuzuia maji ya kiwango cha kunyululuzika na pia kuzuia vumbi

Ni tofauti na IP67 ambayo simu inaweza zama kwenye maji na ikanusurika

Lakini IP64 unaweza ukaitumia wakati mvua inanyesha na sio kuzama kina kirefu

Ubora wa kamera

Infinix Note 50 ina kamera mbili zenye megapixel 50 na 2

Kmaera kubwa inajitahidi kupiga picha vizuri

Kwenye mwanga wa kutosha muonekano wa vitu mzuri kiasi

Kitu kimoja kinachoweza kisifurahishe baadhi ni mkorezo mkubwa wa rangi

Lakini kuna mazingira uhalisia wa rangi unapungua hasa mwanga wa jua ukiwa mkubwa

Hata hivyo ni kamera nzuri yenye ubora wa wastani

Ubora wa Software

Infinix Note 50 inakuja na Android 15 na itapata matoleo mapya ya android kwa muda wa miaka miwili

Mfumo mwingine ambao utakupatia mifumo mingi ya AI(akili mnemba) ni XOS 15

Kuna mifumo ya AI ipatayo 10 kwneye hii simu

Baadhi ni circle to search, kufupisha taarifa ya kitu, kuondoa kelele wakati wa mawasiliano kwa njia ya simu

Simu nyingi za madaraja ya kati hutoa mifumo ya AI michache ila infinix inayo mingi

Washindani wa Infinix Note 50

Kuna Tecno Camon 40 ambayo bei yake ni sawa na hii infinix

Camon 40 na Infinix 50 ni kama simu moja maana zinafanana vitu vingi mno

Mshindani mwingine ni Samsung Galaxy A16 na Redmi Note 14 4G

Hizi zote zina utendaji unaofanana na bei zake sio kubwa

Kwa kifupi washindani ni wengi katika kipengele hiki cha matoleo ya daraja la kati

Neno la Mwisho

Kwa kuzingatia sapoti ya software ya miaka miwili, bei ya infinix note 50 ina haki kuwa hivyo

Kutoa update maana yake kuna watu wanafanya maboresho ya simu kwa kutazama changamto zinazojitokeza

Kwa hiyo kuna gharama pia ya kutoa update ndio maana simu za bei ndogo sana hazina update

Mbali  na hayo ni vizuri infinix wakaanza kuwezesha video za 4k kwenye simu za matoleo ya Note

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

bei ndogo

Simu za laki tatu zenye ubora wa kuridhisha kwa 2025

Iwapo unapanga kununua simu chini ya laki tatu au zisizozidi laki nne usitarajie kupata simu yenye ubora mkubwa Kwa maana usitarajie kamera kali na utendaji mkubwa Ila kwenye hii post […]

infinix note 50 thumb

Ubora wa simu mpya za Infinix Note 50

Katika baadhi ya nchi, Infinix walitoa toleo jipya la Infinix Note 50 Matoleo hayo ni Infinix Note 50 4G Infinix Note 50s Infinix Note 50 Pro 4G Infinix Note 50 […]

tecno camon 40 pro thumb

Bei ya Tecno Camon 40 Pro na Sifa zake za muhimu mpya

Hapa utaenda kufahamu bei halisi ya Tecno mpya ya 2025 Tecno hiyo ni Tecno Camon 40 Pro ambayo imezinduliwa mwezi wa tatu Camon 40 Pro inafanana kiasi flani na Camon […]

Ujio wa Simu mpya za Tecno Camon 40

Huu mwezi wa tatu 2025 tecno imetangaza ujio wa matoleo mapya ya Tecno Camon 40 Simu hizo ni Tecno Camon 40 Tecno Camon 40 Pro 5G Tecno Camon Pro Tecno […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani
TUFUATE
Youtube Facebook Instagram twitter

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: 0756 077262 au 0683 420543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company