Unataka simu nzuri ya Infinix?
Ni infinix note 40 pro iliyotoka mwaka 2024 mwanzoni mwa mwaka
Ila sasa bei yake ni shilingi milioni moja na laki moja ikiwa na ukubwa wa GB 256
Ubora mkubwa wa Infinix Note 40 Pro upo kwenye skrini, utendaji, betri pamoja na chaji
Tupitie kipengele kimoja baada ya kingine uone ubora mkubwa wa infinix note 40 pro
Sifa za Infinix Note 40 Pro
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | AMOLED, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | 256GB na RAM 8GB |
Kamera | Kamera tatu
|
Muundo | Urefu-6.78inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 1,100,000/= |
Uwezo wa network
Kwanza hii simu inatumia laini za kawaida yaani haitumii muundo wa laini za eSIM
Inasapoti mtandao wa 5G hivyo kama upo kwenye maeneo ya 5G utakuwa unapata kasi kubwa ya kupakua vitu
Uzuri ni kwamba inasapoti 5G za aina zote yaani SA na NSA
Kama mtandao una miundombinu ya SA 5G utapata 5G ya ukweli na yenye kasi
Kwa hapa Tanzania NSA ndio inayotumika zaidi kutokana na SA kuwa na gharama kubwa na ni teknolojia mpya inayohitaji vifaa vipya kabisa
Upande wa 4G, kasi yake inafika ziaidi Mbps 2000
Lakini kuipata spidi hii inategemea sana na uwezo wa mtandao husika ambapo kwa Tanzania ni changamoto
Ubora wa kioo cha Infinix Note 40 Pro
Kioo cha Infinix Note 40 Pro ni angavu sana kwani kina nits 1300
Kinaruhusu kutumika kwenye mazingira yoyote na vitu vikaonekana kwa uzuri
Ni cha aina ya amoled chenye refresh rate ya 120Hz
Refresh rate kubwa hufanya kioo kuwa fasta na chepesi
Na amoled utajiri wa rangi ni mkubwa na rangi za vitu huonekana kwa usahihi ukilinganisha na vioo vya LCD
Nguvu ya processor Mediatek Dimensity 7020
Kwanza Infinix Note 40 Pro ina ufanisi mzuri wa matumizi ya betri kwa sababu ya aina ya processor iliyotumika
Processor hiyo mediatek dimensity 7020
Dimensity 7020 ina core mbili zilizoundwa kufanya kazi kubwa lakini kwa matumizi madogo ya umeme
Sehemu(core) hizo ni Cortex A78, na core sita zilizobaki ni aina ya Cortex A55 kwa ajili ya kazi zisizohitaji nguvu kubwa kama kutuma meseji kupiga simu nk.
Kwenye app za kupima uwezo wa procesor, dimensity 7020 ina alama za kuridhisha
Katika vipimo vya antutu, chip ina alama 470,000
Na geekbench, chip ina alama 884, simu za madaraja ya chini huwa na alama za chini zaidi
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya Infinix Note 40 Pro ina ukubwa wa mAh 5000
Hivyo ukaaji wa chaji ni wa kuridhisha
Simu inaweza kuchajiwa kwa njia mbili
Na zote zinaweza kujaza betri hii kubwa kwa haraka ndani ya muda mfupi
Yaani simu inaweza chaji kwa njia ya waya au bila waya(wireless)
Chaji ina kasi ya kupeleka umeme wa wati 45 ambayo inaweza kujaza betri kwa 100 ndani ya dakika 70
Na wireless kasi yake ni wati 20
Hii ni tofauti na simu nyingi ambapo wireless chaji huwa na kasi ndogo
Ukubwa na aina ya memori
Hii simu inatumia memori za muundo wa UFS ambao huwa na kasi kubwa sana ya kusafirisha data
Na kuna toleo la aina moja tu upande wa memori
Ambapo utapata yenye ukubwa wa GB 256
Na ram ya GB 8
Huu ukubwa unafaa na kutosheleza kuhifadhi mafaili mengi
Uimara wa bodi ya Infinix Note 40 Pro
Infinix wameendelea kuboresha simu wanazoziingiza sokoni
Kwa matoleo mengi ya nyuma infinix hazikuwa na viwango vya IP
Viwango vya IP huashiria uwezo wa simu kuzuia maji
Ila toleo la Infinix Note 40 Pro linabainisha kuwa na waterproof ya IP53
IP53 inaashiria uwezo wa simu kuzuia maji ya kiwango cha kunyunyuluzika
Tofauti na IP67/IP68 ambavyo vinabainisha simu kutopitisha maji hata ikizama kwenye kina cha mita 1.5 kwa muda wa nusu saa
Labda matoleo yatakayofuata yatakuja na waterproof imara zaidi
Ubora wa kamera
Kama umesoma mwanzo mwisho utaona infinix note 40 pro ubora wake ni mkubw maeneo mengi
Ila kwenye kamera kuna vitu vinakosekana ukilinganisha na bei yake
Kwanza ina kamera tatu huku kamera mbili zina megapixel 2 tu
Na pia kamera mbili hazijurikani ni za aina gani bali kamera moja ya megapixel 108 ina lenzi ya wide
Hii ndio kasoro kubwa ninayoiona
Kamera kuu upigaji mzuri hasa kwenye mazingira yenye mwanga wa kutosha
Ila haiwezi kurekodi video zenye resolution za 4K
Hii inasababishwa na uwezo wa processor kuwa mdogo kwenye kuchakata video za resolution kubwa
Ubora wa Software
Infinix Note 40 Pro inatumia mfumo endeshi wa Android 14 na XOS 14
Kuna vitu vingi vimeongezwa kwenye XOS 14
Kimoja wapo kizuri ni uwezo wa kutumia app mbili kwa wakati mmoja
Yaani unaweza ukaigawanya skrini katika mbili, ya juu na ya chini
Sehemu ya juu ukawa unaangalia youtube, na sehemu ya chini ukawa unasoma whatsapp
Hii inaitwa dual app
Washindani wa Infinix Note 40 Pro
Mshindani wa kwanza ni toleo la Samsung Galaxy A54 na pia Samsung Galaxy A55
Samsung Galaxy A55 ina ubora mwingi unaoizidi Infinix kwenye kila eneo
Pia kamera za samsung zipo tatu zinazoweza kurekodi video za 4K
Moja ya kamera zake ni ya ultrawide
Pia A55 ina skrini ya hdr10+ na waterproof ya IP67
Waki huo bei ya Samsung Galaxy A55 ni chini ya milioni moja
Simu mbadala nyingine ni Redmi Note 13 Pro
Redmi Note 13 Pro ina kioo kizuri chenye dolby vision, utendaji wenye nguvu kuliko infinix
Na Redmi Note 13 Pro inauzwa kwa bei ya chini ya laki nane
Na simu kali nyingine ambayo infinix note 40 pro haifui dafu ni OPPO Reno11 Pro
Bei ya OPPO Reno11 Pro inaendana na hii infinix
Kiujumla kwa aina ya bei, simu hii ya infinix inajiingiza katika kundi lenye simu nyingi kali
Neno la Mwisho
Bei ya Infinix Note 40 Pro inaashiria wazi kuna ubora mkubwa ukilinganisha na simu za matoleo ya Smart au Hot
Pamoja na hayo maboresho, kuna baadhi ya maeneo simu ilihitaji kuwa na maboresho zaidi ili kuendana na ushindani na simu zingine za namna hiyo.
Hata hivyo kwa mtumiaji na pia kwa asiependa infinix ataona utofauti mkubwa na matoleo ya nyuma ya infinix
Ni matumaini hii simu itakuwa inapokeo maboreshi ya mfumo mpya wa Android kwa miaka kadhaa