Google Pixel 9 ni simu mpya kabisa ya pixel kwa mwaka 2024
Ni simu kali sana upande wa utendaji, kamera na software hasa katika matumizi ya AI(akili mnemba)
Maboresho makubwa yamekuja na bei kubwa pia ukilinganisha na pixel za miaka ya nyuma wakati wa uzinduzi
Kwani bei ya Google Pixel 9 ya GB 128 inauzwa kwa zaidi ya shilingi milioni mbili na laki mbili kwa bei rasmi kutoka google
Hivyo basi kwa Tanzania bei yake inaweza kuzidi milioni 2.5
Swali la kujiuliza, kuna vitu gani hasa vinavyopelekea pixel 9 kuuzwa bei kubwa
Hii posti inajibu hilo kwenye upande wa sifa za simu hii.
Sifa za Google Pixel 9
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | OLED, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS , 256GB,128GB na RAM 12GB |
Kamera | Kamera mbili
|
Muundo | Urefu-6.3inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 2,500,000+/= |
Uwezo wa network
Google Pixel 9 ni simu ya 5G inayosapoti laini aina za eSIM
Kwa sasa kampuni zinazosapoti eSIM kwa Tanzania ni Airtel, Vodacom na TTCL
Simu inasapoti aina zote za 5G ikiwemo mmWave ambayo ndio yenye kasi kubwa zaidi
Pia 4G inasapoti masafa mengi hivyo hata kwa hapa Tanzania simu inaweza kutumika bila tatizo
Ubora wa kioo cha Google Pixel 9
Google Pixel 9 inakuja na kioo cha OLED chenye resolution ya 1080 x 2424 pixels
Ni resolution kubwa ambayo, na pia skrini yake inaongezewa ubora na uwepo HDR10+
HDR10+ inaongezea skrini kina cha rangi
Hivyo vitu vingi vinakuwa na muonekano mzuri wenye usahihi mkubwa wa rangi
Kwa wapenzi wa gemu watafurahia kutumia hii simu kwa sababu skrini ina kiwango cha refresh rate 120hz
Kiwango kikubwa cha refresh rate kinaifanya skrini ku-sense kwa haraka na smooth wakati unapoperuzi
Kiujumla kioo cha google pixel 9 kina ubora mkubwa na pia ni cha gharama
Nguvu ya processor Google Tensor G4
Simu inatumia processor ya Google Tensor G4 ambayo ni mpya
Pamoja na upya wa hii chip, kiutendaji inaachwa na chip za mwaka jana snapdragon 8 gen 4 na hata Apple A17 Pro
Ikumbukwe kuwa Tensor G4 imetengenezwa kwa ushirikiano na kampuni ya Samsung
Naweza sema Google Tensor G4 ni Exynos 2400 ya Samsung
Mbali na hayo, hii processor ina nguvu ya kufanya vitu vingi bila tatizo
Hii inatokana na core yenye nguvu kubwa sana kuundwa kwa muundo wa Cortex X4
Kiutendaji Cortex X4 imeongezeka kwa asilimia 15 ukilinganisha na muundo wa Cortex X3
Uwezo wa betri na chaji
Hii simu unaweza kuichaji kwa kutumia waya au bila waya kwa maana “wireless”
Na kiwango cha umeme kinachoweza kuingia ni wati 27
Kimakadirio, betri yake inaweza kuchukua takribani dakika 85 mpaka kujaa kwa 100%
Kitu kimoja cha kuangalia.
Ukubwa wa betri, betri ina kiwango cha 4700mAh
Japo ipo chini kidogo ya viwango vya betri nyingi ila kiwango hiki kinaweza kukaa na chaji hata kwa angalau masaa 11 ukiwa kwenye intaneti muda wote
Aina ya chaji ya hii simu ni usb type c
Ukubwa na aina ya memori
Kuna matoleo mawili tu upande wa memori ambayo yana ukubwa GB 128 na GB 256
RAM za simu ukubwa wake ni GB 12
Hii simu ina mifumo ya AI mingi ambayo kiujumla inahitaji memori kubwa
Ndio maaana inaambatana na RAM kubwa kwa ufanisi mzuri wa AI
Pia muundo wake wa memori ni wa UFS ambao kasi ya kusafirisha data ni kubwa
Uimara wa bodi ya Google Pixel 9
Bodi ya Google Pixel 9 imeundwa na bodi yenye waterproof aina ya IP68
Hii inamaanisha iwapo simu itazama kwenye kina cha mita 1.5 kwa muda wa nusu, maji hayataingia
Hali hii inakupa uhuru wa kutumia simu hata kwenye mazingira yenye unyevu unyevu
Kwenye ulinzi wa skrini, pixel 9 inakuja na vioo vya gorilla victus 2
Kampuni ya corning glass, inasema vioo vya gorilla victus 2 vinalenga kuzuia simu kupasuka pindi simu ikianguka katika uso wa ardhi ambao ni rahisi kioo kupasuka
Na pia ina uimara kwenye mikwaruzo
Kiujumla bodi ya simu ni nzuri ya kuweza kudumu kwa muda mrfu
Ila tu umakini unatakiwa katika mazingira yote
Ubora wa kamera
Hii simu ina kamera zipatazo mbili
Kamera zote zinatumia ulengaji wa dual pixel pdaf
Na kamera kubwa inaambatana na laser af, laser af mara nyingi hutumika zaidi nyakati za usiku
Kuhusu ubora wa picha, kamera kuu inapiga picha vizuri
Usahihi wa rangi ni mkubwa na dynamic range inafanya kazi kubwa sana katika utofautishaji wa rangi
Kwa kiasi kubwa kamera inapiga picha zenye muonekano halisi kwa sehemu kubwa
Upande wa video, kamera ya google pixel inaweza kurekodi mpaka video za 4K
Ubora wa Software
Google Pixel 9 inakuja na Android 14
Kitu kikubwa kinachopatikana kwenye software ni ongezeko la matumizi ya Artificial Intelligence
Hili unaweza kuliona kwa uwepo wa chatbot ya Gemini ambayo ni mshindani chatgpt
Pia kuna matumizi ya AI upande wa kamera
Kwa mfano mpo watu wawili na mnataka mpige picha ya pamoja mtakayotokea wote wawili
Camera ya pixel inakupa hiyo nafasi, kwa kuanza unapiga picha ya kwanza.
Halafu unatoka kwenye kamera kisha unaenda kupigwa picha wewe
Baada ya muda app inaunganisha picha zote mbili, na kuonekana kama ilipigwa kwa wakati mmoja
Washindani wa Google Pixel 9
Kwa kuwa Google Pixel 9 ni simu ya daraja la juu, washindani wake moja kwa moja watukuwa ni Samsung Galaxy S24, Apple iPhone 15
Pia Oppo matoleo ya find x, na baadhi ya simu za Xiaomi bila kusahau oneplus
Changamoto kubwa Google Pixel 9 anayoipata mbele ya washindani wake ni utendaji
Simu nyingi za Android za daraja la juu zinatumia processor ya Snapdragon 8 Gen 4
Tayari utendaji wa Snapdragon 8 Gen 4 ni mkubwa sana ukilinganisha na Google Tensor G4
Na bado kumekuwa na malalamiko juu ya kuzidi kwa joto unaosababishwa na chip ya tensor g4
Kwa bahati mbaya kuna mfanano wa bei na hizo simu
Neno la Mwisho
Bei ya Google Pixel 9 ni kubwa unapolinganisha kipato cha watanzania wengi
Pamoja na bei kuwa kubwa ubora wa simu pia ni kiwango katika maeneo mengi
Kuanzia kamera, uimara wa bodi, chaji na betri, na pia software na kamera ni balaa tupu
Kama unapenda kupiga sana picha google pixel ni toleo la kuipa kipaumbele
Iko vizuri zaidi katika kipengele hiko.
Wazo moja kuhusu “Bei ya Google Pixel 9 na Sifa zake muhimu”
Kwa bora,ilionao, inastahili kuzwa bei hiyo