SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

About

Sihaba Mikole

SimuNzuri ni tovuti inamilikiwa na WebAppLabs wanaojishughulisha na uundaji wa apps za android na Website.

SimuNzuri.com kama jina linavyojieleza inafafanua kwa lugha nyepesi sifa za simu.

Smartphone zinatengenezwa kwa kuwekewa hardware na software zinazotofautiana ubora.

Kwa asiyefahamu jinsi ya kutazama ubora simu hupata wakati mgumu kuchagua simu sahihi.

Hapo ndipo simunzuri.com inapokuja kutatua changamoto hiyo.

Jinsi simunzuri.com inavyotafiti

Makala nyingi zilizomo ndani ya tovuti ya SimuNzuri hufanyiwa tafiti.

Tafiti zetu zinatumia majaribio yaliyofanywa na watumiaji wa simu na majaribio ya wataalamu

Kwa maana hiyo taarifa za simu husika zinatoka kwa

  • Watumiaji wa simu
  • Wataalamu na wachambuzi
  • Kampuni husika
  • Maoni ya watumiaji
  • Majaribio

Kwa kuwa tovuti haina uwezo wa kumiliki simu nyingi tunakuwa makini sana katika ukusanyaji wa taarifa.

Na pia makala zetu zinazingatia uzoefu wetu katika matumizi ya simu.

Aina zipi za simu zinazoelezewa na SimuNzuri.com

SimuNzuri inajikita zaidi katika ufafanuzi kuhusu simu janja yaani SmartPhone.

Kwa bahati mbaya simu za batani hazielezewi.

Simu janja hugharimu kiasi kikubwa cha pesa.

Kila mwaka, kila mwezi simu janja mpya zinaingia sokoni.

Na smartphone nyingi huja na teknolojia mpya ukilinganisha na simu za aina nyingine hasa za batani.

Uchambuzi wa kina kwenye smartphone unahitajika.

Kuna simu chache za batani zinatumia android lakini nyingi zinakuja na vitu vile vile vya miaka yote.

Simu zinazoelezewa na SimuNzuri zinatumia mifumo endeshi ya Android au Apple iOS na kidogo Harmony OS ya huawei.

Hivyo hautakutana na mifumo endeshi kama Windows Mobile, KaiOS, Symbian OS, ama Ubuntu na mifumo mingine.

Vipengele vilivyomo ndani ya SimuNzuri.Com

Uchambuzi wa simu uliopo umegawanyika katika makundi sita.

  1. Bei nafuu
  2. Brand za simu
  3. Sifa za simu
  4. Miongozo
  5. Bei Nafuu
  6. Ulinganishi

Kipengele cha bei nafuu kinafafanua simu zinazouzwa chini ya 350,000/=

Kiuhalisia simu nyingi za bei nafuu zina ubora wa chini.

Kipengele hiki kinajaribu kukuonyesha simu za bei nafuu ambazo zina ubora wa kati.

Kipengele cha Brand kinaweka orodha ya simu zilizotengenezwa na kampuni moja ya simu.

Ukurasa wa Miongozo unafafanua vitu ambavyo huja na simu mfano processor, kamera, display nk.

Sifa za simu ni ufafanuzi wa ubora na mapungufu ya simu husika moja.

Ulinganishi ni ushindani wa ubora na madhaifu kati ya simu mbili.

Kipengele cha simu mpya kinaorodheshwa simu mpya iliyotoka ndani ya miezi miwili ya mwaka uliopo.

Mawasiliano

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 624 21 30 48

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani
TUFUATE
Youtube Facebook Instagram twitter

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company