Kuna teknolojia mpya ya betri imezipa betri za simu uwezo mkubwa sana
Kwa sababu ya hii teknolojia simu zinakaa mpaka SIKU NNE bila kuchaji
Na si siku nne ukiwa unaitumia kidogo – unaangalia video za tiktok, instagram, unacheza gemu na kila aina takataka unayotaka kuifanya
Lakini cha kushangaza
Sio simu zote mpya za 2026 zinatumia teknolojia hii mpya nitakayokueleza baadae
Nitakuonyesha simu 10 zenye uwezo mkubwa wa betri unaoweza kukusahngaza kweli
Uwezo ambao hujawahi kushuhudia
Realme P4 Power 5g
Ukubwa wa betri wa Realme P4 Power mAh 10,0001
Hii simu inaisha chaji baada siku mbili ukiwa unautumia bila kupumzika
Utendaji wake pia ni mkubwa

Kwani inatumia prosesa nzuri aina ya Dimensity 7400 Ultra
Bei yake ni shilingi laki tisa kwa Tanzania
Poco X8 Power
Poco X8 Power betri yake ina ujazo wa mAh 10,000
Pia inaweza kuchukua takribani siku mbili bila kuchaji
Inatumia prosesa ya Snapdragon 6 Gen 5

Hivyo utendaji wake pia unaweza kusukuma vitu vingi
Bei yake ni shilingi milioni moja na laki mbili
Vivo V80 Lite
Vivo V80 Lite na yenyewe inaweza kukaa na chaji zaidi ya siku mbili
Maana betri yake pia ina mAh 10,000
Ila hii chaji yake inapeleka umeme wa wati 44

Betri itachukua muda kidogo kujaa
Bei ya vivo v80 lite ni shilingi milioni moja na laki mbili
Redmi Note 17 Pro Max
Redmi Note 17 Pro Max ina betri la 10,000mAh na chaji ya wati 100
Inachukua takribani lisaa limoja kujaza hii betri kwa kiwango cha wati 100
Na ikishajaa inachukua takribani siku mbili mpaka chaji

Hii kama ukiwa unaitumia mara kwa mara
Bei yake kwa Tanzania ni shilingi milioni moja na laki nane
Honor Win
Simu nyingine ya betri ya maH 10,000 na chaji ya wati 100
Pia inasapoti wireless chaji ya wati 80
Hivyo chaji inaweza kujaza betri ndani ya dakika 70

Na baada ya hapo betri inaweza kuchukua siku mbili hadi kuisha
Bei yake ni shilingi milioni moja na laki sita
Honor Win RT
Honor Win RT ina bonge la betri na nguvu ya utendaji
Betri yake ina ukubwa wa mAh 10000
Na chaji yake ni fast chaji ya wati 100

Utendaji wake unachagizwa na chip ya Snapdragon 8 Elite
Bei yake ni shilingi milioni mbili kwa Tanzania
Ulefone Armor 29 Ultra
Ulefone Armor 29 Ultra ndio simu yenye betri kubwa zaidi
Hii inakaa na chaji takribani siku nne ikiwa inatumiwa muda wote
Kwa maana betri yake ina ukubwa wa mAh 20,000

Hakuna simu yenye ujazo huu mpaka sasa
Betri yake ina kasi ya wati 120
Bei yake ni shilingi milioni mbili na laki tano
Vivo iQOO Z11S
Betri yake inadumu na chaji takribani siku mbili ukiwa unaitumia muda wote
Betri yake ni kubwa kama simu zilzopita
Ukubwa wa betri ni mAh 10000
Ila chaji yake inapeleka umeme wa wati 40

Hivyo itachukuwa muda kujaa
Bei yake ni shilingi laki na nane
Oppo Find X9 Pro
Oppo Find X9 Pro inauzwa shilingi milioni mbili na laki nane
Betri yake inadumu kwa takribani masaa 22 (siku moja)
Betri yake ina ukubwa wa mAh 7500

Bei yake kubwa inachangiwa na vitu vingi
Tembelea hapa: sifa za oppo find x9 pro
Redmi Note 17 Pro
Betri ya Redmi Note 17 Pro ina ukubwa wa mAh 9000
Kiwango hiki kinadumu kwa takribani siku mbili
Chaji yake inapeleka umeme wa juu kabisa wati 67

Hivyo lazima itachukua muda kidogo
Kwa bei ya China simu inauzwa shilingi laki tisa
Hitimisho
Hizi simu zina uwezo wa kutunza chaji kwa sababu ya teknolojia mpya
Teknolojia hiyo inatumia matirio ya Silicon Carbon
Kwa hiyo betri zilizomo kwenye simu hizi zinaitwa betri za silicon carbon
Betri hizi zina uwezo wa kuhifadhi chaji zaidi kwa ukubwa ule ule wa betri
Lakini zina changamoto ndio maana baadhi ya kampuni hazitumii