SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Simu za Google Pixel sahihi za kununua (2026)

Miongozo

Sihaba Mikole

January 20, 2026

Hapa Tanzania Google Pixel imeshika kwa sasa

Ni simu zilizovuta wengi na kununua kama vipofu

Matokeo yake wengine wameibuka kununua Google Pixel ambazo hazifai kwa sasa

Baadhi za Google zina mapungufu upande wa utendaji, software na utunzaji wa chaji

Kwa sababu Pixel nyingi zinazonunuliwa hapa Tanzania ni za zamani

Zijue zipi sahihi usije  ukajichanganya huko mbeleni

Kuna mamilioni ya sababu kwa nini ununue hizi Google Pixel

Na ni nafuu mara mia kuepuka matole kuanzia Google Pixel 4 kwenda chini ikiwezekana

Hizi ndio sababu na naamini utanishukuru kukuepushia hasara mbeleni

Ukubwa wa betri

Simu za Google Pixel ya mwaka 2019 kuja chini zina betri ndogo sana

Kwa mfano Google Pixel 4 ukubwa wa betri ni mAh 2800

Hii betri kiuhalisia haiwezi kudumu na chaji hata kwa masaa nane

Simu nyingi kwa sasa kufikisha masaa 12 ni jambo la kawaida

Kumbuka Google Pixel 4 inakaribia miaka 7 tangu itoke

Hivyo ubora hauwezi kuwa sawa kama awali

Hivyo kama bajeti yako ni chini ya laki tano walau unapaswa ununue Google Pixel 5

Nguvu ya utendaji

Google Pixel zilizotoka mwaka 2021 zina pafomansi kubwa sana

Pamoja na utendaji mkubwa hazitumii kiwango kikubwa cha chaji

Mwaka 2021 Google walianza kutumia prosesa wanazoziunda wao wenyewe

Prosesa hizo Zinaitwa Google Tensor

Zinaambatana na core aina ya Cortex X1 kwa ajili ya kazi zinazohitaji nguvu kubwa

Kwa kufipi kama unataka kuitumia simu kwa mambo mengi basi Google Pixel 6 kwenda mbele chaguo zuri zaidi

Na uzuri bajeti ya hizi simu zipo kati ya 500,000 hadi 600,000

Ukubwa wa RAM

Unajua katika kipindi cha miaka 2 iliyopita simu zinakuja na mifumo mingi ya AI

Mifumo ya AI inatumia sana RAM

RAM ikiwa ndogo baada ya muda simu inaanza kuwa nzito

Google Pixel 3, kwa mfano, ina kiasi cha RAM ya GB 4

Kwa sasa hiki ni kiwango kidogo

Wakati kuanzia Google Pixel 5  zinakuwekea RAM ya GB 8 na kuendelea

Zipo Google Pixel hadi za GB 12

Maboresho ya Software

Simu nzuri ni ile inayotunza thamani yake muda mrefu

Simu inayokupa nafasi ya kuweza kutumia teknolojia mpya kwa kupata toleo jipya la mfumo endeshi

Kuna baadhi ya simu za Google Pixel hazitopoeki tena toleo la android jipya

Kwa sasa Android mpya kabisa ni Android 16

Google Pixel 5 kwa mfano inapokea mwisho Android 14

Wakati huo Google Pixel 6 inapokea Android 16 na matoleo yatakayofuata

Matoleo mapya ya Android huasidia kuboresha pia usalama wa simu

Mifumo ya kamera

Simu za Google Pixel kabla 2020 zina machaguo machache ya aina ya kamera

Kwa mfano Google Pixel 4 ina kamera mbili tu haina kamera aina telephoto

Lakini Google Pixel 6 Pro inakuja na kamera tatu

Huku ikiwa na kamera ya ziada ya lenzi ya ultrawide

Kwa hiyo kwa mpenzi wa kamera hana budi kununua Google Pixel 6 Pro kwenda mbele

Ubora wa display(kioo)

Vioo vya simu miaka hii vya daraja kati vinatumia refresh rate ya 120Hz

Hii inafanya tachi kuwa nyepesi na muonekano mzuri unapo-scroll

Pia Google Pixel za zamani vioo havina muangaza mkubwa

Mara nyingi muangaza huwa ni chini ya nits 1000

Lakini vioo vya goole pixel 6 nits ni kubwa

Na kioo cha hdr10+ hivyo vitu vinaokana kwa kina kikubwa cha rangi

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

-google pixel 10 pro

Simu mpya za Google Pixel 10 na bei zake (ubora na sifa)

Mbabe wa kamera upande wa simu ametoa matoleo mapya Si mwingine bali ni Google Pixel 10 Google Pixel 10 unaweza kuiona kuwa haina tofauti na Pixel 9 Lakini haipo hivyo […]

infinix hot 60

Simu mpya za Infinix Hot 60 na bei zake

Infinix Hot 60 ni matoleo ya daraja kati yaliyoingia rasmi sokoni mnamo mwezi Julai 2025 Bei zake sio kubwa ni za wastani huku ukiwa na uhakika wa kupata mifumo mingi […]

sony xperia xz3

Simu za Sony Xperia za bei rahisi kwa Tanzania

Simu ya Sony iliyotoka mwaka huu 2025 ni Sony Xperia 1 VII Bei yake unaijua ni shilingi ngapi? ni milioni nne na  laki tano huko duniani Ni bei kubwa sana […]

pixel thumbnail

Simu za google pixel za bei rahisi zenye utendaji mzuri (2025)

Simu mpya za Google Pixel hupatikana kwa bei kubwa ambayo kwa Tanzania ni wachache wanayomudu Simu za google pixel hutengeneza simu za madaraja ya juu kama uonavyo iPhone Hivyo katika […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani
TUFUATE
Youtube Facebook Instagram twitter

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: 0756 077262 au 0683 420543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company