Hizi hapa ni orodha ya simu bora za bei zinazoanzia milioni mbili kwenda mbele
Ndizo simu janja zilizo kamili kwenye vipengele vingi
Hivyo ni simu bora duniani kwa mwaka 2025 japo na nyingine zipo (hizi ni baadhi)
Ukimiliki moja ya simu hizi utamiliki simu yenye nguvu, kamera kali na teknolojia mpya za kurahisisha kazi zako
Tuitazame kila simu kufahamu kiundani thamani ilizonazo
Samsung Galaxy S25 Ultra
Hii ni simu ya toleo la juu ambayo bei yake kwa Tanzania inafika milioni 4
Samsung Galaxy S25 Ultra inazipita simu zingine hasa upande wa kamera, software pia uwepo pen (stylus)
Kwa upande Galaxy S25 inapiga picha nzuri kuliko simu nyingi
Na utendaji wake ni mkubwa

Hii ni simu ya android inayotoa sapoti ya softwrae kwa kipindi cha muda mrefu
Ukiwa nayo, utakuwa unapokea matoleo mapya android kwa muda wa miaka 7
AI ni levo nyingine, ina mifumo ya kutafsiri lugha za sauti
Hivyo ukiwa unaongea na mtu asilewa lugha yako hii simu itatafsiri
iPhone 17 Pro Max
Bei ya iPhone 17 Pro Max kwa Tanzania ni shilingi milioni 4 pia
iPhone 17 Pro Max inajitofautisha na matoleo mingine hasa kiutendaji, ukaaji chaji, software na usalama
Hakuna simu yenye ufanisi mkubwa kwa sasa kama iPhone 17 Pro Max
iPhone 17 Pro Max inaweza kudumu na chaji hadi masaa 18 kwenye matumizi ya intaneti ya kawaida
Kucheza gemu muda wote simu inadumu hadi masaa 12

Kwenye utendaji, iPhone 17 Pro Max inatumia prosesa yenye nguvu kuliko zingine hadi sasa
Kwa bahati mbaya Apple hawajmasta vizuri upande wa AI
Wamekuwa nyuma mbele ya simu nyingi za Android
Vivo X300 Pro
Bei ya Vivo X300 Pro kwa Tanzania ni shilingi milioni 4.1
Vivo ipo kwenye orodha ya simu bora zaidi duniani 2025 kwa sababu hii
Ni simu yenye kamera kali kuliko simu nyingine
Unajua unaweza ukaigeuza hii simu kuwa profesheno kamera

Pia simu ina prosesa yenye nguvu sana, prosesa hiyo ni Mediatek dimensity 9500
Kwa miaka sita mfululizo, inapokea Android mpya
Kitu kinachotunza thamani ya simnu kwa muda mrefu
Xiaomi 17 Pro Max
Bei ya Xiaomi 17 Pro Max kwa Tanzania inaenda hadi shilingi milioni 3.3
Xiaomi 17 Pro Max ni moja ya simu bora duniani kwa sababu ya muudo wake wa kipekee
Pia ni moja ya simu yenye betri kubwa sana kuliko simu nyingi
Hivyo hii ndio simu inayokaa na chaji muda mrefu sana

Yaani kwenye matumizi ya inteneti ya kawaida betri inadumu hadi masaa 20
Pamoja na betri kwenye kucheza gemu inaachwa na iPhone 17 Pro Max
Muundo wake umeongeza display upande wa nyuma
Hii display inasaidia kupiga picha ya selfi kutumia kamera kuu
Oppo Find X9 Pro
Bei ya Oppo Find X9 Pro kwenye masoko ya dunia ni shilingi milioni 5.4
Hii simu ipo kwenye orodha ya simu kali duniani kwa sababu zifuatazo
Kwanza, kwenye hii orodha ndio simu inayoongoza kwa kukaa na chaji muda mrefu
Ni moja ya simu yenye utendaji mkubwa

Pia inapokea maboresho mapya ya Android kwa miaka mitano mfululizo
Kwenye ukaaji chaji simu inadumu hadi masaa 21 kwenye matumizi ya kawaida mfululizo
Ndio simu inayokaa na chaji masaa takribani 13 ukiwa unacheza gemu muda wote bila kupumzika
Kiujumla, Oppo Find X9 Pro ndio simu inayokaa na chaji zaidi duniani
Huawei Mate XTs Ultimate
Bei ya Huawei Mate XTs Ultimate kwa Tanzania ni shilingi milion 11
Ni simu yenye gharama kubwa kuliko zote zilzopo
Sababu kubwa ya uwepo wake kwenye orodha ni muundo wake wa kipekee

Vitu vingine mate xts ultimate inaachwa mbali sana na simu zingine kwenye orodha
Muundo wa hii simu umetengenezwa na uwepo skrini tatu kwenye simu moja
Yaani simu unaweza kuikunja mara mbili
Ama kuikunjua na kuwa pana
OnePlus 15
OnePlus 15 bei yake ni shilingi milioni 2.4
Ukiilinganisha na simu zingine zilizopo kwenye orodha kuna kitu utakiona
Ina vitu vingi vyenye kuendana ikiwemo utendaji mkubwa wenye nguvu
Sababu kubwa ya uwepo kwenye ni bei yake kuwa rafiki ukilinganisha na simu zingine bora duniani

Ina vitu vingi vinavyopatikana kwenye simu za gharama kubwa zaidi
Kwa hiyo kama bajeti inakaza sana OnePlus 15 inakupa mbadala
Sony Xperia 1 VII
Sony Xperia 1 VII inauzwa shilingi milioni 4 kwa hapa Tanzania
Kama unataka simu ya kamera kali sana Sony Xperia 1 VII ni chaguo mojawapo
Kwenye mazingira yote, mwanga hafifu na mwanga picha inatokea vizuri

Mbali na kamera simu ina utendaji mzuri
Na mfumo wake ni simpo sana hauna mambo mengi
Sony Xperia 1 VII itakuwa inapata maboresho mapya ya Android kwa miaka 4