Je unajua kuwa simu ya Infinix Hot 60 Pro inaiacha mbali Samsung Galaxy A16?
Wakati huo Infinix Hot 60 Pro bei yake iko chini ukilanganisha Samsung
Kwenye hii post utafahamu sifa za muhimu na bora zaidi za infinix hot 60 pro
Bila kusahau bei yake kwa hapa Tanzania
Bei ya Infinix Hot 60 Pro GB 128
Kwa hapa Tanzania, Infinix Hot 60 Pro ya GB 128 na RAM ya GB 8 bei yake ni laki nne (400,000)
Laki nne ni bei ndogo ukilinganisha sifa zake na matoleo kutoka kampuni zingine
Maana kwa sifa hizi simu nyingine bei huanzia laki nne na nusu
Kitu kizuri matoleo yote yanatumia RAM kubwa
Hivyo mifumo ya AI itakuwa inafanya kazi vizuri
Zitazame sifa kisha linganisha na Samsung utaona tofauti baina ya simu hizi mbili
Sifa za Infinix Hot 60 Pro
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | AMOLED, Refresh rate:144Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS 2.2, 128GB,256 na RAM 8GB |
Kamera | Kamera MBILI
|
Muundo | Urefu-6.78inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 400,000/= |
Uwezo wa network
Infinix Hot 40 Pro ni simu ya 4G inayosapoti laini mbili
Haitumii laini za eSIM bali laini za plastiki
Aina ya 4G simu inayosapoti ni LTE Cat 13
Hii uwezo wa juu wa kudownload ni 600Mbps
Ni kasi kubwa kama mtandao wa simu utakuwa na hiyo nguvu
Kwa sababu kufikia spidi ya 600Mbps inategemea na intaneti
Ubora wa kioo
Kioo cha Infinix Hot 60 Pro ni cha aina ya AMOLED
Refresh rate yake inafika kiwango cha juu cha 144Hz
Hii inasaidia skrini kuwa chapesi na mwitikio wa haraka
Kioo kina uangavu mkubwa unaifika nits 1600
Kwa maana hata ukiwa kwenye jua kali vitu vitaonekana vizuri
Nguvu ya processor Mediatek Helio G200
Processor ya Mediatek helio G200 ina uwezo wa wastani
Vitu kama magemu makubwa mfano wa Bus Simulator Indonesia haiwezi kucheza kwa frem(fps) nyingi bila kupata joto jingi
Na kuepuka kuganda ganda itakulazimu kupunguza ubora wa graphics (picha)
Kwa mujibu wa app ya Geekbench inayopima uwezo wa processor, Helio G200 ina alama 740
Hii inaishiria ni chip inayoweza kufanya vitu vingi kwa sehemu kubwa
Kiujumla ina sehemu mbili kwa ajili ya kufanya vitu vinavyohitaji nguvu
Uwezo wa betri na chaji
Ukubwa wa betri ya Infinix Hot 60 Pro ni mAh 5160
Na chaji ina kasi ya kupeleka umeme wa wati 45
Kiwango kinajaza simu kwa muda mfupi kwenye hii betri ya 5160
Kiwastani ndani ya dakika 65 simu inajaa kwa 100% kutoka sifuri
Na ukaaji wa chaji unachukuwa takribani masaa 14 kwa matumizi ya intaneti ya kuperuzi
Uimara wa bodi
Kioo cha hii simu kinalindwa na protekta ya glass kutoka kampuni ya Corning
Protekta hiyo Gorilla Glass 7i
Gorilla Glass 7i lengo kubwa ni kuilinda kioo cha simu pale inapondoka
Zingatia kioo kutopasuka inategemea uso wa eneo simu ilipondoka
Na pia kimo, Gorilla Glass 7i wanasema uwezo wa kuzuia madhara ni kimo chA MITA 2
Ukiondoa protekta simu ina waterproof ya kiwango cha IP64
ip64 inazuia maji ya kiwango cha kunyunyulizika na sio kwa kuizamisha
Ubora wa kamera
Simu ina kamera zipatazo mbili, ila kiuharisia ni kamera moja
Kamera ina megapixel 50
Kamera inapiga picha za ubora mzuri kwenye mazingira yenye mwanga wa kutosheleza
Ila kuna mazingira mng’ao wa kitu unakuwa mkubwa kuliko muonekano halisi
Kamera hii inarekodi video za fhd+ pamoja na kuwa na megapixel kubwa
Haina OIS(Optical Image Stabilization)
Ubora wa software
Simu inakuja na mfumo XOS 15 ikiwa inafanya kazi kwenye Android 15
XOS 15 inakupa mifumo mingi ya AI ambayo kwa kampuni zingine huweka kwenye simu za bei kubwa
Mfumo mmoja wapo ni wa kufupisha mada kwa kuipunguza maneno
Pia XOS 15 inakupa mfumo unaitwa circle to touch
Unasaidia kuchagua kitu kimoja kutoka kwenye picha na kutafuta taarifa zake google
Hakuna taarifa kama Infinix Hot 60 Pro itapata android 16 na matoleo yanayofuata
Hapa ndipo Samsung Galaxy A16 inapoizidi Infinix Hot 60 Pro
Washindani wa Infinix Hot 60 Pro
Kwa bei yake, mshindani mkubwa wa hot 60 pro ni Infinix Hot 50 Pro
Ukizitazama sifa za simu hizi mbili huwezi kuona tofauti
Vitu vinavyotofautiana ni viwili ambavyo ni betri na chaji
Infinix Hot 50 Pro kwa sasa bei yake ni ndogo
Hii inamaanisha mtumiaji wa Infinix Hot 50 Pro anaweza asishawishike kuchukua infinix mpya
Lakini pia usisahau Samsung Galaxy A16 ambayo itatoa matoleo mapya ya Android kwa miaka sita mfululizo
Neno la mwisho
Kwa mwaka 2025, Infinix Hot 60 Pro ni moja ya simu bora za daraja la kati
Inakupa radha ya simu za daraja juu kwa bei rafiki
Uwepo wa IP64 na skrini protekta gorilla 7i inaimarisha simu
Ila upande wa kamera na software hapavutii sana hapa maboresho ya Android
Maoni 4 kuhusu “Bei ya Infinix Hot 60 Pro na sifa zake muhimu”
Ni simu nzuri sana je hio Infinix hot 60 mAh 5160 je ni bei gani
260k
Nimeipenda kwakweli ni simu nzuri sana
Je iyo infinix hot 60 ya gb256
Ni shingapi