SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Simu za Sony Xperia za bei rahisi kwa Tanzania

Bei Nafuu

Sihaba Mikole

May 17, 2025

Simu ya Sony iliyotoka mwaka huu 2025 ni Sony Xperia 1 VII

Bei yake unaijua ni shilingi ngapi? ni milioni nne na  laki tano huko duniani

Ni bei kubwa sana na simu nyingi za sony zinauzwa kwa bei za viwango hivyo

Kwenye hii post utazioana simu za sony xperia za bei rahisi ambazo wengi wanaweza kuzimudu

Hata hivyo simu zote ni za zamani hivyo utapata ikiwa imeshatumika (sawa na kubeti)

Hizi ndizo simu zenyewe za sony

Sony Xperia 5

Bei ya Sony Xperia 5 ni shilingi 320,000 (laki tatu)

Utendaji wake ni wa wastani na baadhi ya simu mpya za matoleo ya kati zinapittwa na xperia 5

Simu hii ina kamera tatu na zinatoa picha nzuri na inaweza kurekodi video za 4K

sony xperia 5

Ni nadra kupata simu ya laki tatu yenye kamera ya 4K kwa sasa, ila hii ni ilitoka 2019

Upande wa software, simu inapata mpaka toleo la android 11 wakati kwa sasa kuna android 14

Kikubwa zaidi kuhusu hii simu ina kioo cha oled, na waterproof aina ya IP68

Sony Xperia L4

Sony Xperia L4 inauzwa shilingi 300,000 kwa ya GB 64

Ilitoka rasmi mwaka 2020

Haina utendaji mkubwa ukilinganisha na simu Sony Xperia 5

Kwa sababu processor yake ya Helio P22 haiwezi kusukuma vitu vingi vikubwa

xperia l4

Ndio maana hata kamera zake zinaweza kurekodi video za full hd kwa kiwango cha 30fps

Betri yake sio kubwa sana ina mAh 3580, kwa sasa betri nyingi zina ukubwa wa mAh 5000

Simu haina uwezo wa kupata android nyingine mbali na ile inayokuja nayo ambayo ni Android 9 (Pie)

Sony Xperia 5 II

Sony Xperia 5 II ni simu ya mwaka 2020, ila ina vitu vingi ambavyo vyenye hadhi hata kwa sasa

Cha ajabu, bei yake ni shilingi laki tatu na themanini (350,000)

Sifa zake nzuri ni hizi, kioo chake ni cha oled chenye refresh rate ya 120hz

Kamera zinapiga picha zenye muonekano mzuri hata kwenye mazingira yenye mwanga hafifu

xperia 5 ii

Na zinaweza kurekodi video za 4K kwa kiwango cha 120fps

Hiki ni kitu kisichopatikana hata kwa simu za madaraja ya kati kama Samsung Galaxy A36

Changamoto ni kuwa inapokea toleo la android 12 pekee

Na betri yake ina mAh 4000 ambayo ni ndogo kwa viwango vya sasa

Sony Xperia 10 III Lite

Sony Xperia 10 III Lite ni simu ya mwaka 2021, ina miaka minne tangu itoke

Bei yake kwa Tanzania inapatikana kwa kiasi cha shilingi laki nne (400,000)

Ni simu ya kamera tatu yenye utendaji wa wastani

xperia 10 iii

Kwani inatumia chip ya Snapdragon 695 5G

Tukirudi upande wa kamera, kamera zake zinaweza kurekodi mpaka video za 4K kwa kiwango cha 30fps

Betri yake ni kubwa kidogo ina mAh 4500

Inaweza kupata hadi Android 13

Sony Xperia 1 III

Kwenye hii orodha ya sony za bei rahisi hii ndio ina bei kubwa

Lakini ndio sony experia yenye uwezo mkubwa na ilitoka 2021

Utendaji mkubwa unachabgiwa na utumiaji wa processor ya Snapdragon 888 5G

Sony Xperia 1 III inauzwa shilingi laki saba (700,000) na imekamilika kila idara

xperia 1 iii

Mfano upande wa kamera, kuna kamera tatu aina ya wide, telephoto na ultrawide

Kamera zote zina mfumo wa ulengaji wa kiutomaki wa dual pixel pdaf

Kutokana na nguvu kubwa kamera yake inaweza kurekodi video za 4k kwa kiwango cha 120fps

Chaji yake ina ukubwa wa mAh 4500 na chaji ya wati 30, na kioo chake ni cha oled

Ila hii Sony Xperia 1 III inapata mwisho toleo la Android 13

Sony Xperia XZ3

Bei ya Sony Xperia XZ3 ni shilingi laki mbili na nusu (250,000)

Ni simu ya kitambo sana tangu mwaka 2018, yaani ina miaka saba (7) tangu itoke

Na kwa bahati mbaya haipokei sapoti yoyote toka kwa sony

sony xperia xz3

Ila sasa ni simu yenye kioo cha Oled na utendaji wa wastani

Ni simu yenye kamera moja yenye uwezo wa kurekodi video za 4K kwa kiwango cha fremu 30fps

Betri yake sio kubwa ina mAh 3300

Hitimisho

Sifa za sony zilizoorodheshwa zinazifanya kuwa simu shindani hata kwa wakati uliopo

Ukitazama simu zinazouzwa chini ya laki tano zina sifa chache sana nzuri ukilinganisha na hizi sony

Kwa kuwa ni simu za zamani kuna uwezekano ukaipata ikawa ina baadhi ya changamoto hasa za betri

Kikubwa ni kuwa makini wakati ukinunua popote pale duniani

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

pixel thumbnail

Simu za google pixel za bei rahisi zenye utendaji mzuri (2025)

Simu mpya za Google Pixel hupatikana kwa bei kubwa ambayo kwa Tanzania ni wachache wanayomudu Simu za google pixel hutengeneza simu za madaraja ya juu kama uonavyo iPhone Hivyo katika […]

bei ndogo

Simu za laki tatu zenye ubora wa kuridhisha kwa 2025

Iwapo unapanga kununua simu chini ya laki tatu au zisizozidi laki nne usitarajie kupata simu yenye ubora mkubwa Kwa maana usitarajie kamera kali na utendaji mkubwa Ila kwenye hii post […]

iphone 16 pro

Kampuni bora za Simu duniani (2024/2025)

Pamoja na uwepo wa makampuni zaidi ya 100 ya kutengeneza simu bado kampuni zilezile zimeendelea kushika soko kwa sehemu kubwa duniani, kampuni hizo ni apple, samsung na xiaomi na nyinginezo. […]

samsung a06

[VIDEO]-ubora wa picha na kiutendaji wa Samsung Galaxy A06

Hii ni video inayokupa nafasi kushuhudia sifa za ziada za samsung galaxy a06 hasa upande wa kamera Kama hujui, Galaxy A06 NI simu mpya ya daraja la chini ambayo imetoka […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani
TUFUATE
Youtube Facebook Instagram twitter

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: 0756 077262 au 0683 420543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company