Mpaka kufikia 2025, kampuni za simujanja zimetoa matoleo mengi ya daraja la kati
Wanaotaka kununua simu za daraja la kati wana machaguo mengi ya kuchagua
Moja ya simu mpya za madaraja hayo ni Samsung Galaxy A26 na Samsung Galaxy A36
Ni simu zilizotoka mwezi machi 2025 na bei zake ni 650,000 na 850,000
Hapa, kwa ufupi, tutaangalia ubora katika vipengele vya
- Kamera
- Software
- Ukaaji wa chaji
- Utendaji
Samsung Galaxy A26
Simu inakuja katika matoleo manne ikiwa na mgawanyiko wa ukubwa GB 128 na GB 256
Upande wa RAM unaweza kuta ya GB 6, 4 AU 8
Urefu na upana ni inchi 6.7 na simu ya 5G
Software
Samsung Galaxy A26 inatumia mfumo endeshi wa Android 15 na One UI 7
Itakuwa inapokea matoleo mapya ya Android kwa kipindi cha miaka 6
Ni mageuzi makubwa maana zamani Samsung walikuwa wanatoa update miaka michache
Hivyo mfumo endeshi mpya unampa nafasi mtumiaji kupata vitu vipya
Na kuipa simu thamani muda mrefu hata pale utakapotaka kuuza
Kamera
Simu ina kamera tatu ambazo ni aina ya wide, ultrawide na macro
Kamera kubwa ina megapixel 50 ikiwa na OIS
Inaweza kurekodi video za 4K ambazo huwa na mng’ao mkubwa wa picha
Ila kamera ya mbele ukubwa wake ni megapixel 13 tu
Na inaweza kurekodi video za full hd pekee
Ukaaji wa chaji
Betri ya Samsung Galaxy A26 ina ukubwa wa mAh 5000
Na katika matumizi ya kawaida simu inaweza kukaa na chaji kwa msaaa karibu 11
Kwenye uchezaji magemu mara kwa mara inaweza kustahimili kukaa na chaji masaa karibu nane
Kwa maana hiyo wastani wa ukaaji wa chaji sio mbaya
Utendaji
Nguvu ya utendaji ni ya wastani na inaweza kufanya mambo pasipo tatizo
Hii inatokana simu kutumia processor ya Exynos 1380
Ambapo core yenye nguvu sana zimeundwa kwa muundo wa Cortex A78
Na zipo core mbili kwa ajili ya kazi zinazohitaji nguvu kubwa
Samsung Galaxy A36
Samsung Galaxy A36 inakuja na ukubwa wa GB 128 au GB 256
Na upande wa RAM zipo za matoleo ya GB 6, 8 na 12
Kwa picha ya haraka Galaxy A36 ubora wake uko mbele ya Galaxy A26
Software
Inatumia Android 15 na itapata maboresho ya Android mpya kwa miaka sita(6)
Yaani utapata hadi Android 21
Kwa maana kwa changamoto zitakazohusiana na mfumo endeshi, simu itapata marekebisho
Kamera
Upande wa kamera, kuna kamera tatu za wide, ultrawide na macro
Hapa hakuna tofauti na Samsung Galaxy A26
Na pia inarekodi video za 4K kwa kiwango cha 30fps
Na kamera ya mbele ya self ina megapixel 12 inayoweza kurekodi video za full hd pekee
Ukaaji wa chaji
Katika matumizi ya kawaida BETRI yake ya ukubwa wa 5000mAh inaweza kukaa na chaji mpaka masaa 12
Kwenye kucheza gemu simu inachukua masaa saba mapaka chaji kuisha ukiwa unarekodi muda wote
Na inasapoti chaji ya wati mpaka 25
Hivyo kuwahi kujaa kwa muda mfupi ni swala la kawaida
Utendaji
Hii simu inatumia processor ya Snapdragon 6 Gen 3
Kimuundo inaendana na Exynos 1380 maana zote zinatumia muundo wa Cortex A78
Lakini utendaji wa Snapdragon ni mkubwa kwa kiasi fulani
Na hivyo inaweza kufanya vitu na kwa matumizi ya umeme kidogo