Kuelekea mwishoni mwa mwaka Infinix imekuja na matoleo ya simu za Infinix Hot
Hii post imeorosheshwa kwa ufupi simu 4 za infinix hot, moja ya infinix smart na ya zero flip
Kwenye kila simu utajua sifa za muhimu zaidi kwa kila simu
Simu mpya matoleo ya Infinix hot
Zifuatazo ni sifa za kila simu ambazo ni muhimu ili ujue ipi inakidhi sifa unazozihitaji
Infinix Hot 50 Pro+
Bei ya Infinix Hot 50 Pro+: 510,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM: 8GB
Infinix hot 50 Pro+ inakuja na kamera tatu ila kamera moja ndio maalum kwa kupiga
Kamera kubwa ina megapixel 50 na inaweza kurekodi video za full hd+
Nguvu ya utendaji ni ya wastani kwa sababu inatumia processor ya Mediatek helio g100
Inatumoia mfumo endeshi wa android 14 na inatarajiwa kupata toleo jipya la android 15 baada ya hapo haitopekea mfumo endeshi mwingine
Kioo chake ni cha aina ya amoled na betri yake ina ukubwa wa 5000mAh huku simu ikisapoti chaji yenye kasi ya wati 33 ambayo haichukui muda kujaza hii betri kubwa
Infinix Hot 50i
Bei ya Infinix Hot 50i: 310,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM: 4GB
Infinix Hot 50i ni simu ya daraja la chini, ina vitu vichache vizuri ukilinganisha na Infinix hot 50 pro+
Ina kamera moja yenye ukubwa wa megapixel 48 inayoweza kurekodi video za full hd pekee
Utendaji wake sio mkubwa kutokana na kutumia processor ya mediatek helio g81
Skrini yake sio ya amoled bali ni IPS LCD yenye resolution ndogo
Betri yake ni kubwa ila kasi ya chaji ni ndogo
Kwani chaji yake inasapoti wati 18 ambayo huchukua masaa hata matatu mpaka kujaa
Hii simu inatumia Android 14 na haijaainishwa kama itapata Android 15
Infinix Hot 50 4G
Bei ya Infinix Hot 50 : /= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM: 6GB
Infinix Hot 50 4G haina tofauti sana na infinix hot 50 pro
Utofauti mkubwa upo kwenye aina ya skrini na kasi ya kuchaji simu
Kioo cha Infinix hot 50 4G kina resolution kubwa ila ni cha aina IPS LCD
Kumbuka vioo vya amoled huwa ni bora zaidi kuliko vioo vya IPS LCD
Pia kasi yake ya juu ya kuchaji ni wati 18 hivyo betri itachukua muda kidogo kujaa
Infinix Smart 9
Bei ya Infinix Smart 9: 330,000/= ,Ukubwa wa Memori: 64GB, RAM: 4GB
Infinix smart 9 haina tofauti kubwa na toloeo la infinix hot 50i
Ila smart 9 inazidiwa ubora upande wa kamera, kasi ya chaji na aina ya mfumo endeshi
Smart 9 ina kamera moja tu yenye ukubwa wa megapixel 13 na inaweza kurekodi video za full hd pekee
Inatumia Android 14 aina ya Go Edition
Go Edition ni android inayolenga simu zenye kiwango kidogo cha RAM ambapo smart 9 ina mpaka matoleo ya ram za 3gb
Ina kasi ndogo ya kuchaji kwani chaji yake inapeleka umeme wa wati 10 kama kiwango cha juu
Infinix Zero Flip
Bei ya Infinix Flip: 2,000,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM: 8GB
Katika orodha ya simu zilizotoka kwenye ngwe ya mwisho ya mwaka 2024, inifinix zero flip ndio toleo bora zaidi
Kwanza inatumia processor yenye uwezo wa kufanya kazi kubwa bila tatizo
Processor hiyo ni mediatek dimensity 8020
Ina kamera mbili zote zikiwa na megapixel 50 na zinaweza kurekodi video za 4K hata selfie kamera
Betri yake ina ukubwa wa 4700mAh na inasapoti chaji ya wati 70
Chaji ya wati 70 inaweza jaza simu ndani ya dakika 30 kwa asilimia mia
Uzuri simu itakuwa inapokea matoleo ya android kwa kipindi cha miaka miwili
Yaani hii inamaanisha simu itapata hadi Android 16