Matoleo ya simu yamekuwa yakitoka mara kwa mara yakiwemo yenye bei kubwa na zinazotamaniwa na watu wengi
Aina hizi ya simu huvutia watu wasio waaminifu kutengeneza simu feki zenye ufanano na origino
Kiasi cha kwamba inakuwa ni ngumu kujua simu origino ni zipi na zipi ni feki
Kwa kifupi ni kuwa, simu origino ni zile simu zinafanana kwa 100% na sifa zilizoainishwa na mzalishaji halisi wa simu husika
Ukiona baadhi ya sifa hazifanani hata kama ni moja basi jua simu unayotakaka kununua sio orijino
Mara nyingi wahanga simu feki ni iPhone na Samsung za bei kubwa,
Swali ni kuwa unatumbuaje na kutofautisha simu feki na orijino.
Fanya yafuatayo kabla ya kununua.
Chunguza Muundo wa bodi ya simu
Kitu cha kwanza kabla ya kununua simu tazama video na fuatilia makala mbalimbali zinazofafanua sifa za simu unayotaka kununua
Tovuti ya simunzuri.com ni sehemu moja wapo kuzijua sifa za simu janja
Kwa maana angalia kwa umakini muundo wa skrini, aina ya bodi na pia muundo wa kamera nyuma na mbele
Watengenezaji wa simu feki hupata shida kunakiri kwa usahihi muundo wa simu orijino
Kwa mfano hii picha ya chini ni muonekano wa samsung galaxy s22 ultra origino na ile ambayo ile sio orijino
Samsung orijino kioo chake kimepinda kwenda wakati hii feki kioo kipo flat na upande wa juu hakijapinda kwenda
Waliotengeneza samsung s22 wamekutana na ugumu wa kupata kioo chenye muundo huu
Hivyo kwa macho unaweza kuitambua simu ambayo ni orijino ila lazima uifuatilie simu kiundani hasa kwa kutazama video na picha kabla ya kununua ndio utaweza kuzifananisha kama zinaendana.
Fuatilia aina ya Processor ya simu
Simu feki huwa hazitumii processor(cpu) zilizopo kwenye simu orijino
Mara nyingi cpu za kwenye simu orijino huwa zina gharama kubwa kitu kinachowapa ugumu kuziweka
Tuchukulie mfano wa simu ya iPhone 13 Pro Max
Processor yake inaitwa Apple A15 Bionic kama umefuatilia sifa zake hii ni moja ya taarifa inayowekwa
Simu ambayo ni feki haiwezi kutumia kutumia hii chip
Ukidownload app zinazocheki vitu vilivyopo kwenye simu utaona vitu vipo tofauti na sifa za simu husika
Hii ni picha ya iphone 13 pro max ambayo ni feki,
Kwenye upande wa CPU app inaonyesha Mediatek Qualcomm Snapdragon 888 plus kitu ambacho hakipo na ni tofauti na cpu ya iphone 13
Hapo ilipaswa isome Apple A15 Bionic
App ya CPU-Z inaweza ikakujulisha taarifa za simu lakini sio ya uhakika kwa sababu haina uwezo wa kujua kama taarifa inazozitoa simu ni feki
Kwenye hii simu CPU-Z inaonyesha memori ya simu feki kuwa ni GB 250 na RAM ya GB 8
Ila baada ya kutazamwa kiundani kwa kutumia kompyuta kwa software ya Android Studio, simu ilionekana kuwa na GB 8 na RAM ya GB 1
App nzuri kwa kiasi fulani ni kingroot na CPU X kwa ajili ya kucheki taarifa za simu
Cheki mfumo Endeshi wa simu(Operating System)
Kwenye sifa za simu yoyote kitu cha kwanza kinachoainishwa ni aina ya mfumo unaotumiwa na simu husika
Taarifa hizi unaweza kuzipata kwenye tovuti rasmi ya kampuni inayounda simu au mitandao kama gsmarena, simunzuri ni kwingineko
Kama kampuni inasema kuwa mfumo endeshi ni Android 13 na One UI 5, basi kwenye about phone inapaswa ionekane hivyo
Ila hapa umakini ni muhimu.
Kwa sababu kuna simu feki huwekewa theme zenye muonekano wa kama wa simu origino kiasi cha kwamba unaweza usitambue
Kwa kuwa una app kama CPU X au kingroot ni rahisi kutumbua kama sifa za simu zinaendana na simu orijino
Chunguza IMEI number
Kila kifaa cha mawasiliano huwa na imei namba yake ya kipekee inayotofautiana na nyingine
Kuna tovuti na app nyingi unazoweza kutumia kuangalia iwapo imei inaonyesha simu husika
Hata hivyo kutumia imei number sio njia nzuri kwa sababu kuna apps zinaweza kubadilisha
Kama ukibonyeza *#06# kuangalia imei itakuonyesha imei iliyobadirishwa
Lakini ni njia nzuri ya kuanzia
Kuna tovuti zinaweza kukusaidia kuonyesha imei, moja wapo ni imei check
Hii inakuruhusu kuingiza tarakimu 15 utakazozipata baada ya kupiga *#06#
Taarifa itakazorudisha zinapaswa ziendane na sifa za simu yako
Ikiwa ni tofauti jua kuwa hiyo sio simu origino
Kumbuka hii sio njia kwa sababu IMEI hubadirishwa
Hitimisho
Hizi ni njia chache za kuweza kujua simu origino ni zipi
Kuna njia nyingi zinazochimba kiundani
Unapoenda kununua simu fanya settings pale pale dukani na halafu download app ya CPU X au Kingroot
Kwenye CPU X bonyeza CPU utaona jina la cpu na aina za core zilizotumika
Kisha tafuta taarifa za simu yako kuhusu processor CPU ukiona tofauti fahamu kuwa ni feki na uirudishe kwa muuzaji
Maoni 3 kuhusu “Simu Origino ni Zipi na Unazitambuaje? (Hatua za kufuata)”
Je, kati ya pixel 8 pro na S23 Ultra ipi ni bora zaidi?
S23 ultra bila shaka
S23 iko powa