SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Bei ya infinix hot 8 na Sifa Zake 2023

Bei Nafuu

Sihaba Mikole

May 18, 2023

Infinix Hot 8 kwa sasa imekuwa simu ya kitambo kwa sababu ilitoka mwaka 2019

Kutokana na kutoka muda mrefu, simu inauzwa kwa bei ndogo sana hivyo ni nafuu kwa wenye kiasi kidogo cha pesa

Kwani bei ya sasa ya infinix hot 8 haizidi laki mbili ni chini ya hapo

Kutokana na kutoka kwa matoleo ya Hot 30 na Hot 12 inafaa ujiulize kama hot 8 inakufaa kwa mwaka 2023 na kuendelea

Utafanya maamuzi mazuri kama utafuatilia sifa zake zote muhimu zilizopo hapa

Bei ya Infinix Hot 8 ya GB 32

Hot 8 yenye GB 32 na RAM GB 2 inapatikana kwa kima cha shilingi 150,000/= hapa Tanzania

Kwa ambazo zimetumika inaweza kupatikana chini ya hapo pia

Sababu kubwa ya bei ndogo kwanza ni kiwango cha memori ambacho kwa anaetumia sana whatsapp kitakuja kuwa kidogo

Na pia utendaji wake sio mkubwa kwani inazidiwa na infinix hot 10

Kuna machache mazuri yanayoshawishi kuimiliki hii simu kwa nyakati za sasa

Sifa za Infinix Hot 8

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
  • CPU – Mediatek Helio A22
  • Core Zenye nguvu(-) –
  • Core Za kawaida(4) – 4×2.0GHz Cortex
  • GPU-PowerVR GE8320
Display(Kioo) IPS LCD
Softawre
  • Android 9
  • XOS 5
Memori eMMC 5.1, 64GB,32GB na RAM 2GB,4GB
Kamera Kamera tatu

  1. 13MP,PDAF(wide)
  2. 2MP(depth)
  3. QVGA
Muundo Urefu-6.52inchi
Chaji na Betri
  • 5000mAh-Li-Po
  • Chaji-
Bei ya simu(TSH) 150,000/=

Upi Ubora wa simu ya Infinix Hot 8

Ni simu ya bei ndogo ambayo ina 4g ndani yake

Inakaa na chaji masaa mengi kwa sababu ina betri kubwa na ina matumizi madogo ya chaji

Ni ndevu hivyo kwa wapenzi wa simu ndefu wanaweza kupata kwa kiwango kidogo

Mengineyo kiuhalisia ni ya kawaida ikizingatiwa ni simu ya daraja la chini

Uwezo wa Network

Infinix Hot 8 inasapoti mtandao mpaka wa 4G

Aina ya 4G inayotumia ni LTE Cat 7 ambayo kasi yake ya juu ya kudownload ni 300Mbps

Kwa kulinganisha uwezo wa network na simu ya Tecno Spark 10 Pro hii ni kasi ndogo

Pamoja na hivyo kwa Tanzania ni nadra kupata mtndao wa 4G inayofika kasi hiyo

Kasi hii kwa hapa kwetu utaipata kwa mtandao wa 5G

Ina masafa karibu yote yanayotumika na mitandao ya simu nchini

Hivyo basi karibu laini zote zitaweza kufanya kazi vizuri

Ubora wa kioo cha Infinix Hot 8

Kioo cha hii simu ni aina ya IPS LCD ambacho kina resolution ndogo

Resolution yake ni 720 x 1600 pixels

Hii inafanya vitu kutoonekana kwa ubora mkubwa sana kama simu zinazotumia vioo vya amoled

Muonekano ungeamilika kama resolution yake ingekuwa ni full hd

Kiwango cha refresh rate ni cha kawaida na pia inakosa vitu vingine vya muhimu

Hata hivyo zingatia kuwa gharama ya simu ni ndogo usitarajie kuwa na sifa kubwa kama iPhone 14 Pro Max

Nguvu ya processor MediaTek Helio A22

Infinix hot 8 inatumia chip ya mediatek helio a22 ambayo ni ya daraja la chini

Inaundwa kwa core zenye nguvu ndogo aina ya Cortex A53 zipatazo nne

Hii inamaanisha kuwa Hot 8 sio simu nzuri kwa mpenzi wa magemu

Core aina ya Cortex A53 huwa ni kwa ajili ya kazi zinazotumia nguvu ndogo

Ndio maana simu nyingi siku hizi huchanganya sehemu yenye nguvu kubwa na ndogo

Ila hii chip haina

Kuwepo kwa muundo huu pekee yake kutakusaidia kuitumia simu masaa mengi ila utakumbana na ugumu pale unapofungua vitu vingi kwa wakati mmoja au kucheza magemu makubwa

Uwezo wa betri na chaji

Simu inakuja na betri ya ukubwa wa 5000mAh

Kiwango cha betri ni kikubwa na ukizingatia hot 8 inatumia processor yenye nguvu ndogo

Betri za 5000mAh zinaweza kukaa na chaji kwa masaa zaidi ya 14 ukiwa unatumia intaneti muda wote

Hivyo na infinix hii ipo hivyo

Changamoto utakayoipata ni kuwa mfumo wake wa chaji hauna fasti chaji

Hivyo betri inachukua muda mrefu kujaa kwani ni kubwa na chaji inapeleka taratibu

Ukubwa na aina ya memori

Infinix Hot 8 inakuja na matoleo mawili kwa upande wa memori

Ipo ya GB 32 na GB 64 na RAM ya 2GB au 4GB

Aina ya memori memori simu inayokuja nayo eMMC 5.1 ambayo huwa na kasi ndogo ya usafirishaji

Kwa maana kadri vitu vinavyokuwa vingi simu inaweza kuwa nzito

Ni tofauti ni mfumo wa memori wa UFS ambayo kasi yake ni kubwa

Ni vizuri ukachukua ya GB 64 ili uweze kujaza mafaili mengi

Kwani siku hizi GB chini ya hapo itaifanya simu kuwahi kujaa nafasi

Uimara wa bodi ya Infinix Hot 8

Bodi ya Infinix Hot 8 imeundwa kwa bodi ya plastiki upande wa nyuma na pembeni

Haina viwango vya IP ambavyo huashiria uwezo simu kuzia maji kupenya

Hivyo si simu imara inapozama ndani ya maji

Inakulazimu kuwa makini sana unapotumia hii simu

Pia ni vizuri kutumia kava ili rangi isiwahi kuchunika kwa haraka

Kwa sababu bodi za plastiki kama sio mtumzaji zinawahi chakaa

Ubora wa kamera

Simu ina jumla ya kamera zipatazo tatu ila kamera moja ndio yenye ubora kiasi

Ambayo kamera hiyo ina megapixel 13 na inatumia ulengaji wa PDAF.

Kamera nyingine ni depth, hii sio kwa ajili ya upigaji na haina umuhimu kwa sasa kutokana na teknolojia ya kamera kukua

Kiujumla mfumo wa kamera wa simu sio wa kuvutia na unakosa vitu vya msingi vingi

Upande wa video simu inaweza kurekodi mpaka video za full hd pekee

Kwani processor haiwezi kuchakata video za 4K

Ubora wa Software

Simu inakuja na android 9

Na haiwezi kupokea toleo la mbele ikiwemo Android 13

Bado utaweza kutumia app zote muhimu

Hakuna app itakayokwama kutumika kwenye android 9

Na pia inakuja na mfumo wa XOS 5 ambapo kwa sasa infinix ipo kwenye XOS 8

Washindani wa Infinix Hot 8

Kutokana na sifa zake nyingi kuwa na kiwango cha kawaida kama sio cha chini simu haifahi kulinganishwa na matoleo ya hivi karibuni

Hivyo washindani wake wanafaa kuwa simu zote zinazotumia chip ya Helio A22

Hivyo washindani sahihi ni Huawei Y6 Pro, Infinix Smart 7, Tecno Spark Go 2023, Xiaomi Redmi A1 na NOKIA 2.3

Ila simu zote hizo zinaendana sifa, mfano Tecno Spark Go 2023 ya mwaka huu ina mfanano wa kila kitu ila ina chaji yenye kasi kiasi fulani

Hivyo kama unataka toleo la bei nafuu jipya basi tecno inaweza ikawa chaguo zuri

Neno la Mwisho

Infinix Hot 8 kwa sasa nyakati zake zimeshaisha, itumie kama bajeti ya kununua simu ni ndogo

Uwezo wake kiutendaji na vitu watu wanavyovitaka siku hizi haviendani

Sio mbaya ukawa mvumilivu kwa kujichangachanga kutunisha mfuko na kisha ununue simu yenye maboresho zaidi

Maoni 11 kuhusu “Bei ya infinix hot 8 na Sifa Zake 2023

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

samsung a06

[VIDEO]-ubora wa picha na kiutendaji wa Samsung Galaxy A06

Hii ni video inayokupa nafasi kushuhudia sifa za ziada za samsung galaxy a06 hasa upande wa kamera Kama hujui, Galaxy A06 NI simu mpya ya daraja la chini ambayo imetoka […]

No Featured Image

Bei ya Samsung Galaxy A06 na Ubora wake

Samsung Galaxy A06 ina betri inayokaa na chaji muda mrefu na ni simu ya daraja la chini Hii inamaanisha watu wengi kwa hapa Tanzania wanaweza inunua Kwa sababu bei ya […]

No Featured Image

Bei ya Tecno Spark 30C na Sifa Zake Muhimu

Tecno wameleta toleo jipya la simu ya madaraja ya chini yenye maboresho Ina maboresho upande wa skrini(kioo) kuwa na refresh rate kubwa ambayo mara hupatikana kwenye simu za daraja la […]

thumbnail

[VIDEO]:Simu zote za iPhone za bei ndogo na zinazofaa

Kabla ya kununua iphone za bei rahisi ambazo mara nyingi huwa ni used, kitu cha kwanza cha kuangalia ni kama itakuwa inapata sapoti ya kupokea mfumo endeshi wa iOS Tofauti […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani
TUFUATE
Youtube Facebook Instagram twitter

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: 0756 077262 au 0683 420543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company